Mapenzi yana nguvu yenye mvutano mithili ya sumaku. Hoja hapa ni kuwa
endapo kutakuwa na mapenzi ya kweli, mara nyingi mtajikuta mpo kwenye
mstari mmoja, kwani kuna nguvu ya asili ambayo hamuioni, inayowaweka
pamoja muda wote. Ni nadra kutofautiana.
Ni lazima itatokea mara
chache kutofautiana kwa maana ninyi si malaika. Mantiki ni kwamba hata
kama mnapendana kiasi gani, haiwezekani kila siku wote mkawa mna mawazo
ya aina moja, hivyo mtapingana, japo kutokana na mapenzi ya kweli,
mtapata suluhu mapema.
Kuna
kukosea, kwa hiyo kibinadamu kuna wakati utamkosea mwenzi wako. Ila
uwepo wa penzi la kweli, utasababisha mpate muafaka mapema. Utaguswa
kuomba msamaha, naye atahamasika kukusamehe. Mvuto wako ndani yake,
utamfanya asichelewe kupitisha msamaha. Hayo ndiyo mapenzi.
Ukiona
wewe na mwenzi wako mnatofautiana, suluhu inakuwa ngumu kupatikana, siku
zinapita hamzungumzii tatizo lililowafanya mkawa kwenye sura ya
mfarakano, hapo maana yake kuna mambo makuu matatu, na moja lazima ndilo
litakuwa sahihi.
Mosi; inawezekana umemkosea kitu kikubwa sana
mwenzi wako. Alikuamini mno na hakutaraji kwamba utamfanyia hicho
ulichotenda. Kutokana na moyo wake kuingiwa ganzi, inakuwa vigumu kwake
kuketi mezani kutafuta suluhu, kwani anakosa imani aliyokuwa nayo awali.
Hapa
nikupe angalizo kwamba ni bora uwe huaminiki au imani ya watu kwako iwe
ya wastani. Endapo watu watakuwa na imani kubwa kwako, siku wakigundua
una nyendo chafu za siri, heshima yako hupotea kabisa. Kama huaminiki,
watu watasema ni kawaida yako. Waliokuamini wastani nao watanena hukuwa
ukiaminika asilimia 100, hivyo halitakuwa gumzo.
Unapokuwa unaaminika
kwa asilimia 100, maana yake hakuna shaka yoyote kwa watu juu yako.
Hivyo basi, unapoboronga, heshima yako itashuka kwa kasi. Mitaani
simulizi itakuwa wewe, kwani ni jambo geni na halikuwahi kutabiriwa
kwako. Tafadhali, ishi maisha yako, usiishi maisha bandia. Utaumbuka.
Vivyo
hivyo kwenye mapenzi. Mpenzi wako anayekupenda na kukuamini kupita
kiasi, siku ukimtenda ndivyo sivyo, atakaa na maswali mengi kwa muda
mrefu. Utageuka kinyaa mbele yake, kwa hiyo hata kukusamehe atapenda
kufanya hivyo lakini atachelewa kwa sababu heshima yako kwake, imeondoka
kabisa.
Pili; mapenzi yenu ni kama mnalazimisha. Hampendani kabisa
au yeye hakutaki, kwa hiyo anaona hiyo ni fursa ya kukuadhibu.
Utashangaa umemkosea jambo dogo lakini anavyolisimamia utadhani umeua
mtu. Kama sura ya aina hiyo, inajiri kwenye uhusiano wake, jaribu
kutazama mbele kwa matumaini. Hakupendi, atakupotezea muda.
Tatu; mapenzi yake kwako ni ya wastani. Ulivyo kwake, ukiwa naye ni sawa na hata usipokuwa naye
Saturday, August 18, 2018
HILI NI DARASA HURU, KUCHUJA PENZI HALISI NA MAZOEA
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment