Lipo jambo muhimu analopaswa kuzingatia kila aiye kwenye uhusiano ikiwa anataka kutosheka na penzi la mpenzi wake.Kwanza
ni lazima uitosheleze kwanza akili yako, lakini pili, unapaswa kuamini
kwamba uliyenaye ni bora na hata ikiwa kuna kasoro, jambo la msingi ni
kuzungumza kuondoa tatizo hilo, siyo zaidi.Anachanganya mambo, hatoshekiUkweli
ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki katika mapenzi ni wale
wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo,
nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.Lakini
pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao wa zamani,
ambao labda walikuwa wana uwezo mkubwa zaidi katika tendo hilo kuliko
sasa.Hata
hivyo, wakati mwingine wanashindwa kuelewa kuwa hata wale wanaofikiri
ni wazuri, kama wangekuwa nao hadi leo, huenda wasingeweza kuendelea
kuwa imara.Hii ni kwa sababu, watu wengi baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu hupoteza nguvu au shauku ya tendo hilo.Zipo
sababu nyingi za hali hiyo, mojawapo ni kutobadilika kwa mazingira au
wapenzi kuanza kutoelewa kwa sababu mbalimbali kama vile kutojaliana na
kadhalika.Kama
hukuwa unafahamu; ni kwamba, idadi ya wanaume wasiyo na uwezo wa
kufanya vyema tendo la ndoa inazidi kuongezeka. Tafiti zinabainisha kuwa
wastani wa ndoa nne kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea
zinakabiliwa na tatizo hilo.Pia
wanaume sita kati ya 10 wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume,
kwamba kama siyo kuwa na uwezo mdogo, basi hukosa kabisa nguvu za
kuendelea.Wengine wanaweza kuanza, lakini hawawezi kuendelea au wengine hata kuanza ni shida.Ingawa
tiba yake ni ndogo, hasa mchanganyiko wa vyakula kama nilivyowahi
kueleza mara kadhaa.Idadi kubwa ya wanaume bado wanasumbuliwa na tatizo
hili, hasa kwa sababu ya kutokuwa tayari kuchukua hatua hasa za
kuzingatia ushauri.Ziko
sababu nyingi za kukumbwa na hali hii, ikiwamo ulevi, kutofanya
mazoezi, kujichua au utumiaji holela wa vyakula, hasa vyenye mafuta.
Hata hivyo, kwa kuzingatia tiba sahihi ya vyakula bora, mtu anaweza
kupona.Kwa
mfano kuna baadhi ya vyakula vikichanganywa kwa ustadi kama pilipili,
parachichi na kadhalika vinaweza kumfanya mtu kuondokana na tatizo hilo.Wengi
wa watu walio kwenye ndoa za miaka mingi, wanafanya mapenzi kwa sababu
tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja, lakini siyo kwa sababu ya kuwa na
hisia kali.Matokeo yake ni wanandoa wengi hupata msisimko mdogo katika tendo la ndoa wanapokuwa na wenzi wao.
No comments:
Post a Comment