Haijalishi ni kwa namna gani uhusiano umeanza au umeisha, kila mara tunapokuwa katika uhusiano lazima kuna somo tunajifunza.
Hakuna uhusiano ambao ni mkamilifu, lazima mtazozana kwa maneno au
vitendo na wakati mwingine kugombana kabisa. Lakini kuzonazna huko
hakumaanishi kwa uhusiano wenu umefikia mwisho, japokuwa mkiwa watu wa
kugombana kila siku, inabidi mkae chini mzungumze kuweza kufahamu tatizo
ni nini.
Kuwa na furaha ni jambo moja, lakini kujua kuwa upo katika uhusiano
ambao utadumu licha ya kuwa mnapitia magumu kiasi gani, ni jambo jingine
ambalo kila mmoja analitamani.
Hapa chini ni ishara saba ambazo zinazungumza kuhusu uimara wa uhusiano wenu.
Mawasiliano
Kikubwa ni kujiuliza mnazungumza kuhusu nini na mna mazungumzo ya aina
gani. Manaweza mkawa mnazungumza kuhusu jinsi ya kufanya maamuzi, tabia
nzuri amba mbaya zinazowakera au kuhusu maisha yenu ya mbeleni.
Chagua muda sahihi na mahala sahihi pakuzungumzia jambo lako, dunia
haitaisha kama ukiamua kusubiri saa moja ili uweze kupata sehemu sahihi
ya kuzungumza na mwenza wako. Fahamu unataka kusema nini, utakavyokisema
na mazingira utakayosemea ili kuwa na mawasiliano madhubuti.
Makubaliano
Hii sio kwenye uhusiano wa kimapenzi pekee, hata kwa rafiki wa kawaida
ni muhimu kuzingatia hili kwani huwezi ukawa kila mara wewe unapokea tu,
lazima pawepo wakati wa wewe kutoa pia.
Mnapoingia katika uhusiano, kila mmoja huwa na tabia zake na uelewa wake
juu ya mambo, lakini wapenzi ambao ni imara, watakaa na kujadili kuona
namna bora ya kuweza kuchanganya tabia zao na kutoka na moja ambayo wote
wataikubvali.
Ukiwa wewe hutaki kubadilika ila unataka mwenzako ndio kila mara
abadilike kufuata mawazo yako, hakika kila mara mtaishia kugombana.
Uaminifu na kusamehe
Vitu hivi viwili ni muhimu sana katika uhusiano wako, kila mmoja
anatakiwa kuweka nguvu sawa kuhakikisha vinaendelea kuwa nguzo muhimu
kati yenu wawili. Usiwe na nafasi ya kuwa na mawazo hasi na mwenzako, na
unapokuwa na wasiwasi, mwambie na yeye akueleza ukweli pasi na kupepesa
macho.
Jifunze kusamehe na kusahau, haiwezekani kwenye uhusiano kila mara nyie
mkawa ni watu wa kugombana tu, mtapata wapi muda wa kufurahia uwepo wa
mwenzio? Samehe na sahau vitu ambavyo hamuwezi mkaendelea kuvijadili.
Haiwezekani mkawa mnaendelea kujadili tatizo lililotokea mwezi uliopita.
Jitambue
Hili huwakumba zaidi wanawake. Wanapoanza kuwa kwenye uhusiano, wapenzi
wao huwa ndio dunia yao. Huwapoteza marafiki zao na kuacha kufanya vile
vitu alivyokuwa akivipenda, na badala yake sasa anafanya vitu ambavyo
mpenzi wake anavipenda.
Hii huwa haitokei sana kwa wanaume, ni mara chache sana utakuta mwanaume
ameacha kuangali mpira kwa sababu tu mpenzi wake hapendi aangalie.
Hakikisha unaendelea kuwa na marafiki, na kufanya vitu ulivyokuwa
ukivipenda hata baada ya kuwa kwenye uhusiano. Hivyo vitakusaidia wewe
endapo chochote kitatokea katika uhusiano wenu. Hata ikitokea mkaachana
na huyo mpenzi wako, bado una marafiki wa kukusaidia.
Wanahitaji kuwa kwenye Maisha yako
Hakuna mtu anayekuwaga ‘busy’ akashindwa kufanya kile anachokipenda.
Kama kweli mpenzi wako anakupenda, atatafuta muda kwa ajili yako bila
kujali ametingwa kiasi gani kwa sababu tu anakupenda.
Na anapotenga muda kwa ajili yako, mkiwa pamoja awepo pale kiakili na
kimwili, sio mwingine akifika anaanza kuchezea simu yake na hakuna
kuongeleshana.
Anakufanya ujisikie vizuri na mwenye furaha
Sio lazima uwe umejiremba ndio mpenzi wako aonyeshe kuvutiwa na wewe,
hata kama ndio umeamka kutoka usingizi au umetoka kuoga na hujajiremba
avutiwe na jinsi ulivyo na hicho kitakufanya ujiamnini na kujiona upo
kwenye mikono salama.
Kuwa na mtu ambaye anakuthamini, anayeijua thamani yako, anayeyaweka
mawazo yako mbele na akikosea hasiti kuomba msamaha, mtu ambaye ukiwa
naye unajisikia Amani kuliko ukiwa na mwingine yeyote.
Kuwa wachangamfu (having fun)
Uhusiano wako ni salama, mpenzi wako ni msaidizi wako, uhusiano wako ni
mbingu ndogo hapa duniani hauna haja ya kujificha na kutojionyesha wewe
ni nani (the real you) ili tu mwenza kwako akukubali.
Ni ninyi wawili tu duniani, Hakuna mwingine, hivyo mnapokuwa na nafasi, furahini, kila mmoja awe huru kwa mwenzake.
Tuesday, June 12, 2018
Mambo 7 Yanayoonyesha Wewe na Mpenzi Wako Mna Uhusiano Imara
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment