Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q ameeleza ni kwanini sasa hivi
ameamua kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi tofauti na hapo awali.
Hitmaker huyo wa ngoma ‘Fresh’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa
kwa sasa amempata mtu ambaye wanaendana sawa kimtazamo hasa katika
maongezi yao.
“Sikuwa na hiyo picha kwamba nakuja kuwa wa kwake, sema nilikuwa
navutiwa na maongezi yake, yaani naongea na mtu ambaye anajua vitu vingi
ambayo na mimi navijua,” amesema Fid Q.
“Unajua kuna vitu fulani unakuwa unaongea na watu, kuna watu wanakuwa
wanakuona kama chizi na kuna mtu mwingine ikitokea unaongea naye na
anakuelewa, labda vitu vya kisaikolojia na anakuelewa unaona inanoga,
kwa hiyo hicho ndio kitu kilivutia zaidi,” ameongeza.
Rapper huyo ameongeza kuwa baada ya mazungumzo ya hapa na pale na mrembo
huyo amegundua kuwa wapishana siku moja katika kuzaliwa (birthday), Fid
Q amezaliwa, August 13 na mpenzie August 14.
Saturday, June 9, 2018
Fid Q Afunguka Kuhusu Mahusiano Yake ya Kimapenzi
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment