"Tujua ni rahisi kuamini wanawake wote ni vichaa, hawakuelewi, hawajui kipi wanahitaji na mengine mengi!".
Tunaweza sema pole kwa bahati mbaya ulionayo, iwapo kama bahati ingekua kweli ndo inasababisha wewe kuachwa kwa kila uhusiano unaokuanao, tukiendana na ukweli kabisa, sababu ipo kwa yule unaemwangalia kwenye kiio kila mara ujiangaliapo, haiwezekani wewe kuwa unaachwa kwenye kila uhusiano unaokuanao na kusema sababu sio wewe.

Sio
kusema kuwa wewe ni mtu mbaya au una sura ngumu kushinda wengine,
hapana!, ila unakua unarudia kufanya maamuzi mabaya pamoja na kuwa na
tabia flani flani mbaya ambazo zinasababisha haya kwa kila uhusiano unao
ufanya na wewe kujikuta ukiachwa, kuna baadhi ya makosa kwenye uhusiano
unajikuta unafanya bila ya wewe kujua.
Kama
unataka kujua kwanini kuachwa ni kitendo kinachokua kinakutokea kwenye
kila uhusiano, soma hapa na uone kama haya mambo ni mapya kwako..
1. Unamuhitaji mpenzi wako kupita kiasi.
Hali ya kumuhitaji mpenzi wako ni kitu cha kawaida katika mahusiano, na ni hali ya kupendeza sana, ila hio hali ikivuka mipaka ni mbaya sana, inawezekana inatokana na shauku ya kuwa nae au hali ya wewe kutojiamani, na unakuwa tegemezi sana kihisia, usipomuona unakua kama unaumwa, na ukimwona kila saa unataka kuwa nae, hii inampa presha kubwa mpenzi wako kiasi mpaka anakuona kama mzigo na inashusha hamasa ya mapenzi kwake, hata mapenzi yanaitaji nafasi, na inawezekana ndo kisa cha kuachwa kwenye uhusiani uliopita, bila wewe kujua na kwenye uhusiano huu ndo unaongeza juhudi zaidi bila kujua ndo unaharibu zaidi.
2. Una wivu unaopitiliza.

Kuwa na
wivu kidigo kwenye mapenzi ndo chachu ya mahusiano, ila kuanzisha ugomvi
kila saa unapokuta amesimama na mwanaume ni mbaya, kama mpenzi wako
anakushitumu kuwa na wivu wa kupitiliza unao mkera ujue uhusiano huo
unaelekea pabayam na hamasa ya mapenzi kwa mpenzi wako itaanza kushuka.
Kwanza hapo inamaanisha unatatizo la kutomwamini, ambalo inawezekana
limesababishwa na uhusiano wa nyuma kabla ya huu ulionao, kwa mfano kama
ulishawahi kufumania kwenye uhusiano uliopita au hujiamini kama mpenzi
ulionae anakupenda kwa dhati!, na ni chanzo kikuu cha kuanzisha ugonvi
usiokuwa na maana, na kurudisha nyuma hamasa za mpenzi wako kwako.
Weka akilini sio kila mwanamke sio mwaminifu, jiamini na jiamini unapendwa.
3. Hauchukui wajibu kwenye makosa yako...
3. Hauchukui wajibu kwenye makosa yako...
Wanaume
wengi hupenda kurumbana, na wanahisi kurumbana na kutoa shutuma ndio
kuwarekebisha wapenzi wao, na ndo jia pekee ya kufanya wapenzi wao
wawaheshimu, na saa nyingine haya maono yanawapeleka mbali kiasi kwamba
hata wenyewe wakifanya makosa hawajui kuchukuwa wajibu, jambo lolote
likitokea ambalo wamesababisha wao hawawezi kukubali kosa, kiasi
wanawaona wapenzi wao sio waelewa, maono haya husababisha kuachwa na
kukimbiwa na wapenzi,hakuna
binadamu atakaye weza kukuvumilia kama hujui kuchukua wajibu na
kukubali makosa yako, na inawezekana kabisa baada ya hapo bado
wakaendelea kumshitumu msichana kwa kuondoka.
Ukitaka kukaa na msichana kwenye uhusiano na uendelee kwa muda mrefu jifunze kuchukua wajibu kwenye makosa yako.
4. Unajishusha kwa kila jambo...
4. Unajishusha kwa kila jambo...
Unajaribu
kumvuta mpenzi wako kwa kujishusha, haulalamiki, haubishani,
unabembeleza kila kitu kupita kiasi, saa nyingine kosa umefanyiwa wewe
bado tena wewe mwenyewe ndo unaenda kuomba msamaha, hata huwezi
kumkaripia na akikuacha na kuhisi wewe uko kama bwege na kwenda kwa
mwanaume mwingine bado unalalamika, na ukipata uhusiano mwingine mpya
unaendelea kujishusha zaidi.
Wanawake
wanapenda watu wenye msimamo na wanaojiamini, mtu anayeweza kuongoza
familia, kama akikuacha akaondoka naomba usimshutumu maana nae anatafuta
mwanaume aliye bora ambae hata kama akianzisha familia nae anaweza
kuiongoza familia.
5. Haubagui...
5. Haubagui...
Ukijikuta
unaachwa mfululizo, ni kwa sababu haubagui, unahisi labda ukijishusha
na kuwa na mpenzi yeyote yule hata kama hamuendani kimawazo na kimaono
labda atakaa, hii inakufanya umpate msichana asiye endana nawe na
kusababisha mparanganyiko na tofauti za kihisia kati ya wewe na yeye
kwenye mahusiano yanayosababisha kuachana kwenu.
6. Unahisia zako ziko juu mno kupita hali ya kawaida...
6. Unahisia zako ziko juu mno kupita hali ya kawaida...
Kuwa na
hisia kupitiliza ni moja ya sababu unaendelea kuachwa, unakua unamweka
mpenzi wako katika hali tata, maana jambo dogo kutokana na hisia zako
zilivyojuu sana unakua unaliona ni kubwa, hii inasababisha ugomvi ambao
haupo, na utakua unaona unakosewa katika kila kitu mpenzi wako
anachofanya, akili yako inakua inafikiria vitu ambavyo havipo, na
kusababisha kutokua na amani kwenye mahusiano, na hii inashusha hamasa
kwa mpenzi wako na kujikuta ukiachwa na pia hauta jua hata nini lilikua
kosa lako.
Kama
unaendelea kuachwa katika kila mahusiano uliyonayo, ni vizuri ukaanza
kuchunguza na kuangalia nini unakosea na kurekebisha tabia zinazopunguza
hisia na hamasa kwenye mapenzi, ni muda wa kuanza kufanya mabadiliko.
No comments:
Post a Comment