Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia inasadikika hakuna kitu
ambacho kina nguvu sana kama mahusiano ya mapenzi, hata hivyo kutokana
na nguvu hiyo ya mahusino, watu wengi husaani mwanaume ndio ambao
wanaathiriwa kwa kiwango kiubwa na nguvu hiyo.
Watafiti wa masuala ya mahusiano wanazidi kusema ya kwamba, mwanaume
kila baada ya dakika tano ni lazima awaze masuala ya kimapenzi, hii ni
kutokana wanaume wengi hupenda zaidi jinsia ya kike kwa kuona kwa macho.
Ndo maana ukichunguza kwa makini wanaume huwa wanakuwa wanazingatia
zaidi katika kutazama jinsia hii ya kike mahali popote walipo.
Hivi hujawahi ona wanaume wamekaa mahali wanapiga stori ghafla akapite
mwanamke mzuri mbele ya macho yao ghafla stori zile zikasimama kwa muda?
Bila shaka umewahi kuona. Utawasikia wakisema kwa minong'ono aaah
angalia kifaa hicho, wapo wengine utawasikia wakisema mcheki chura huyo.
Hii ina maana ya kwamba macho ya mwanaume ndio chanzo kikubwa cha
kuingia katika mahusiano kabla ya kumjua tabia aliyonayo mtu huyo.
Lakini ukweli ambao upo nyuma ya pazia ni kwamba wanaume wengi huingia
katika matamanio ya kimahusiono kwa kuona kwa macho zaidi tofauti na
mwanamke. Hata hivyo mahusiano ya kimapenzi aliyonayo mwanaume ni
matokeo ya macho yako. Kwa maneno mengine tunaweza kusema matamanio ya
hisia za mwanamke yapo katika kuona zaidi kuliko kitu chichote.
Lakini ukienda upande wa pili wa shilingi, mwanamke huwa yupo tofauti
sana ukilinganisha na mwanaume katika suala zima la kuingia katika
mahusiano. Hisia za mwanamke huwa zipo zaidi katika maneno na mguso
katoka kwa mwanaume. Hisia za mwanamke huwa hazipo katika kuona kwa
kiwango kikubwa ukilinganisha na mwanaume.
Mwanamke huamini sana katika maneno ambayo ataambiwa na mwanaume, kwa
mfano mwanamke akiambiwa anapendwa zaidi ya kitu chochote katika dunia
hii mwanamke huamini hivyo,hivyo maneno ya mwanaume yana nafasi kubwa
katika kuziteka hisia za mwabamke.
Lakini pia kama hiyo haitoshi mwanamke hupata hisia zaidi pale
anapoguswa na mwanaume, hivyo ndo maana kama utakutana na msichana kwa
mara ya kwanza atakaa usimguse katika mwili wake, hii ina maana mguso wa
mwanaume una nguvu sana katika kuamsha hisia mwili wa mwanamke.
Hivyo kama ndivyo hivyo basi hii ni uofauti mkubwa ulipo kati ya
mwanaume na mwanamke katika kuamsha hisia za kimapenzi. Na kitu kikubwa
ambacho huongoza hamasa na kudumu katika mahusiona ya kimapenzi ni
"mawasiliano" , mawasiliano ndiyo chachu kubwa katika mahusiano yenu.
Hivyo kila wakati ili muweze kudumu katika mahusiano yenu hakikiasha
unakuwa na mawasilino bora kati yako na mwenzi wako.
Sunday, June 17, 2018
Utofauti kati Ya Mwanamke na Mwanaume Katika Hisia Za Kimapenzi
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment