Inaeleweka kuwa wapendanao iwe wanandoa au wapenzi hupenda kufanya mapenzi sehemu yenye mwanga hafifu au gizani.Tofauti na watu na mataifa mengine, kwa Waafrika suala hilo ni siri na linahitaji faragha kukamilika. Lakini
kwa baadhi ya watu imekuwa kero kutokana na kutamani kufanya tendo hilo
gizani, huku wanawake wakitajwa kuwa vinara wa kuzima taa.Utafiti
mpya umebaini kuwa katika kila wanawake wanne, mmoja anapenda na
anakuwa huru kufanya mapenzi gizani kwa sababu mbalimbali ikiwamo
kutojiamini.Carl
Loudgers aliyeshiriki kwenye utafiti huo na kuwauliza wanawake zaidi ya
2,000 kwa kukusanya majibu kwa njia ya mtandao anasema walibaini
asilimia 60 ya wanawake hao wanatamani kuwa na ujasiri wa kukutana
kwenye mwanga lakini wanashindwa.Anasema zaidi ya asilimia 75 walisema hawapendi miili yao, huku asilimia 66 wakisema wanaona aibu kutokana na mwonekano wao.Utafiti
huo uliofanywa na mtandao wa Weight Watchers, ulibaini asilimia 27
wanafanya mapenzi gizani kwa sababu hawaamini miili yao kama inavutia
kwenye mapenzi.Ulionyesha
pia asilimia 38 ya wanawake na wanaume waliohojiwa walisema kuwa
wanaamini wapenzi wao hawatawaona wanavutia wakiwa watupu.Sheiilar Gregam miongoni mwa wanandoa waliohojiwa kwenye utafiti huo alisema jambo linalochangia hali hiyo ni mitandao. Alisema
wanawake wanaoonekana wakiwa watupu kwenye mitandao ni wale wanaovutia
kiasi ukijilinganisha nao inakuwa ngumu kukubali kukaa bila mavazi, huku
wapo ambao wanavutia.“Nikiangalia
mastaa walivyo na maumbile ya kuvutia, baadhi yao wamezaa, natambua
kuwa wapo wanaojirudishia wakiharibika kama mimi baada ya kuzaa, lakini
nakosa kujiamini kabisa na ninaamini hao wanapendeza zaidi yangu,”
alisema Sheiilar katika mahojiano ya utafiti huo.Baadhi yao wamekuwa wakiona aibu ya vitu vilivyomo mwilini mwao kama matiti, alama za mwilini na makovu ya upasuaji.Maziwa kuanguka baada ya kunyonyesha mara tatu.Kuning’inia nyama za tumbo na kuongezeka uzito ni moja ya sababu za kuzima taa.Matokeo
ya utafiti huo pia umebaini wanawake wawili katika kila wanawake watatu
huchukia kuangalia wanawake wenzao wakiwa hawajavaa nguo.Ulibaini kuwa asilimia 60 ya wanawake hawapendi kabisa kujitizama wao wenyewe kwenye kioo wakati wa kuvua nguo.Loveness
Ayoub mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam anasema hupata
wakati mgumu anapokutana na mwanaume mzuri kwa sababu hukosa kujiamini
na hivyo hufurahia zaidi wakijamiiana gizani.Anasema
akijitizama na rafiki zake humwambia amenenepa, hivyo akiwa na mwanaume
anayevutia huamini atamuacha kutokana na umbo lake lilivyo.“Tangu
nipo chuo rafiki zangu walikuwa wananishangaa nikivua nguo, kiasi
kwamba sikuwa nafanya hivyo wakiwepo, hali hiyo imenijengea uwoga na
kunipotezea kujiamini.“Nikiwa
na mwanaume mtu mzima huwa sijali kwa sababu naamini ameona wanawake
wengi amekuja kwangu kwa ajili ya kupumzika na sihitaji kuwa naye
maishani ukilinganisha na wanaovutia ambao natamani hata wanioe,”
anasema Ayoub.“Nimeoa
nina watoto wawili na huyo mke wangu, lakini nikitaka kumuona vizuri
umbo lake akiwa mtupu nimvizie anaumwa au kalala, tofauti na hapo
hajawahi kuvua nguo akakaa mbele yangu,” anasema Omari Kiyungi.Kiyungi
anasema licha ya kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka tisa mkewe hataki
kabisa kukaa mtupu mbele yake kwa madai ya kuona aibu.“Sipendi,
natamani nimuone akiwa hajajiziba na ‘manguo’, lakini juhudi zangu
zimegonga mwamba, hana dalili hiyo na hataki kabisa,” anasema.Anasema
alikuwa anachukia hadi sasa amezoea na akimuona mwanamke amevaa
kihasara hasara anamdharau na kumuona hajiheshimu kwa sababu amezoea
kufichiwa maungo.Alisema
akitizama mwili wake kwenye kioo hasa baada ya kuzaa mara mbili na
kunenepa huogopa na kuhisi anamuangusha mumewe kwa umbile lake.Msimamizi
mkuu wa utafiti huo na mshauri wa masuala ya saikolojia Keren Smedley
alisema wengi wa waliobainika kuona aibu kuvua nguo mbele ya wapenzi wao
hawakuwa na tatizo na walikuwa na kila sifa ya kumshawishi mtu
kuwatizama.Akizungumzia
hali hiyo mfundaji kutoka Mbagala Charambe, Zakia Kilimi maarufu
Mchambaji, anasema wanawake wamekuwa na hali hiyo kutokana na tamaduni
za siku za nyuma kuwa mapenzi hufanywa kwa siri.Anasema
wakati huo hasa kwa familia za kawaida walikuwa wanaishi katika chumba
kimoja, hivyo upende usipende utazungumza na mwenzi wako gizani.“Hii
hali imesababisha hata wanawake wengi kushindwai kuachia hisia zao kwa
wapenzi wao wakiamini wataonekana malaya na wasio na maadili kwa sababu
imezoeleka mambo hayo ni ya kunyata nyata,” anafafanua.Anaongeza
kuwa siku hizi hayo mambo ndiyo yanakwisha na wanawake bila kujali wana
umbo zuri, baya, makovu wanajiachia na kutambua umuhimu wa faragha ni
kuonana hivyo wazazi wasiwatishe watoto wa kike kuwa kujiachia ni uhuni.Zainabu
Jumanne (siyo jina lake halisi) anasema kuwa mpenzi wake anajivunia
kuwa naye lakini wakiwa faragha anashindwa kukaa mtupu. Anasema vivyo
hivyo hata wanapojamiiana kukiwa giza hufanya kila aina ya mbwembwe
tofauti taa ikiwa inawaka.Anafafanua kwa sababu hiyo mumewe akitaka kuburudika na kukata kiu ya kuzungumza naye faragha huzima taa kabla hajaambiwa.“Sijiamini kabisa kukiwa na taa, nahisi kama ananichora ninavyoweweseka, lakini kukiwa giza ashindwe yeye tu,” anasema.Anaitaja sababu nyingine ya kupenda kujamiiana gizani ni matiti yake yamelala halafu hayana nyama.Anasema anatumia ufundi wa faragha kuziba yote hayo kwa kumuonyesha mitindo mipya, lakini ili ayapate hayo sharti iwe gizani.“Kukiwa
giza akakubali kukutana nami, akiniacha nitatambika sina historia ya
kuachwa tangu nikiwa msichana hadi nimeolewa, ingekuwa najiamini na
kujamiiana kwenye mwanga na mautundu niliyonayo, naamini ningekuwa mkali
zaidi, nimejaribu nimeshindwa na kwa hapa nilipofika haiwezekani tena,”
anasema.Mkazi
wa Tandika jijini Dar es Salaam, Yusufali Yusuph anasema hataki hata
kumsogelea mwanamke anayependa kujamiiana gizani kwa sababu huamini kuna
kitu anaficha.Anasema siku hizi maradhi mengi, anaweza kudhani anaona aibu au hajazoea kumbe kuna jambo anaficha.“Haa raha ya mapenzi muonane jamani gizani tena! Siwezi na simtaki mwanamke wa aina hiyo,” anasema Yusuph.Mtaalamu
wa masuala ya saikolojia Modester Kamongi anasema yapo mambo mengi
yanayochangia mwanamke kuogopa ikiwamo kutokujiamini.Anasema
mila, desturi na tamaduni ni miongoni mwa mambo yanayochochea hilo kwa
sababu wanawake wengi huamini stara ndiyo sifa ya kuwa mke bora na
kushindwa kutofautisha mahali pa kujistiri pa kujiachia.Kamongi
anasema linapokuja suala la aibu siyo kwa wanawake pekee wapo wanaume
wenye aibu na wameumbwa hivyo, ikitokea kukutana na mmoja wa watu hao
cha kufanya ni kuwazowesha taratibu hatimaye kama binadamu watakubaliana
na hali halisi japo kwa shida.“Huwachukua
muda kuzoea, lakini uwezekanao upo na wakasahau kabisa kama walikuwa
hawawezi, lakini inahitaji utayari wa kuwazowesha badala ya
kuwalazimisha, ”alisema Kamongi.Anaitaja sababu nyingine inayochangia wanawake kukataa kukaa utupu kuwa ni kutojiamini.Anasema hali hii hutokana na maneno anayosikia au aliyosoma kuhusu umbo lake.Anafafanua
kuwa kuna baadhi ya familia mtoto akiwa mnene au mwembamba au ana umbo
fulani uhusisha umbo hilo na neno ukiolewa sijui itakuwaje.“Mtoto
hukuwa na neno au misemo ya aina hiyo hivyo anapoolewa au kuwa na
mpenzi hukumbuka na kutamani asimuone kwa sababu hajui itakuwaje kama
alivyokuwa anaambiwa.“Wengine
hudhani mwanaume akiona umbile lake ambalo lilikuwa linawaisha ndugu,
rafiki zake litamtisha pia na kuamua kumuacha, hivyo huona afadhali nusu
shari kuliko shari kamili ya kuachwa,” anasema Kamongi.Anaeleza
wote hao wanaweza kubadilika iwapo wataeleweshwa na kujengewa kujiamini
ikiwamo kwa kusifiwa kila wanapokaa bila nguo hata kwa bahati mbaya.“Wengi
wao hawajiamini, wakisifiwa na muhusika kuonyesha kutamani kuona
maumbile yao mazuri yakiwa wazi taratibu watabadilika,” anasema.Ushauri
wazazi wawajenge watoto wa kike kuthamini vile alivyo navyo hususan
kuukubali mwili wake badala ya kuwasema kwa ubaya kwa eneo lolote la
mwili lililozidi au kupungua.
No comments:
Post a Comment