Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni
wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo
wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe
kushiriki kwenye mapenzi hayo.
Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda
kupenda na pia tunapenda kupendwa in . Na siku zote ukipenda na
usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine
hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale
mapenzi yanapokuwa machungu kwao.
Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna
mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila
siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na
kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa
maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani
au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.
Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na mpenzi wako
kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote pale
mtakapokuwa na mtakapoishi.
1. Kuwa na muonekano chanya kwa mpenzi wako.
Ukiwa Ni Mtu Wa Kuangalia Mabaya/Kasoro Sana Kwa Mpenzi Wako Kuliko
Mazuri Yake Hautakuja Kukaa Kwenye Relationship Kwa Muda Mrefu Hata Siku
Moja...Utaendelea Kubadilisha Wanaume/Wanawake Kila Siku Na Mwisho Wa
Siku Utajiona Huna Bahati Kwenye Mapenzi Na Wakati Unayeyaharibu Mapenzi
Yako Ni Wewe Mwenyewe...Hakuna Asiye Na Kasoro (Ukiwemo Wewe Mwenyewe).
Kwa Hiyo Muonyeshe Mpenzi Wako Mapenzi Bora Na Umrekebishe Pale
Anapokosea Bila Kuwa Na Lawama Mara Kwa Mara, Kuna Makosa Mengine Ni
Madogo Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na Mpenzi Wako
Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue Kubwa Kwao Na
Kusababisha Mwisho Mbaya.
2. Samehe na kusahau.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa lolote alilokosa basi hakikisha
umemsamehe kiukweli na ujitahidi kusahau kosa alilotenda itasaidia uwe
na amani ya moyo zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu lakini moyoni ukawa
na Donge bado, hii hupelekea kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani kwake
na kujikosesha furaha ya mapenzi.Anapokosea siku nyingine usimkumbushe
kosa lake la nyuma kwa sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na ajione
kuwa hakusamehewa.
3. Mpe nafasi na uhuru mpenzi wako.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa hali na mali kupeana
nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma zaidi na
kimaisha.anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na
umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo
yake.usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka
kwenye biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo
muulize kwa upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana
kurudi au kwenye biashara zake au shuleni tofauti na zamani.
Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na kupayuka mbele yake
na huku yeye akiwa hata hajapumzika na itamfanya siku nyingine aione
nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote wawili.
4. Kuwa mbunifu katika mapenzi.
Napozungumzia ubunifu hapa nakuwa simaanishi kwenye upande mmoja tu wa
kwenye yale mambo yetu ya chumbani, hapana. Hapa namaanisha ubunifu
kwenye mambo mengi ndani na nje ya nyumba, jitahidi mara kwa mara kubuni
vitu vipya vitakavyofanya azidi kukupenda na kukuona kama mpya kwake
kila siku. Kama amezoea kupata zawadi za aina Fulani kutoka kwako basi
jitahidi siku moja kumbadilishia zawadi kutegemea na unavyomfahamu
mpenzi wako anapenda nini na nini. Hakuna anayemjua mpenzi wako zaidi
kuliko wewe kwa hiyo lazima ujue ukifanya nini kwake na kwa wakati gani
atafurahia na kujivunia kuwa nawe.
5. Mfanye mwenza wako ajivunie kuwa nawe kila wakati.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya mpenzi wako ajivunie
kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe miongoni mwa
wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu na kwa
yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye. Wapo wengi
sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo
usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na
kumsumbua.Ukianza kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa
unamkosesha amani ya mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya
mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.
6. Msadie kwa khali na mali kila inapowezekana.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda na kushuka miongoni mwa wapenzi na
hasa kiuchumi na hata kisaikolojia. Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi
kama mtu kupata tatizo na akasaidiwa na mpenzi wake katika hali ambayo
hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako akipata tatizo lolote hakikisha
wewe ndo unakuwa wa kwanza kulifahamu na kulifanyia kazi.
Sio matatizo yote yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri na kumpa mawazo
chanya inasaidia sana na kumfanya awe na furaha kuwa nawe.Kama unampenda
usione tabu kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti unahonga, huyo ni
mpenzi wako kwa hiyo jiamini na umpe kile anachostahili kusaidiwa na
mpenzi wake.
Yapo mambo mengi sana ambayo kama mkiyafanya kwenye mapenzi basi
uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na wenye furaha sana ingawa hapa
nimezungumzia kwa uchache sana lakini nina imani itasaidia sana kwa wote
walio kwenye mahusiano .
Mapenzi hayana ndumba au limbwata hata siku moja, unapoona wapenzi wengi
wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa sababu wanavumiliana kwa mengi na
kusameheana kwa mengi. Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na
Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue Kubwa
Kwao Na Kusababisha Mwisho Mbaya.
Tuesday, June 12, 2018
Kanuni Sita (6) za Kudumu Katika Mahusiano ya Kimapenzi
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment