Ushawahi kujiuliza kwa nini kuna baadhi ya wanaume wakiingia katika
klabu hutoka na wanawake wanaopendeza zaidi? Ama ushawahi kujiuliza ni
kwa nini kuna baadhi ya wanaume wakiingia katika klabu wanawake wote
wanataka kuongea ama kutangamana nao. Na je mbinu hii inaweza
kufanikishwa kivipi?
Hebu tuangalie hii mifano...
Hali #1: Kikundi cha wanaume watatu wameingia katika klabu.
Wanaume hao wanatafuta meza ya kukaa. Wanapata sehemu ya kukaa na
wanachukua masaa mengi wakinywa bia na kufuata kila mwanamke anayepita
kwa macho huku wakipigana makumbo kuonyesha wanaridhika. Wanawake
wanawadokezea macho ya kigeni na wanaipita sehemu walioko haraka
iwezekanavyo. Baadae, wanaume hao watatu wanaapproach kikundi flani cha
wanawake katika meza flani na wakatumia michongo yao mizuri kuwavutia.
Hao wanawake waliangaliana, wakasimama na kuenda zao.
Hali #2: Kikundi cha wanaume watatu wanaenda katika klabu
nyingine na mara moja walianza kusalimia watu walioko katika klabu hio
kabla hawajaenda katika meza iliyokuwa kando. Kwa muda wa lisaa moja
walikuwa wakitumia muda wao wakitangamana na (wanaume au wanawake)
waliokuwa wakipita, na cha kushangaza ni kuwa wanawake walionekana
wakijitokeza kutoka sehemu yeyote kuja kuwasalimia wanaume hao. Baadaye,
waliapproach kikundi cha wanawake ambao walikuwa wametulia katika meza
flani. Na bila kupoteza muda wanawake hao walikubali kudensi na wanaume
hao katika sakafu.
So tofauti ni ipi katika makundi haya mawili? Jibu ni kuwa kundi la pili
lilitumia 'nguzo ya maingiliano' ilhali kundi la kwanza halikutumia.
Kundi la kwanza halikuwa na hadhi ya kijamii. Walijitawanya na kujitenga
kwa dunia yao. Tendo walilolijenga la kujitenganisha lilijenga athari
hasi kwa kila mtu katika sehemu hio. Katika lile la pili, kundi hilo
lilijenga mazingira ya kuonyesha kuwa wako huru kutangamana na yeyote
hivyo ni rahisi kwao kuongea nao na kuwaaproach. Mwanamke hatohisi shoto
kupita karibu na meza ya kundi hilo na kukaa hapo.
Kuwa na marafiki waliokuzunguka, na kuonyesha uwezo wa kujenga urafiki
na watu kutaongeza hadhi yako ya kijamii mbele ya macho ya wanawake
ambao unataka kuwavutia. Utakuwa "umechagulika" na wanawake ambao tayari
wamevutiwa kwako.
Jambo zuri kuhusiana na mbinu hii ya nguzo ya maingiliano ni kuwa
unaweza kuitekeleza hata kama utakuwa uko pekeako. Pindi tu utakapoingia
katika himaya ya kujamii, jenga urafiki na utangamane nao. Usijitenge
kwa kona halafu utarajie kuwa wanawake watakuaapproach; hawatathubutu.
Hii hapa ni mbinu ya haraka ambayo itajenga nguzo ya maingiliano na uweze kutambulika na wanawake:
Hatua #1. Ingia ndani ya klabu na uweke tabasamu kwa mwanamke
kando yako. Ukiona kikundi, approach halafu ufunguke. Tumia madakika
kadhaa na wao mkibadilisha salamu na mawazo kabla ya kujiondoa. Kama uko
na rafiki yako unaweza kumtuma katika kikundi kingine.
Hatua #2. Tangamana na ujenge urafiki na kila kikundi halafu
katulie katika sehemu ambayo imetulia katika hio klabu na rafiki mpya
ambaye umekutana naye kwa moja wapo ya makundi hayo. Ongea na kusalimia
yoyete ambaye umekutana naye awali katika klabu hio.
Hatua #3. Usichague wala ubague. Ni lazima utangamane na uongee
na kila kundi hata kama mwanamke unagemuwinda hayuko katikayo. Fikra hii
ni kukufanya utangamane zaidi ili uongeze hadhi ya kijamii na ukutane
na watu wengi zaidi.
Kufikia mwisho wa usiku, utakuwa ukiongea na kubadilishana mawazo na
karibu kila mwanaume na mwanamke hapo. Na katika harakati hii
itakusaidia wewe kupata mwanamke unayemvizia kwa urahisi sana. [Soma: Mbinu rahisi ya kupandisha hadhi yako kwa wanawake]
Kazi kwako sasa!
Sunday, April 29, 2018
Jinsi Ya Kutumia 'Nguzo Ya Maingiliano' Kuwavutia Wanawake
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment