Salam enyi watanzania wenzangu.
Mungu kanituma niwaeleze haya mambo mazuri kwa ajili ya kudumisha mahusiano yetu, hasa mke na mume au wachumba nk.
Kwanza kabisa, wanawake wana akili sana katika kututawala sisi wanaume
na wana uelewa na creativity kubwa sana ya kukusoma vizuri mwanaume kila
unachofanya na kila unakokwenda na issues zako zote. Hata kama
hakwambii, elewa anajua kila kitu, anakustahi tu.
Kujiamini ni nguzo muhimu sana kwa sisi wanaume kumkalisha mwanamke
chini, awe billionea, awe professor, awe na cheo nk kwako si kitu kama
mwanaume unayejiamini.
Asijue kitu fulani hujui, asijue kitu fulani huna, asijue kama
umeshindwa mahali. Wanawake hutumia "failures" za mwanaume kuwa
"opportunities" kwao. Atafanya ya ajabu kwakuwa anajua huwezi kitu
fulani, huna kitu fulani, huna uwezo fulani.
Hata kama ikitokea ndani hakuna kitu, mwambie tu 'kuna mtu nimemwelekeza
ataleta hapa nyumbani'. Hata kama huna hela mwambie tu 'kuna jamaa
anatuma sasaivi kwenye mpesa'.
Hata kama huyo mtu asipoleta, huyo mtu asipotuma kwenye simu, we kauka
tu...endelea hivyohivyo kubadili visentensi ili aridhike, huku wewe
unaplan/unastruggle kinyakimya kuhakikisha chochote kuhakikisha mambo
yanakaa vyema.
Usirogwe ukamwambia mwanamke "siwezi, sijui, sina, nitaangalia, ngoja
kwanza, ". Otherwise atafanya anachoweza kuhakikisha anapata kila kitu
na hata kukulisha wewe.
Kujiamini, kujiamini, kujiamini ndo dawa ya 'Eva' huku duniani.
No comments:
Post a Comment