Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu
kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha
na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu
unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo
zinamfanya amsaliti mumewe:
1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI
Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni
kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume,
watoto, nyumba na familia kwa ujumla.
Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa
kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble
kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu
anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo
fursa.
2. UKOSEFU WA MAHABA
Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji
kupendwa, mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu
basi anaridhika.
Mwanamke anahitaji kupetiwapetiwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji
aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu,
mwanamke anataka hivyo, anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu
anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake, ampe
lugha ya kimajnun, mwanamke anamtaka Majnun. Sasa akimpata mtu wa aina
hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu, mnanipata hapo?
3. USALITI WA MUME
Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale
anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti. Hapo mwanamke anaweza
akabadilika kabisa. Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi.
4. KUTOJIAMINI
Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi
jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea
mengine kabisa. Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa
makini mambo haya.
Monday, June 11, 2018
Haya Hapa Ndio Makosa ya Mwanaume Yanayosababisha Mke au Mchumba Amsaliti
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment