Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Saturday, March 24, 2018

Changamoto za kiuchumi zinayumbisha penzi langu

Salam wanajamvi, vipi habari yenu hii?

Natumai mko salama kabisa, kuna tatizo ambalo limenichukua muda mrefu sana mpaka kufika kuweza kuliwasilisha kwenu ni kwa maana limekuwa ni tatizo sugu katika mahusiano yangu.

Ni kwamba takribani miezi saba nyuma nilifanikiwa kuanza nae mahusiano ijapokuwa yeye ni mjane wa watoto wa 3, ila ni mzuri kuliko binti bikra kimuonekano na pia kitabia ila mimi hapo nyuma nilikuwa vyema kiuchumi sababu nilikuwa kazini but nilipofanikiwa kupata nafasi ya kuendelea na elimu ya juu, kazini ikanibidi niache kutokana ni sekta binafsi.

Sasa tatizo kumuhudumia kwangu, kwasasa hivi si sawa na hapo nyuma, ijapokuwa namuhudumia kama kidume kweli, kweli mawasiliano yangu pia ni ya nadra kwa siku mara 2 au 1 lakini kwa siku lazima niwasiliane nae but huwa ana complaints mara nyingi mpaka ikafikia wakati akahitaji kubreak mahusiano yetu, lakini kwasasa nina chanzo kimoja cha mapato ambacho nilifanikiwa kujijenga nilipokuwa kazini kinaniwezesha kupata si chini ya lak 4 kwa wik 5 au 6.

But kinachoniumiza zaidi ni kwamba watoto wote wako shule za Englsh medium, hapo nyuma nilikuwa nahudumia kumpa pesa yeyote aitakayo akiniomba na hata akinidanganya nilikuwa simuhoji sana ila kwasasa tatizo lililopo ni kwamba anahitaji fedha za watoto wawili hao kwenye swala la ada na mimi chanzo changu cha mapato akisapoti kuhudumia wote hao.

Siku moja alililia sana kwenye simu nilipokuwa masomoni na yeye kazi anayojishughulisha ni ka duka ka rejareja ambako ni vgumu kuhudumia watoto kimasomo, huko nyuma niliwahi muhoji katika hili aliniambia babu yao ndio aliyeahidi kusomesha watoto hao kwasasa ameshindwa kutoka na lile waruwaru la Magufuli makazini akaondolewa.

Sasa kwa hiki kipindi tukipiga stori ananihadithia baadhi ya wanaume wanavyo msumbua mbaya zaidi baadhi ya mwalimu wa kiume mmoja katika shule watoto wanaposoma amemsumbua sana kisa tu swala la ada na akahitaji kuwa nae kimahusiano, siku nyingine akanigusia mmoja wa wazee mtu mzima niliwahi kumuona siku moja akadai anamuhitaji kimahusiano na yuko tayari kumpa moja ya nyumba anayojenga, mzee huyo ni mstaafu serikalini.

Sasa wanajamvi kinachonichanganya hapi ni changamoto hii ya kifedha, mambo haya mwanamke wangu na kiukweli nampenda sana nimezunguka sana ila kwake nimenasa, jamani nifanyeje?
 

No comments:

Post a Comment