Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Sunday, April 29, 2018

Jeuka Uwe Mwanaume UJUBA Uvutie Wanawake

Wiki chache zilizopita nilimuona huyu mwanaume akiapproach mwanamke katika klabu.

Hio approach yake ilienda hivi:
Alitembea mpaka pale mwanamke aliko.
Yani alivyokuwa akimsogelea alikuwa akitembea na mwendo wa kupapatika, anaenda upande wa kulia na kushoto.
Wakati alipokuwa akimuapproach alikuwa akiangalia kila kitu isipokuwa huyo mwanamke.
Niligundua hapo hapo kuwa huyo mwanamke hakuwa interested.
Halafu sasa akaanza kuongea...
"Hi, natumai sijakutia wasiwasi, je nikununulie kinywaji?"
Kimtizamo wangu aliongea kama mtoto mdogo ambaye anaomba msamaha kutoka kwa mamake kwa kosa alilofanya.
Mwanamke alikubali kuitishiwa kinywaji, mwanaume alisimama hapo akionekana amezubaa kiasi.
Kufikia hapo huyo mwanaume hakusema lolote na alijeuka upande ule mwingine wa klabu na kuagiza kinywaji.
Nilikaa  nikimuangalia kwa dakika mbili akiwa na huyo mwanamke...
Unajua alisema nini baada ya hayo madakika mawili machungu?
"Sasa...ushawahi kuja katika hii klabu awali?
Hivyo tu...
Unajua mwanamke alimjibu nini?
"La, hii ni mara yangu ya kwanza.
Unajua alisema nini?
"Oh, poa. Pia mimi."
Na stori ikaisha na hapo.
Hakuendeleza kumuuliza maswali. Hakubanta. Hakusema, "Huwa kawaida naenda sehemu flani inaitwa X. Ushawahi kuenda huko? Unapaswa kutembea huko coz utajienjoy..."
Niko sure unajua jambo ambalo lilitendeka baada ya hapo, mwanamke alijitafutia kisababu akatoka na hakurudi tena.
So tatizo lilikuwa wapi reader wa N.M Blog?
Alifanya kosa ambalo wanaume wengi wanafanya wakati wanapokutana na wanawake...
Alionekana mnyonge na mpole sana...
"Natumai sijakutia wasiwasi" na "Je nikununulie kinywaji?"
Maneno hayo ni ya kijinga na wanawake hawayapendi.
Unajua kitu ambacho kinawasisimua wanawake?
UJUBA
Ni vile ambavyo unatamka na kuyamiliki matamshi yako.
Unapoaproach mwanamke  mwangalie machoni muda wote.
Weka kifua chako mbele, kichwa kisimamishe wima.
Kuwa confident na maneno unayoyatamka. "Hey, napenda viatu vyako. Hizo heels zina urefu kiasi gani? Haviumizi miguu yako? Mimi naagiza vinywaji. Unataka kinywaji kipi?"
Si ujeuri. Si ufidhuli. Na wala si kiburi.
Ni UJUBA.
Inaonyesha nguvu na nishati na inawasisimua wanawake.
Jeuka uwe na ujuba na utajeuka yule mwanaume ambaye kila mwanamke anatamani kuongea naye.
Hii haimaanishi kuwa utafaulu kwa kila mwanamke...
Lakini watataka kujua zaidi kukuhusu.
Watakuwa interested na wewe.
Na watatamani kukuona tena.
Sahau zile mbinu zako ambazo ni za kuomba.
Ukitaka kuonekana mwanaume mwenye ujuba basi lazima ujifunze kujiamini. [Soma: Jinsi ya kujiamini]

No comments:

Post a Comment