UWEZEKANO wa prodyuza na mfanyabiashara wa masuala ya muziki wa
Marekani, Suge Knight, kwenda kwenye maziko ya mama yake ambaye
amefariki juzi (Jumapili) hospitalini, unazidi kuwa finyu kwa vile
mamlaka ya magereza imesema haiwezi kumruhusu prodyuza huyo kwenda nje
kwa vile anakabiliwa na kesi ya mauaji.
Mama yake Suge aliyekuwa anaitwa Maxine Chatman, alifariki kutokana na matatizo ya kiharusi.
Pamoja na habari kwamba huenda mtuhumiwa huyo akakata rufaa dhidi ya
uamuzi wowote wa kumgomea asiende kwenye maziko hayo, bado inaaminika
kwamba mahakama haitabadili uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment