Nipo tena kwa Mara nyingine katika kubadilishana uzoefu juu ya mambo
mbalimbali yanayohusu mahusiano,kuna jambo limekuwa likiniumiza kichwa
sana ni swala zima la kulogwa au kupewa limbwata na mwanamke.
Nidhahiri kabisa mambo haya katika jamii yetu yanafanyika kwa baadhi ya
wanawake huwa wanawafanyia wanaume,na tatizo hilo limezidi kushamiri
zaidi kutokana na ongezeko kubwa la waganga wa kienyeji.
Nimefanya research kwa baadhi ya waganga wameniambia wateja wao wakubwa
ni wanawake na shida kubwa wanayokuwa wanahitaji ni kuolewa au
kuwadhibiti wanaume zao.
Nami mekuja kugundua wanaume wengi huwa wanafanyiwa madawa ila wakati
mwengine mungu huwalinda hawazuriki bila ya wao kujua na wanaume wengi
ambao wapo katika hatari hiyo ni wale wenye kipato kidogo ambacho
kinarizisha.
Sasa basi nimejaribu kutafuta prevention za ki psychology, ambanzo
hazihusiani na mambo ya kishirikina ambazo zinaweza kukusaidia uepukane
na janga hilo nimejaribu kutumia experience yangu ni kama zifuatazo:
Kwanza kabisa kama mwanaume unapoanza mahusiano ya kimapenzi na mwanamke
unatakiwa umwambie mwanamke vitu ambavyo huvipendi na moja katika ya
vitu ambavyo utamwambia hupendi ni mambo ya kishirikina na unatakiwa
umsisitizie kwamba endapo kama wewe utagundua yeye anapenda mambo ya
kwenda kwa waganga umwambie siku hiyo ndio itakuwa mwisho wa mapenzi
yenu.
Jambo la pili ukiwa unaishi na mwanamke ndani usipende kula chakula peke
yako hata kama umechelewa kurudi umerudi labda saa sita usiku mwambie
mke wako mle wote chakula cause peke yako hujazoea kula au kama mna
mtoto wenu ama ndugu wa mwanamke kula nae chakula.
Kwa kufanya hivyo mwanamke atajua hupendi kula peke yako na unampenda
yeye na ndugu zake kumbe unalako moyoni unajilinda na limbwata,jambo la
tatu pendelea kufanya ibada ukitaka kula na ukitaka kulala na
mshirikishe mkeo katika ibada na wakati mwingine msomee maandiko ya
vitabu vya mungu ambayo yanakataza ushirikina na adhabu zake watakazo
zipata wanaofanya mambo hayo,mengine mnaweza mkaongezea.
Note:Mwanamke anaweza akawa sio mshirikina lakini akashawishiwa na
marafiki zake akufanyie hivyo,kwa hiyo kama mwanaume ni bora ukachukua
tahadhari mapema.
No comments:
Post a Comment