MIONGONI mwa vilio vya wanandoa wengi jijini Dar, mbali na hali ngumu ya
kimaisha inayosababishwa na vyuma kukaza, matatizo ya kiafya na majanga
mengine mengi, ni suala zima la uaminifu kwenye uhusiano wa kimapenzi
na magonjwa ambukizi kwa njia ya ngono.
Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Ijumaa ulibaini kwamba, masuala ya kusalitiana yanazidi kushamiri siku hadi siku.
Imebainika kwamba, wengi waliopo kwenye uhusiano wa kimapenzi, wanalia kutokana na mateso ya usaliti.
Uchunguzi huo ulibaini kwamba, kati ya watu mia mbili, wanaoishi maeneo
ya Sinza, Mwananyamala, Buguruni, Temeke, Mbagala na Kimara waliofikiwa
kwenye utafiti huu, asilimia 75 (watu 151), waliweka wazi kuwahi
kusalitiwa.
Ni asilimia 25 (watu 49), pekee walidai kulisikia suala la usaliti kutoka kwa jirani zao.
Pamoja na sababu nyingi ambazo Ijumaa limeelezwa kwenye utafiti huu,
lakini saluni ambazo zinatoa huduma za masaji zinatajwa kuwa ni chanzo
kikubwa cha usaliti na magonjwa ambukizi.
Katika maeneo hayo yaliyofikiwa, imebainika pia kuwa kati ya mitaa mitatu mpaka minne, kuna saluni moja inayotoa huduma hizo.
UTAZITAMBUAJE SALUNI ZA MASAJI NA HUDUMA ZITOLEWAZO HUMO?
Ijumaa lilikwenda mbele zaidi na kuchimba saluni hizo zinazotoa huduma
za masaji. Lilibaini kwamba, zipo saluni za aina nyingi zinazotoa huduma
hizo.
Zipo ambazo huandikwa jina fulani alafu mbele yake zinatambulishwa kwa
maneno ‘MASSAGE’. Hizi unakuta ni katika nyumba fulani ambazo tofauti na
kibao cha utambulisho unaweza kufikiri ni makazi ya mtu.
Mfano; utakuta kibao kimeandikwa Q Massage ambapo ukiingia katika nyumba
hizo utapokelewa na akina dada warembo, wanaovutia ambao
watakukaribisha na kukueleza aina za huduma za masaji wanazotoa.
Aina hizo ni pamoja na masaji ya kawaida. Hapa mteja anakuwa amevaa nguo
zake, lakini analala kitandani, mezani au kwenye kibaraza maalum cha
kufanyia masaji na anapewa huduma.
BODY TO BODY
Aina nyingine ya masaji ya mwili kwa mwili (body to body.) Katika aina
hii ya masaji mteja anavua nguo zake zote na anayemhudumia anakuwa hana
nguo au pengine amevaa nguo ya ndani tu!
Lakini huduma hii pia hutolewa kwenye saluni za kawaida za kiume zilizopo mitaani.
Katika saluni hizi, nyingi, bila kuwa na mteja unaweza usifahamu kama kuna huduma ya masaji inayotolewa ndani yake.
Unakuta tofauti na huduma ya kunyoa, kuremba nywele kwa mafuta ya aina
tofautitofauti, ndani ya saluni hizo, kuna kichumba maalum chenye
kitanda, meza kubwa au kibaraza kilichojengewa vizuri kwa ajili ya
kufanyia masaji.
NGONO HUFANYIKAJE KWENYE SALUNI HIZO?
Ijumaa lilizungumza na baadhi ya watoa huduma hizo za masaji ambazo kwa
jijini Dar, hutolewa kwa watu wote, wanaume kwa wanawake;
“Mteja anapokuja unaweza kumwambia kuwa masaji ni kiasi fulani, labda
ile ya mwili kwa mwili. Sasa mnapoingia huko chumbani na kuanza kufanya
masaji, kwa kuwa mnakuwa wawili tu na hamna nguo, baadaye anageuka na
kudai kuwa amezidiwa.
“Anakutaka mfanye mapenzi na anakuongezea pesa. Kwa hiyo wengi wetu
unakuta tuna shida na kiukweli kwenye sehemu za masaji, wengine
wanalipwa posho za siku tu na wengine hawalipwi kabisa, ni juhudi za
kila mtu kupata pesa kwa njia yoyote unapopata mteja.
“Unakuta tunashawishika na kufanya mapenzi kwa sababu ya pesa. Mtu
akikolea, anachukua mawasiliano yako na mara kwa mara anakuwa anakuja
kwa ajili ya kupata huduma, wakati huu unakuta hataki masaji tena, bali
ngono tu,” anasema Amina, mtoa huduma ya masaji kwenye nyumba moja
iliyopo maeneo ya Sinza-Kwa Remmy.
Je, ni kwa kiasi gani huduma hii ya ngono imeshamiri kwenye saluni hizi?
Ni kweli kuwa machangudoa kwa sasa wamekimbilia kwenye saluni hizi?
Hayo na mengine mengi usikose toleo lijalo.
GPL
Saturday, August 18, 2018
Hivi Ndivyo..Saluni za Masaji Zinavyovunja Ndoa Dar es Salaam
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment