1. Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda kuolewa.
2. Usimsubiri mwanaume mpaka aje ndio uanze kuishi. Unaweza kuishi maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.
3.Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa stress na wewe unaweza kufa pia.
4. Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu
hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kupatia mpenzi....
5. Tengeneza mazingira ya kuilinda afya. Jitahidi Kunywa maji mengi na
Chakula kwa diet achana na viofa ofa vya bure, vimesha waponza wenzio
wengi mpaka sasa.
6. Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya kuongea nawe
7.Usitumie sex kama ndio mzani wa mapenzi. Unaweza ukaachika tuu pamoja na penzi lako taamu.
8. Usiolewe na mtu kwa sababu ya fedha; Utabakia kuwa mtumwa wake
9. Jiongezee ubora wako, Tafuta kazi, Usiwe mpuuzi ukaamini mwanaume atatatua matatizo yako yote.
10. Jiheshimu sana kwa kuangalia namna ya uvaaji wa mavazi yako na
mwonekano wako mbele ya jamii…. Usitegemee kuvaa kimini ukutane na
mwanaume wa suti… wewe utampata wa milegezo na kubana pua tu.
Saturday, August 18, 2018
MAMBO 10 AMBAYO KILA MSICHANA ALIYE SINGLE ANATAKIWA KUYAFAHAMU. CHEKI HAPA
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment