Mwanadada mmoja katika mji wa Dera Ismail Khan nchini Pakistan
ametembezwa uchi wa mnyama mbele ya mamia ya wanakijiji ili kufidia
adhabu ya kaka yake aliyezini na msichana mdogo kiumri mwaka 2015.
Taarifa kutoka kwenye gazeti la Tribune la nchini humo zinaeleza kuwa
kaka wa msichana huyo aliyetembezwa akiwa uchi, alifanya mapenzi na
binti wa familia nyingine hivyo baraza la kijiji liliamuru kaka huyo
alipe kiasi cha rupia 150,000 za Pakistan sawa na Tsh milioni 2.2 mwaka
jana ili kuyamaliza matatizo hayo kifamilia.
Hata hivyo familia ya Mwanaume huyo mzinifu aliyetambulika kwa jina la
Sajjad ilishindwa kutoa fedha hizo ndipo baraza hilo la kijiji
lijulikanalo kama (Panchayati) lilipotoa hukumu hiyo ya kumtembeza dada
wa Sajjad uchi wa mnyama mbele ya wanakijiji ili liwe funzo kwa familia
nyingine.
Tayari polisi nchini Pakistan wametangaza kuwakamata watu saba kufuatia
tukio hilo la udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia, wengi wa
waliokamatwa ni viongozi wa baraza la kijiji waliotoa hukumu hiyo.
Matukio kama hayo sio mageni nchini Pakistan hii kutokana na msimamo na
maamuzi makali ya mabaraza ya vijiji nchini humo kuwakandamiza wanawake.
Mwaka 2002 kulitokea hukumu ya ajabu kama hiyo ambapo mwanamke mmoja
ajulikanae kwa jina la Mukhtar Mai aliamriwa kubakwa na kundi la vijana
ingawaje alienda kutoa taarifa mapema Polisi.
Mabaraza ya vijiji nchini humo yamekuwa yakitumika kusuluhisha kesi
mbalimbali kwenye jamii huku yakilaumu kuwa mahakama nchini humo ni
dhaifu katika utendaji ingawaje serikali nchini pakistani haitambui
uwepo wa mabaraza hayo.
Thursday, August 23, 2018
Home
/
Unlabelled
/
Mwanadada Atembezwa Uchi Mbele ya Mamia ya Wanakijiji Kufidia Adhabu Ya Kaka Yake Aliyezini na Msichana Mdogo Kiumri
Mwanadada Atembezwa Uchi Mbele ya Mamia ya Wanakijiji Kufidia Adhabu Ya Kaka Yake Aliyezini na Msichana Mdogo Kiumri
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment