Kiumeni.com tunachokuambia sio sura yako au swaga zako ndo zitakazo
mfanya msichana akupende Zaidi ya yeye atakavyo, ila ni kwa jinsi wewe
unavyomfanya ajisikie akiwa nawe, jinsi anavyojihisi na kupokea upendo
unaotoka moyoni kwake na kuukubali, ndicho kitu kikuu kitakacho mfanya
mpenzi wako apagawe nawe na kujikuta akikupenda kupitiliza.
Hakikisha kila mda unaotumia nae unamtengenezea kumbukumbu nzuri,
afurahie vitendo mnavyofanya pamoja na kutengeneza historia yenu wawili,
kumbukumbu zinazomburudisha moyo wake kiasi hata ukiwa mbali na
akazifikilia, zinamfanya atabasamu na hisia za kukumisi kumjaa mara
dufu, hizo hisia za kumtaka awe tena karibu yako zimfanye asiache
kukutafuta kwenye simu na kukutumia meseji.
Mfanye ajione tofauti, ajihisi unamwona spesho na sio kwa sifa unazompa
ila kwa jinsi unavyomchukulia, aone kwa vitendo, aamini kwa macho yake
mwenyewe, hii itamfanya akupende bila kujihisi, afanye vitu kwa jinsi
mapenzi yanavyompeleka yeyewe, ajitoe kwa moyo na kukuona kuwa nawe ni
bahati hivyo atajikuta anaitumia hio bahati kwa marefu na mapana, huku
akiwa ajiulizi wala kujishuku.
Iwapo ukimwondolea hii hofu na kujikutaanakuamini kutamfanya akupende bila mipaka, bila mashaka na kukolea kwenyemapenzi Zaidi na Zaidi na Zaidi.
No comments:
Post a Comment