Mwanamke mmoja nchini Uganda ambapo amekamatwa na Polisi wa nchini humo
kwa kosa la kushirikina na ndugu zake kumuua mume wake na kumzika kwa
siri.
Dina Ainomugisha anadaiwa kumuua mume wake ambaye alikuwa ni mfanya
biashara wa ndizi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi juu ya mali za
familia yao.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ibanda Rogers Chebene
amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa ambaye alishiriki katika zoezi hilo
ambaye hakupata mgao wake wa fedha kama walivyokubaliana ndiye aliyewapa
taarifa jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.
Watuhumiwa wengine walioshiriki katika tukio hilo wametajwa kuwa ni
Keresensio Mwesigye Alias Kamwesi, Experito Kacunguza, Stephen Mukama
pamoja na Medrine Kabasiita ambao wote kwa sasa wametiwa nguvuni na
jeshi la Polisi.
Aidha mwili wa Marehemu umechukuliwa na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Ruhoko kwa uchunguzi zaidi.
Sunday, July 1, 2018
Mwanamke Ashikilikiana na Ndudu Zake Kumuua Mume Wake
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment