Katika
hali nisioitegemea tumegongana ana kwa ana gest mi na shemeji yangu wa
karibu ambae mme wake tunafanya kazi pamoja. mimi nikiwa nampeleka
mgeni wangu kwenye chumba alichofikia mara ghafla chumba chumba cha
pili mlango ulifungulia na kikatokea kichwa tu kugeuka tukagongana ana
kwa ana huyo shemeji yangu ilichukua takriban sekunde 30 kukodoleana
macho na baada kutoa salam sauti ya chini mimi niliingia chumba cha
mgen wangu kumuaga na kumtakia safari njema wakati natoka huku mwili
ukiwa umekufa gan kwa kutoamin nilichokiona kwa shemeji yangu na
kutambua alienipokea zamu ya lindo saa 12 jion mke wake ana madudu
niliishiwa nguvu kabisa, alikuja mhudum wa ile gest akaniitia chemba
baadae akaja jamaa ambae sikuweza kumtambua kutokana na mazingira na
kunieleza kilichotokea muda mfupi uliopita anaomba iwe niifanye kuwa
siri kwanza ametokanae mbali isitoshe ni mzazi mwenzie na akanikabidhi
elfu 70 ambayo mi nilikataa kuipokea huku nikimwambia kwasasa nahitaji
kuwahi nyumbani mambo mengine tutawasiliana kwa simu ili kukwepa
ushaidi niliondoka lakin hatua chache baadae ilipigwa simkuingalia
ilikuwa ya shemeji yangu akinisihi lile suala anaomba liwe siri kwa
gharama yoyote ile na nimpe muda mfupi mtu wake anafanya michakato ya
hela soon nitapata kwa njia ya m-pesa. kubwa kwangu jamaa tumetokanae
mbali sana urafiki kwetu ni zaidi ya ndugu tumesoma shule ya msingi
moja tumeachana sec. tumeingia depo pamoja na kupangiwa kituo kimoja
yaani kama bahati tu hofu yangu ni kwamba asikie hii isue najua alaf
sikumpa taarifa atanionaje mimi? mpaka sasa natambua kwamba ameoa na
ana watoto wawili huyu jamaa ameniambia kwamba ni mzazi mwenzie
nashindwa kuelewa na proces zote za uchumba mi nilihusika na sikuambia
kama amezaa, katika nyakati tofauti nimeingiziwa kwa mpesa zaidi mil.
1.2 kwa saa 17
No comments:
Post a Comment