Kila ndoa inachangamoto zake na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa
wanandoa kuvumiliana katika changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu
ambazo wanandoa hawawezi kuziepuka lakini kuna zile za kiuanadamua mbazo
nyingi ni za kimakusudi na mtu huamua tu kuwa hivyo. Katika kuangalia
ndoa leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka
kuwa nao;
(1) Wanaojione Kama Wafalume (King Husband); HIi ni aina ya
wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake
zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni
kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka
waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo.
Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi
anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.
(2) Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband); Hii ni
aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya
mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao
wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume
kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza
kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na
marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote
katika ndoa yake.
(3) Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband); Hawa hukasirika kila
mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka
juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na
mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa
kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.
(4) Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband); Hawa wanajifanya
wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke
na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida
akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na
mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia
wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.
(5) Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband); Hawa wanajifanya
wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni
kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali
hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume
sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema
nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi
yoyote kuwafurahisha wekea zao.
(6) Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband); Hawa
huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri
wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka
mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta
vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai
kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama
wanawake, hawajali tena.
(7) Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband); Bado wanatabia
za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu
zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na
kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo
kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu
zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo
kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa
Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.
(8) Mume Mtalii (Visiting Husband); Hawa wanakuja nyumbani kama
wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi
kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana
sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na
marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho
anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya
kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.
(9) Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband); Hii ni
aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu
mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza
anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na
kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye
wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia
huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.
(10) Mwanaume Mbahili (Miserly Husband); Huyu anaweza kuwa na
hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi
yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari
ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia
hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela.
Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na
wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.
Hiyo nji baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa
kuwa nao. Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia
tu. Ndoa ni furaha amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe
kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo na kama ni
mke mezea namba ya mumeo na jua hauko peke yako
Thursday, August 23, 2018
Aina Kumi Za Waume Ambao Wake Zao Wanakereka Kuwa Nao
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment