Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Mimi ni mpangaji nimepanga nyumba moja hapa mjini na nina kama miezi
sita kwenye hii nyumba niliyopanga ambayo mpangaji ni mimi mwenyewe mama
mwenye nyumba ni mjane yaani single mother na ana watoto watatu wote wa
kike.
Kinachonisukuma kuomba ushauri hapa ni nyenendo za huyu mama na binti
yake mmoja yule wa pili, yaani huyu mama anaforce mwanae nimuoe yaani
niishi nae gheto kwangu niwe nalala naye na kuamka naye.
Kila chakula kikiiva naletewa nguo nafuliwa na hadi maji bafuni
napelekewa na wanafanya yote haya si kwamba mimi nataka hapana ni kwa
lazima, yaani chakula unaletewa ki nguvu nguvu kama ni wali unakuwa hadi
ushamwagiliziwa maharage na mchuzi sasa kwa mazingira haya ni vigumu
sana kukataa.
Jana binti kaja usiku kuniletea msosi na hakurudi tena ndani kwao
akabaki hadi asubuhi, mimi leo nimeondoka kwenda kazini nimemuacha gheto
nimerudi nimekuta kapika chakula chetu wawili tofauti na chao kile cha
kwa mama yake.
Sasa kwa staili hii ya kuja gheto Jana usiku na leo nimemkuta kapika si tiari nishakabiziwa mzigo hivi.
Ushauri wenu nifanyaje? Nihame hii nyumba au nifanye nin?
LONDON BABY
Saturday, June 9, 2018
Mama Mwenye Nyumba Anataka Kuniozesha Mwanae Kinguvu Nguvu
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment