Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Baba jana, kumekuwa na mwamko mdogo wa watu kusherehekea sikukuu hiyo tofauti na ya Mama.
Jana, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), lilitoa
taarifa yake na kuwakumbusha wazazi wa kiume namna wanavyopaswa
kuzingatia malezi ya watoto wao hasa wakati wakiwa katika umri mdogo.
Siku ya Baba Duniani huadhimishwa kila ifikapo Juni 17.
Unicef ilisema mzazi wa kiume anayejitahidi kuwa karibu na mtoto tangu
akiwa katika umri mdogo, ana nafasi kubwa ya kuwa kichocheo cha
maendeleo ya watoto.
Unicef imesema tafiti zinaonyesha pia watoto wanapokuwa na ukaribu wa
kipekee na wazazi wao wa kiume wapo kwenye mwelekeo mzuri wa kuwa na
afya njema kisaikolojia, kujiamini na kutosheka katika mfumo wa maisha.
Hata hivyo, wanaume wengi waliohojiwa na Mwananchi wamesema tamaduni na
mila za Kiafrika ndizo zimesababisha siku hii isipewe kipaumbele hasa
kwa nchi za Afrika.
“Huku kwetu haya mambo hatuyapi kipaumbele sana kwa sababu nyingi
ikiwamo zile zilizosababishwa na historia ya makuzi yetu. Haya mambo
hatujawahi kuwa nayo hapo kabla....yameingia katika siku za hivi
karibuni hivyo ni vigumu kuwakuta kina baba wakiyachangamkia,” alisema
Walter Tosha baba wa watoto wa wawili na mmoja wa wanaume waliohojiwa.
Mzazi huyo anaelezea uzoefu wake akisema makuzi ya familia za Kiafrika
ni tofauti na ilivyo kwa familia za nchi za Magharibi ambazo mara nyingi
hukulia katika utamaduni wa namna hiyo.
Sunday, July 1, 2018
Wanaume Waeleza Sababu Siku ya Baba Kutokuwa na Mvuto
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment