Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Sunday, July 1, 2018

Fahamu Sifa za Wanawake Wanaopenda Sana Pesa

Hongereni wanawake kwa siku yenu. Tunawapenda Sana kwani ninyi ndio furaha yetu, amani yetu, utulivu wetu. Bila ninyi dunia hatujui ingekuwaje.
Basi baada ya machache hayo nirejee kunako mada.
Siku hizi kumekuwa na ongezeko kubwa la mamilioni ya wanawake wanaopenda Sana pesa kuliko kitu chochote. Jambo hili lilianza Kama mzaha lakini kwa sasa hakuna wakuuzima moto huu.
Kupenda pesa sio vibaya Bali kuipenda Sana kiasi kwamba mtu yupo radhi auze utu wake na kuudharau kabisa uanamke wake. Kama hiyo haitoshi wanawake wengi wanaopenda pesa ndio huwa chanzo cha maangamizi katika familia.
Zifuatazo ni sifa bainifu za wanawake wanaopenda Sana pesa;-
1. Huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima.
Wanawake wengi wapendao pesa huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima, mambo ambayo hayagusi maisha moja kwa moja. Hata nilipokuwa chuo wanawake wengi waliokuwa wanapenda pesa Sana walikuwa na tamaa za kusikitisha ambazo zilipofusha fahamu zao. Unakuta mwanamke anaomba laki tano kwaajili tuu ya kununua Simu nyingine kubwa wakati akiwa bado na simu mpya. 
Katika maisha ni bora uingie jehanam kuliko kukutana na mwanamke mpenda pesa kwani utateseka Sana kwa ajili yake na bado hata ona msaada wako.
Sio rahisi kujenga familia bora na mwanamke mpenda pesa.
2. Wengi hutoka familia masikini.
Wanawake wengi Kama sio wote ambao hupenda pesa kuliko utu wao hutoka familia kame Sana. Ukame wa kiuchumi mpaka kiakili. Wengi wao huweza kutoa hata rushwa ya ngono ili tuu wapate pesa wasijue miili yao inathamani zaidi ya zile karatasi.
Hata humu jukwaani wapo wengi Sana na comments zao zinajulikana.
Wengi huweka matamanio yao hapa jamvini matamanio waliyoyakosa. Mtu ni masikini unandoto za kuwa na mwanaume mwenye pesa nani alikuambia wenye pesa wanataka masikini. 
Umasikini wako usikufanye ujidharau au mtu akudharau. Ndio maana wanawake pamoja na mchango wenu katika dunia hii lakini bado mpaka wanyama hawawaheshimu.
Lipo kundi dogo la wanawake wanaojitahidi kutetea thamani ya jinsia yao lakini wengi wao ni wakuonewa huruma tuu.
3. Wengi wao hawana elimu ya kutosha.
Mwanamke aliesoma akaelimika hawezi hangaika na pesa ya mtu. Ndio maana wanawake wachache huhangaika kwajili ya kujitegemea na sio kumtegemea mwanaume. Wanawake wengi wenye elimu na vipato vizuri huwezi msikie akiongelea pesa Kama kigezo muhimu kwa mwanaume anayemuhitaji awe mume wake. Wengi wa wanawake humu jamvini ambao hujipa matumaini na comments zao za kujiliwaza iwe wanakazi zenye mishahara duni au elimu ndogo sambamba la kutelekezwa na wanaume kwa ukame wao wa akili.
4. Ni wavivu na wasio na mawazo.
Wanawake wote wanaopenda pesa ni wavivu kupita kiasi. Uvivu wao umeanzia akilini kiasi kwamba hawana mawazo ya maendelo. Utakuta mwanamke anawaza mambo mepesi kabisa Kama urembo, nguo, mtoko, n.k.
Wanawake wapenda pesa ni hatari kwa ustawi wa familia.
Huwezi kuwa na familia kubwa ukiingia katika bahari ya viumbe hawa.
5. Hawana shukrani wala uvumilivu.
Wanawake wapenda pesa huwezi msikia akikushukuru zaidi ya kujichekesha tuu na kubinua makalio.
Kwa mfano amekuomba milioni moja then ukampa laki tano basi utamsikia akisema sasa hii nitafanyia nini, au niongezee tena mume wangu huku akikushika kifua au ndevu. Wanawake wenye hekima hushukuru mpaka mwanaume anasikia aibu.
Suala la uvumilivu halipo kwa hawa viumbe. Shida ikitokea ukishindwa kuitatua kwa wakati huo basi hesabu umeliwa. Yaani kwao kukusaliti ni jambo lisilo na mashaka.
Babu aliwahi kunambia;
Usimpe mwanamke pesa yote aombayo.
Wenye wake mmenielewa.

No comments:

Post a Comment