Mbinu #1: Toa majibu yasiyokuwa moja kwa moja.
Wanawake wanapenda majibu ya moja kwa moja kama wanataka kujua kitu flani kutoka kwako. Mwanamke anaweza kukuuliza "Wewe unafanya kazi gani?" ama "Uko na tatoo kwa mwili wako?" Usijibu maswali haya moja kwa moja. Badala yake mzungushe kwa kumwambia "Mimi ni jasusi siku za juma halafu wikendi nafanya kazi kwa club kama bausa." Kama ataudhika na jinsi umekataa kujibu swali lake moja kwa moja, unaweza kumwambia "Nitakwambia tukikutana" ama "Nitakwambia wakati tunaongea kwa simu."
Mbinu #2: Mtumie meseji ya utani kama hakukujibu.
Kama atashindwa kukutumia meseji baada ya lisaa moja, mwambie "Umefutwa
kazi." Atakupigia na kutaka kujua ni kwa nini umemwambia hivyo na
atataka ueleze kwa upana umemaanisha nini.
Mbinu #3: Weka ratiba ya kupiga simu.
Kama mnatext na moto, kama vile anareply texts zako chini ya dakika moja
baada ya kumtumia text, katiza maongezi yanu kwa kumwambia "Hey, nataka
kwenda, lakini nitakupigia simu kesho jioni." Kama utafanya hivi vile
inavyotakikana atataka akupigie wewe simu na atakuwa active wakati wote.
Wakati unatimiza mbinu hizi, kuna sheria ambazo unahitajika kufanya ili akuheshimu wakati wote.
Sheria #1: Moja kwa moja - Anapaswa kutuma angalau jumbe mmoja kwa kila jumbe ambayo utamtumia.
Sheria #2: Kama hatajibu meseji yako moja, usimtumie meseji siku nzima. Kama hatajibu meseji yako ya pili usimtumie jumbe wiki nzima.
Sheria #3: Usimtext ukimwambia jinsi unahisi vibaya kwa kuwa
anakataa kujibu meseji zako badala yake umpigie simu na umsunze kuhusu
simu yake.
Waweza kusema "Hi, najua kuna kampuni ambayo itakulipia bili ya wiki
nzima ya mjazo wako wa simu kwa kufanya kazi mfano wa mhudumu wa hoteli.
Je unataka nikuunganishe?
Kwa kutumia mbinu hizi tatu + hizi sheria tatu utakuwa uko sawa katika gemu ya kutext.
No comments:
Post a Comment