Mwanamke mmoja nchini Indonesia ameuawa na kumezwa mzima mzima na chatu mwenye urefu wa mita 7.
Licha ya visa kama hivyo kuwa vichache hiki ndicho kisa cha hivi
karibuni cha mtu kuliwa na chatu nchini Indonesia kwa takriban mwaka
mmoja.
Ni kipi kilimpata mwanamke huyo?
Wa Tiba, 54, alitoweka Alhamisi iliyopita wakati akiwa kwenye shamba
lake la mboga katika kisiwa cha Muna mkoa wa Sulawesi. Shughuli kubwa ya
kumtafuta ilifanywa na wakaazi wa eneo hilo.
Viatu vyake na upanga vilipatikana siku moja baadaye huku chatu
aliyekuwa na tumbo lililofura akipatikana mita 30 kutoka eneo hilo.
Mwanamume aliyetoweka apatikana ndani ya chatu Indonesia
Wenyeji walishuku kuwa nyoka huyo alimuua, kwa hivyo wakamuua na kumtoa shambani.
Tumbo la nyoka huyo lilipasuliwa na mwili wa mwanamke huyo ukapatikana ndani.
Picha za kutisha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini
Indonesia zikionyesha mwili wa mwanamke huyo ukitolewa tumboni mwa chatu
huyo mbele ya umati mkubwa.
Chatu wanashambuaje?
Chatu wa sulawesi wanaweza kukua hadi urefu wa miaa 10 na wana nguvu
sana, Wanashambulia kwa kuvizia, wakijifungia kwa windo lao na kulivunja
kwa kufinya hadi kuua.
Sunday, July 1, 2018
Mwanamke Auawa na Kumezwa na Chatu
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment