Kuwavutia wanawake wakati mwingine huwa vigumu. Mwanzo, hata kama una
mbinu ambazo zimehakikishwa kufanya kazi utapata bado wanaume wengine
wanashindwa ikija katika maswala ya kutongoza na kushawishi. Hii ni kwa
sababu mbinu unazopewa na majamaa wanaojiita mabingwa wa kutongoza
wanakupa habari ambazo hazina maana.
Kwa bahati mbaya, wanaume wengine huwa wanafanya makosa mpaka kwa
wanawake wao. Kama haya yote yanakulenga wewe, basi relax kwa kuwa
makosa aina hii yanaweza kutatuliwa. Kile ambacho unahitajika ni kusahau
kila kitu ambacho umekuwa ukishikilia katika akili yako.
Haya hapa ni baadhi ya makosa ambayo yanafanywa na wanaume na ambayo
wanapaswa kuyaacha haraka sana kama wanataka kuwa na maisha mazuri na
mwanamke.
#1 Kuonyesha tabia mbaya
Katika mapenzi na maisha, hakuna kile ambacho kinajalisha zaidi kuliko
matendo. Kama utajiheshimu wewe mwenyewe, watu pia watakuheshimu – na
wanawake watapendezwa na hili jambo na watajaribu kuleta uunganishi na
wewe. So usiseme maneno ambayo hunuwii kusema na usivunje ahadi zako.
Jiamini kila wakati, na pia ni muhimu upate kujua vile ambavyo watu
watakuchukulia kabla haujatamka jambo lolote. Kumbuka: kama utaonyesha
mambo chanya kila wakati, basi kuna uhakika wa juu kwa wanawake
kukuandama na kutaka kutangamana na wewe kila wakati.
#2 Kuwa na confidence ya chini
Katika macho ya mwanamke, hakuna kitu ambacho kinamfurahisha na
kumsisimua kama kumuona mwanaume ambaye ana confidence. So usijaribu
kuonyesha watu kuwa 'unaweza' kuwafurahisha; hii inaweza kuonyesha
unyonge wako. Kama wewe unajiona kama ni mfalme wa hii dunia, basi
wanawake watafikiria vivyo hivyo. Lakini hii haimaanishi kuwa unapaswa
kuvuka mipaka ya kuonyesha confidence zako mbele ya mwanamke. Haina haja
ya wewe kuonekana kama fala ama kujisifu kwa jinsi vile ulivyo mkali
ikija na maswala ya kuwatongoza wanawake wa aina yoyote.
#3 Kudanganya
Kudanganya kiasi kunakubalika. Lakini, kudanganya mara kwa mara
kutaishusha hadhi na uaminifu wako mbele ya wanawake. Kando na hapo
kudanganya sana kunaweza kukakujeukia siku moja au nyingine.
Kwa bahati mbaya, wanaume wengi wanaamua kudanganya ili kuweza kuondoa
ule wasiwasi wa kusema au kuongea ukweli. Lakini kile kitu ambacho
unasahau ni kuwa ukidanganya, kuna siku ambayo unaweza kushikwa; na
ukishikwa utakuwa umeharibu sifa zako zote ambazo ulikuwa ukijenga. So
ni bora zaidi uongee ukweli na uhakika. Kama unashindwa na la kumwambia
mwanamke, basi ni bora zaidi kunyamaza kuliko kudanganya.
Hii pia inaenda kwa ile tabia ya kudeti wanawake wengi wakati mmoja.
Badala la kuruka deti moja hadi nyingine na kuomba kuwa hakuna mmoja
atakayejua, ni bora zaidi kuwaambia kuwa hauko tayari kuingia katika
jukumu lolote na yeyote. Hii itakusaidia kupunguza wasiwasi ambao
ungekuwa nao.
Kama umefanya kosa lolote katika haya ambayo tumetaja, jambo ambalo
unatakiwa kufanya ni kusoma kutokana na makosa haya. Baada ya muda mfupi
utaona utofauti katika maisha yako ya kudeti.
Sunday, April 29, 2018
Makosa Unapodeti Mwanamke Ambayo Unapaswa Kuyaepuka
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment