Katika Sanaa Ya Kutongoza, mwanaume huwa ndie anapaswa kumuaproach
mwanamke . Na katika mchakato huo huwa kuna mambo mawili ambayo
anatarajia: unaweza kutumia nguvu zako zote kwake mpaka akakuona kuwa
wewe ni mtu mlafi wa mapenzi na akakutoroka. Na pia ukienda polepole
kwake anaweza kukuambia kuwa wewe ni mzembe wa mapenzi. Huna mshiko wa
kuonyesha kuwa una haja ya kupenda. Kwa mambo haya mawili, wanaume wa
kazi husema, “Wanawake, kuweni na msemo thabiti, hatutaki kuzungushwa.”
So hivi ni kweli kuwa wanawake wanapenda kufukuziwa?
Jibu ni ndio. Lakini kueleza kimahususi ni kuwa wanawake wanapenda
kufukuziwa na wanaume ambao wameteka interest ama hisia zao. Kwa
wanawake inakuwa rahisi kuwavutia wanaume bila tatizo ukilinganisha na
wanaume.
Na kwa sababu ya hili jambo, wanawake mara nyingi huhakikisha kuwa
wanawazungusha wanaume mpaka ule wakati atapata anayemfaa. Wanafanya
hivi ili kuangalia iwapo mwanaume lengwa anaweza kukeep mwendo wake.
Anakupima iwapo unafaa kutoka deti na yeye. Wanawake hawawezi kukuambia
moja kwa moja kuwa wanakupenda, badala yake wao hutumia ishara fioa ili
ugande kwake.
Ishara zenyewe za kutaka umfukuzie ni kama fuatazo:
#1 Anakuwa mpole na mkali wakati sawia. Wanaume wengi
washakumbana na mwanamke ambaye anakasirika na kuwa mpole wakati sawia.
Ni ule wakati ambapo anaonyesha dalili ya kuwa rafiki yako na pia
anaanza kukurushia mistari lakini wewe kwa upande wako ukijaribu
anakufokea na kukukaa mbali na kukuona kama nuksi ghafla.
Ukiona jambo kama hili linakufanyikia usiwe na wasiwasi. Mwanzo shika
virago vyako uende zako. Kwa akili yake hajakukasirikia bali anajaribu
kukupa ishara ya kuwa anataka umfukuzie.
#2 Anajibu mesej zako haraka kama fastjet. Wakati mwanamke
anajibu mesej zako haraka sana wakati wowote ule wa siku basi hio ni
ishara ya kuonyesha kuwa anataka kuskia zaidi kutoka kwako. Inamaanisha
kuwa amependezwa na wewe na anataka uendelee kuwasiliana na yeye mara
kwa mara.
#3 Yuko tayari kukubali mialiko yako. Kama mwanamke hataki stori
zako, basi kwa kawaida kwa haraka ukimwambia umtoe out ama matembezi
atakataa. Mara nyingi atakwambia kuwa yuko busy muda wote na hana nafasi
ya kutoka out na wewe. Lakini, kama kuna mwanamke ambaye anakuzimia na
anataka umfukuzie, atatafuta njia ya kuhakikisha kuwa anakuwa na nafasi
ya kuitikia mialiko yako, hata kama ni kuvunja mipango yake ya wikendi.
#4 Anakuwa makini na mwonekano wake anapokuwa na wewe. Utamshika
pale wakati amevalia mavazi ya kawaida tofauti na vile ambavyo huvalia
mkiwa nyinyi wawili. Kuvalia urembo ambapo kunaonekana si eti anavaa ili
ajifurahishe, la. Huwa anavalia hivyo ili kuteka atenshen yako. Hivyo
ni wewe tu unangojewa uchukue hatua ya kubadilisha kila kitu.
#5 Anakuwa na mazungumzo ya maana mnapokuwa pekeenu. Hapa
haimaanishi atazungumzia kuhusu udaku wa Wema Sepetu ama Vera Sidika,
bali mwanamke ambaye anataka afukuziwe atazungumza na kugusia maisha
yake ya kibinafsi kwa kuongea maswala muhimu. Anataka uwe na shauku ya
kutaka kujua maisha yake ya ndani ama kuzimu.
#6 Anakutesa. Kutesa kunaweza kumaanisha mambo mengi na tofauti
tofauti. Lakini kama unaona anakutesa kiasi, ni ishara ya kuonyesha kuwa
yuko huru na wewe na unapaswa kujiandaa kukeep company tofauti na vile
ambavyo umezoea, yaani anakukaribisha katika himaya yake ya binafsi. Hii
inachukuliwa kama hatua moja kuu ya kusongea mbele katika approach
yako.
#7 Anawasiliana na wewe kama umekatiza mawasiliano. Kuna wakati
mwingine kumfukuzia kunachosha na unaamua kutulia kiasi. Na mara kwa
maajabu ya Musa, unaona mambo yameenda sengemnege, na unamwona anaaza
kuanzisha mawasiliano na wewe.
Huu si uchawi bali ni ishara ya kuonyesha kuwa ameingiwa na wasiwasi wa
kuwa unashindwa. Hivyo anakupa ishara fioa kukuambia kuwa unapaswa
uendeee kumfukuzia.
#8 Anakuwa na tabia isioeleweka wakati mwingine. Wakati mwingine
mwanamke atakupa jibu usilolitarajia kamwe, ama wakati mwingine unajiona
uko pekeako ukiwa na yeye. Kuonyesha tabia tata kwa mwanamke huwa ni
mbinu ya kijanja ambayo wanawake hutumia ili kukupima iwapo unaweza
kutoboa katika maisha yao. Pia huongeza romance ndani yake.
#9 Analilenga lile swali kuu. Wakati mwingine inaweza kufikia ule
wakati wa kumuuliza swali la iwapo yuko tayari kuingia katika uhusiano
na wewe ili muwe kitu kimoja.
Na wakati unapomuuliza swali hilo analenga, ama anajaribu kuleta mada
nyingine tofauti. Si eti kuwa hataki kukujibu, la. Tunajua mwisho
atakubali kukujibu lakini kwanza atajaribu kukuzungusha huku na kule ili
kujipa time. Hili ni jambo la kawaida kwa wanawake so kuwa na subra
kiasi.
#10 Hatangamani na wewe sana lakini anakwambia kuwa anakumiss.
Hii wakati mwingine inachosha akili. Ukimwambia mtoke out pamoja anaweza
kukuambia yuko busy na hana nafasi lakini anakwambia kuwa anakumiss.
Kama ni kweli anakumiss basi anapaswa kutangamana na wewe mara kwa mara.
Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa anataka umfukuzie.
#11 Anakuuliza kama umemmiss. Anapenda sana kukuuliza swali hili
mara kwa mara. Njia nzuri ya kumjibu ni kumwambia kuwa unammiss na
unataka utoke out na yeye. Kumwambia hivi kutamwacha na bila jibu bali
kukubali.
#12 Anajifanya mgumu kumpata. Wanaume huwa na uhusiano wa
penda-chukia kwa wanawake ambao wanajifanya ni wagumu. Mara nyingi kile
wanachosema huwa hawanaanishi walichonacho akilini mwao. Anaweza kusema
kuwa hajavutiwa na wewe lakini maneno na miondoko yake inasema tofauti.
Ukiona mwanamke anaonyesha tabia kama hizi basi jua kuwa anataka
umfukuzie.
Je ushakumbana na mwanamke aina hii? Kama ndio basi usikate tamaa. Tia bidii mwisho utafualu.
Monday, August 20, 2018
Ishara Za Kuonyesha Kuwa Mwanamke Anataka Umfukuzie
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment