Mwanasayansi wa Maabara ambaye ni mstaafu katika Serikali ya Kenya Dokta
Moses Njue anashtakiwa katika mahakama ya Meru nchini Kenya kwa kosa la
kuiba viungo vya maiti za Binadamu.
Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Claire Murithi amemshutumu Dokta Njue
kwa kuiba moyo wa Polisi wa zamani wa nchi hiyo Benedict Karau huku
akimshutumu pia kuharibu ushahidi wa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Mahakamani March 12, 2015 yalieleza
kuwa Dokta Njue ambaye ndiye aliekuwa kiongozi mkuu wa uchunguzi wa
maiti katika hospitali ya Consolatha aliiba moyo wa Polisi huyo kabla
haujapelekwa katika shule kwa ajili ya Wanafunzi kufundishiwa.
Katika kesi hiyo ambayo imeendelea kusikilizwa , Dokta Njue amekana
mashtaka hayo huku mahakama ikimtaka kuweka dhamana ya zaidi ya shilingi
Milioni 45 za Kitanzania.
Hata hivyo wakili wa Dokta Njue aliiomba mahakama kupunguza dhamana hiyo
kwa kile alichokidai kuwa mteja wake ni mtumishi wa umma ambapo baadae
mahakama ilimtaka Dokta Njue kutoa zaidi ya Milioni 11 za Kitanzania
kama dhamana.
Saturday, June 30, 2018
Mwanasayansi wa Maabara Ashtakiwa kwa Kuiba Viungo vya Marehemu
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment