Wanawake wakubwa huwa wanakuwa na ladha tofauti ikija kwa maswala ya
mapenzi – ile ambayo wanaonyesha kupenda wanaume wadogo kiumri. Na kwa
sababu wanaume wengi huwa wanavutiwa na aina hii ya wanawake, bila shaka
wanaume hawa hutaka kujua jinsi ya kuwavutia wanawake wakubwa kiumri.
Uzuri ni kuwa uhusiano na mwanamke aliyekushinda umri siku hizi
inaonekana jambo la kawaida.
So, kama unataka kujua jinsi ya kuwatongoza wanawake wakubwa basi hizi mbinu saba zitakusaidia vizuri.
#1 Thamini kile ambacho anakupatia
Kama unataka kujua jinsi ya kutongoza wanawake wakubwa kiumri, basi
unapaswa uthamini kile ambacho anacho. Kwa lugha nyingine ni kuwa
unapaswa kusimamisha fikra zako za kuangalia miaka yake au mikunjano ya
uso wake, na uanze kufikiria mambo ambayo anaweza kugawa na wewe ikiwemo
mapenzi. Wanaume wengi hudhania kuwa wanawake wadogo ndio huwa na ujuzi
ikija na maswala ya mapenzi lakini huwa si ukweli.
Ijapokuwa ni kweli kuwa kujua jinsi ya kutongoza wanawake wakubwa
kunahitaji mmoja kuzoea, yaani utahitajika kuthamini na kutambua umri
wake, kiujumla; utakuja kujua baadaemkuwa utakuwa umechukua hatua kubwa
katika kudeti wanawake wadogo na wale wa wasiwasi. Kwa mfano hutapata
mwanamke aliyekomaa akikimbia kwenda msalani ili kuongea na mashoga zake
kuhusu deti aliyoko. Hii bila shaka itakuwa ni mwamko mpya wa kutongoza
na pia utaboresha uwezo wako wa kutumia mistari kiurahisi na haraka.
#2 Mnyeshee heshima
Wakati unapojifundisha jinsi ya kumtongoza mwanamke mkubwa, weka kwa
akili yako kuwa atataka kupewa heshima zake zaidi ya vile wanawake
wadogo utakavyowapatia. Hii ni kwa sababu ana experience ya juu zaidi ya
maisha. Na kwa sababu ambazo zitategemeana na yeye, mwanamke aina hii
anaweza kuwa asiwe huru kufunguka na kukueleza maisha yake ya zamani ama
kukufungukia kuhusu maisha yake. La muhimu zaidi ni kuwa usimwonyeshe
kuwa lengo lako kuu kwake ni kumuonyesha kuwa unatoka deti na yeye ama
una uhusiano wa kimapenzi na yeye kwa sababu huna jingine la kufanya au
umelazimika. Michezo kama hii haiwezi kufanya kazi kwa mwanamke aina hii
– kumbuka hilo.
#3 Muonyeshe kuwa wewe ni classy, mjanja na usiyesomeka
Kama unataka kujua jinsi ya kuwatongoza wanawake wakubwa waliokupita
umri, basi ni jambo la muhimu kabisa kuhakikisha kuwa unakuwa mjanja na
kuwa na tabia za kukomaa. Wanawake wakubwa tayari wanaexprerience ya
kuwa na deti ambazo zilikuwa mbaya awali, so kama unataka kumshawishi
mwanamke ambaye ni mkubwa wako kiumri vizuri, basi utahitajika
kupandisha gemu yako iwe ya juu.
Kimsingi, wanawake wakubwa hawatakuwa interested na wanaume wenye nyege
ambao wanashindwa kumaintain gumzo la kawaida mara kwa mara. Badala yake
watatafuta mwanaume ambaye ni gentleman ambaye anaweza kuongea kuhusu
mambo ya kisiasa na yule ambaye anaweza kutofautisha aina aina za duvai
ama angalau yule ambaye anaweza kuchagua sehemu nzuri ya kutoka dinner.
So, kadri unapozidi kuwa mjanja, ndipo inazidi kuwa rahisi kumtongoza
mwanamke aliyekupita kiumri kuweza kuwa na wewe.
#4 Usijionyeshe
Kuonyesha vitu unavyomiliki ama kuonyesha ujuba wako hakutakusaidia
kutongoza wanawake waliokupita umri. Siku hizi wanawake wanapenda kupata
nafasi ya kuonekana kuwa wana madaraka flani, so mwanamke atapoteza
interest na wewe haraka sana kama utaanza kujidai na kuringa kuhusu
idadi ya wanawake ambao umefanya nao mapenzi ama idadi ya magari
unayomiliki. Kama umevalia suti ya kushonesha ama una Mercedes ya
gharama si lazima umwambie kuvihusu kwani atajionea yeye mwenyewe.
Badala yake msifu na kumpongeza kwa mambo aliyofanikiwa kufanya. Hii ni
njia rahisi ya kuweza kuwatongoza wanawake waliokupita kiumri na
wakakukubali kirahisi.
#5 Jiamini
Njia nyingine rahisi ya kutongoza mwanamke aliyekupita umri ni kwa
kuonyesha kuwa unajiamini kwa kila kitu unafanya au kuzungumza. Wanawake
aina hii huwa kwa kawaida wanapenda wanaume ambao wanauwezo wa kutatua
tatizo lolote ambalo watarushiwa usoni mwao. So, kama wewe ni mwanaume
ambaye hujafikia kiwango cha kujiamini , basi ni wakati wako wa kuchukua
hatua ya kuhakikisha ya kuwa unajenga ujiaminifu wa kuweza kuongea na
wanawake. Unaweza kujifundisha kuhusu biashara, sanaa na mambo ya
kisasa, silaha ambayo unaweza kuitumia iwapo mwanamke aina hii atazua
mjadala akiongea kuhusu swala kama hili. Wanaume ambao wanaelewa kile
ambacho wanaongea huwa wanakuwa na confidence zaidi mbele ya wanawake.
Pia wanaonyesha utawala ikija kwa maswala ya mahusiano. Kama unataka
kuwa bingwa katika kutongoza wanawake waliokupita umri, basi confidence
itakuwa ni silaha kubwa katika mpango mzima.
#6 Yaweke mapenzi yawe ya hali ya juu
Kama unataka kumshawishi mwanamke aliyekushinda kimiaka vizuri, unafaa
kuhakikisha kuwa unaweka mapenzi yawe juu. Hii inamaanisha kuwa,
ijapokuwa hatakuwa na tabia za kama wanawake walio wadogo, unapaswa
humchukulia kama mwanamke mdogo. Mnunulie chokoleti, maua na zawadi
ndogo ndogo mara moja au nyingine. Msifu wakati amevalia nguo nzuri ama
anapopendeza mnapotoka out. Mambo haya madogo madogo ambayo unamsifia
mwanamke yatamfanya mwanamke kuwa na furaha na atapendezwa na wewe.
#7 Usitaje kuhusu utofauti wa miaka yenu
Na lile jambo muhimu la kuzingatia wakati wa kujifunza kutongoza
wanawake waliokupita umri ni: kutotaja tofauti ya miaka yenu. Hata kama
haujiskii huru na kuwa na yeye mara ya kwanza, hupaswi kuzungumzia swala
hili. Ama unaweza kuharibu nafasi yako ya kumtongoza. Badala yake
makinika na mambo ambayo yanahusiana nyote wawili, kama vile kuongea
kuhusu mambo mnayopenda au kuongea kuhusu filamu. Pia unaweza kuingiza
ucheshi katika mazungumzo yenu; hii hufanya kazi nzuri kwa mwanamke.
So hizi ndizo mbinu unapaswa kuzijua ikija na maswala ya kutongoza mwanamke ambaye amekushinda kiumri. Upo!
Sunday, April 29, 2018
Jinsi Ya Kutongoza Wanawake Wakubwa
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment