I was single once, but now i'm a wife and a mother. Nimekaa nikaona sio
vibaya iwapo nta-share tips kadhaa zilizonisaidia kumuweka baba watoto
sawa na mpaka leo hii sijawahi kuhisi wala kugundua kwamba anatoka nje
ya ndoa yetu, japo matatizo ya hapa na pale hayakosekani ila tumedumu na
bado tunaendelea na safari.
Unapokutana na mwanaume akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna
uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa na wewe kweli au kakutamani tu. Kitu
ambacho watu hua wanasahau ni kwamba hata mtu aliyekutamani tu unaweza
ukampa mwongozo/sababu mpaka mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko
ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi kupenda. Ndio maana hata wale
waitwao 'bad girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na kunasika at some
point.
1. Usiigize.
Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k
2. Don't move too fast/act desperate.
Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una
malengo gani na mie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/nataka
nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni
mtu wa aina gani, je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa
muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya
kitu hicho hicho.
3.Don't be too demanding.
Huyo sio baba yako wala sio mume just yet, hivyo chochote
atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda kufanya hivyo na sio
kwakulazimika. Haki hiyo hauna.
4. Kuwa na shukurani.
Learn to appreciate all that he does for you, that way ataona umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.
5. Be real.
Badala ya kufika kwake na kuanza kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi
wa ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa anawezaje weka nyumba
yake katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika wewe
utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale wakukaa miguu juu
huku wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.
6. Learn to cook if you don't know how to.
Waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea.
Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi hua
wanajali ladha. Hiyo ndio hua inawaongezea hamu ya kula na kuwarudisha
nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss pale inaposhindikana kula chakula
chako . Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata tumbo lake unaweza
kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye maisha yake.
7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.
8. Kuwa ngao yake.
Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote yale onyesha utayari wa wewe
kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka yatakapoisha. Pia usikose
kumjali kumpa moyo pale unapoona inahitajika.
9. Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano
yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili aamue kama yuko tayari
kudeal nayo au la.
10. Usiwe na chuki.
Kikifika kipindi cha yeye kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake
onyesha ushirikiano. Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba wewe ndio
wewe.
11. Give your all.
Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.
12.Pendeza.
Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi
yako.
13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo yeye.
Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa wewe tu na story/mambo
utakayo wewe. Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf. mpira/siasa.
14.Kuwa mtulivu.
Usiwe mtu ambae kila saa simu yako inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu
wala marafiki wakaribu na wanaoeleweka. Discpline ni muhimu sana.
15.Usimzonge.
Usiwe mmoja wa wale watu wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa
hawapo pamoja. Mpe nafasi ya kuwa na marafiki zake bila kuhitaji kuzima
simu ama ku-ignore simu/text zako.
16. Mfurahishe/chekeshe.
Joke around sio muda wote yeye ndio awe wakukufurahisha wewe.
17. Jifunze kusamehe.
Mambo madogo madogo yanapoombewa msamaha samehe na uache yapite.
18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa kiroho.
No comments:
Post a Comment