Geita. Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtumishi wa mgodi wa
GGM, Milembe Suleiman anayetuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi
moja.
Mfanyakazi huyo ambaye ni ofisa ugavi kitengo cha manunuzi anashikiliwa
baada ya ‘video’ inayomwonyesha akimvisha pete ya uchumba mwanamke
mwenzake kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Video hiyo ambayo imezua mijadala hasa ikizingatia kwamba iko kinyume
cha utamaduni wa Kitanzania na Serikali ambayo imekuwa ikikemea na
kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsi moja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wanamshikilia kuwa uchunguzi kwa kuwa nchi hairuhusu mambo hayo.
Ofisa Habari wa GGM, Dili Tenga amesema hayo ni masuala binafsi ya
mfanyakazi hivyo wao kama mgodi hawawezi kuyazungumzia lakini
wanaviachia vyombo vya dola viendelee na uchunguzi wake.
By Rehema Matowo, Mwananchi rmatowo@mwananchi.co.tz
Saturday, August 18, 2018
Home
/
Unlabelled
/
Kimenuka..Polisi Wamshikilia Mwanamke Aliyemvika Mwenzake Pete ya Uchumba Baada ya Video Kusambaa
Kimenuka..Polisi Wamshikilia Mwanamke Aliyemvika Mwenzake Pete ya Uchumba Baada ya Video Kusambaa
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment