Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Sunday, July 1, 2018

Huyu Hapa Binti Mrembo Kuliko Wema Sepetu Lakini Anafanya Kazi Chafu Kujinasua Kimaisha

Bila shaka, kila mtu hutia bidii awe mwanaume au mwanamke ili kujikimu kimaisha. Zaidi ni kwamba, kwa wengi haitajalisha aina ya kazi bora tu kipato kinakidhi mahitaji yake.

Wasomi wengi huzikwepa kazi nyingi kwa madai kuwa ni chafu, za kishamba na zisizowafaa watu walio na shahada, ila wengine huzichukulia kama kazi rasmi na bila shaka kipato chao cha kila siku huwa ndiyo furaha yao.

Binti huyo, Ogechukwu Kate, ambaye alifuzu kwa shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Ebonyi aliamua kuasi daraja lake na kujichafua kwa kazi ya makaa ili kujipa kipato chake

Ni kazi ambayo humpa kipato kikubwa na anayoifurahia kama alivyochapisha katika ukurasa wa Facebook.

Alidai kuwa makaa ni dawa zuri sana kwa ngozi hivyo watu hawafai kuhofia kuhusu ngozi.
"...Usijali kuhusu ngozi kuharibika kwani kwa makaa ni tofauti kwani husaidia kusafisha. Husawazisha mafuta ya ngozi. Kwani huoni vile huwa mchafu na mweusi sana nikiwa kazini lakini safi sana baada ya kuoga," Alisema Kate.  

No comments:

Post a Comment