Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Wednesday, March 28, 2018

Hii ni moja ya Mipango ya Kishetani kabisa kupangwa dhidi ya Mwenzi wako

katika mapenzi hakuna kitu ninachokiamini kama willingness. na hii ilinisababishia binafsi niwe mtu ambaye sipendi kutumia nguvu ya ziada kuvukuzia mwanamke. why? kama ananipenda tukionana leo hii na mimi kumwomba uhusiano ataonesha nia mapema tu.kama hayupo tayari namwacha aende. hali kadhalika akifikia kuchoka kuwa na mimi akisema basi sihitaji nguvu kumfanya akae nami. why? kama anahitaji kukaa nami atakaa nami.

ni jambo baya sana kwa mwanaume au mwanamke kupanga fumanizi.why? kama unawaswasi na mwenzio ana cheat tafuta ushahidi kwa njia rahisi sana. lakin kama utataka kupanga ushahidi kwa njia ya fumanizi. jiulize ukimfumania utafanya nini? utapigana au kumpiga anaye cheat na mwenzi wako? ili iweje? anayemlinda mpenzi wako ni yeye mwenyewe mpenzi wako anapaswa kujilinda.anapaswa kujitunza hamna haja ya wewe kumfugia mbwa.

kama unaona anachepuka mwache aende. ameshavunja kiapo cha mahusiano..huwezi mlazimisha.ukimfumania ukampiga na kumuua aliyekuwa aki cheat naye wewe binafsi inakusaidia nini? lakini je mwishowe wewe utapata nini? why usimwache ukatafuta anayekufaa?shetani huwa anashiriki kwa kiasi kikubwa katika mipango hii ili yatokee mambo ambayo kwa ninyi nyote ni ya aibu. mwanaume gentleman hawez panga jambo kama hili. kama unampenda mkeo kwa dhati au mpenzi wako kwa nini upange kumdhalilisha mbele za watu?inakusaidia nini?mwache tu kwa siri .waite wazazi wake na yeye mwenyewe fuateni taratibu then mwambie kwa amani na upendo mama nakurusu uende huko ambako kuna maziwa na asali.

the same kwa wanawake usihangaike kupambana na mwanamke mwenzio. tatizo lipo kwa mumeo au mpenzi wako.mwambie atulie yeye kama hataki mwambie basi akamchukue yule mwingine kuliko kukuletea aibu na magonjwa ya moyo/mwili pia. sikushauri ujipange ili kumfumania mkeo au mpenzi wako. haitakusaidia kitu zaidi ya kujiumiza zaidi.lakini kama umeamua kuw atayari unataka kumwacha. basi ikitokea umemfumania achana na ugomvi na matusi. kwa utulivu na upendo mwambie jamaa yeye aondoke. ubaki na mkeo then naye umweleze tu kwa sasa basi unamruhusu asonge mbele.

Tusigombane. nguvu haikuwahi kuzuia mapenzi wala hisia.uarabuni watu wanapigwa mawe mpaka kufa na bado wanaendelea kufumaniana na bado wanawake wana cheat. mapenzi yenyewe ni nguvu tosha sana ya kufanya mambo ambayo akili ya kawaida haiwezi.

No comments:

Post a Comment