kija katika maswala ya udhaifu katika mwanamke, huwa kuna baadhi ya mambo ambayo huwa tofauti katika kila mwanamke.
Hebu mwanzo tuanze kwa kusema kuwa kila mwanamke yuko tofauti. Si kila
mwanamke anataka kitu kimoja kwa kila mwanaume. Lakini, kuna baadhi ya
mambo ambayo huwa yanajitokeza juu zaidi katika udhaifu wa mwanamke.
Kama mwanaume atafanya mambo vile ambavyo inahitajika, basi itakuwa
vigumu kwa mwanamke kuukwepa mtego.
Mambo ambayo haswa huwafanya wanawake kuvutiwa na wanaume huwa ni tabia
flani ambazo hujitokeza. Hii ni kumaanisha kuwa kila mwanamke huwa
amemakinika zaidi kwa mambo ambayo mwanaume hufanya tofauti na sura
yake.
Wakati unapotongoza mwanamke lazima ujenge connection ya kihisia zaidi.
Hii ni kwa sababu kujenga muungano wa kihisia na mwanamke hudumu zaidi
ukilinganisha na umbo lako. Kile kitu ambacho unahitaji zaidi katika
mahusiano yako ni kuwa na muungano wa kihisia.
Kama kweli unataka kumvutia mwanamke, unahitaji kuwa mdhaifu wake. Kama
atashindwa kujizuia na kuvutiwa kwako, basi utakuwa na nafasi rahisi ya
kuuteka moyo wake. Lakini kwanza, unapaswa kujua ni nini haswa
kinachochangia hadi mwanamke kuwa mdhaifu mbele yao. Haya hapa ni mambo
ambayo humfanya mwanamke kuwa mdhaifu.
#1 Kuwa mkarimu wa ukweli. Hauwezi kufeki jambo hili. Wanawake
kwa kawaida huvutiwa na wanaume ambao wanaonyesha ukarimu wa ukweli.
Ukiwa mkarimu kwa wengine, itamuonyesha mwanamke vile ambavyo
utamchukulia. Huu ni udhaifu mkuu kwa kila mwanamke.
#2 Tabia za usaidizi. Udhaifu wa kila mwanamke ni kuwa na
mwanaume msaidivu. Wakiwa wanapewa sapoti na mtu, huwa kawaida
wanavutiwa na mtu kama huyo. Kuna kitu ambacho hujitokeza ndani yako
wakati kuna mtu anajitokeza na kukusaidia katika maisha yako. Kwa
mwanamke huwa maradufu. Usaidivu wako kwa mwanamke kunamfanya awe dhaifu
kwako.
#3 Kushangilia mambo anayotimiza katika maisha yake. Kwa
kuongezea usaidivu wako, wanawake hupenda mtu ambaye anafurahia na
kushangilia mambo ambayo anatimiza maishani mwake. Wakati wamepandishwa
cheo kazini ama amemaliza kufanya mradi wake, kukiwa na mtu karibu yake
ambaye atashangilia mafanikio yake kila wakati ni jambo ambalo kila
mwanamke anatamani.
#4 Kupendezwa na hamu zake. Hii haimaanishi kuwa udhaifu wa kila
mwanamke ni kuiga kila kitu ambacho anapenda, la. Hii ni ile hatua
ambayo unakuwa na interest na mambo muhimu ambayo huyapenda zaidi katika
maisha yake. Kwa mfano ukimwona mwanamke anapenda sana mchezo wa
magongo ama anapenda kufuatilia maisha wa wasanii aina flani, basi wewe
jifunze kucheza mchezo wa magongo na pia uanze kuwatambua wasanii
husika. Akiona kuwa unapenda mambo ambayo anapenda utakuwa
umemdhaifisha.
Haya ndio mambo muhimu ya kuzingatia kama unataka kumfanya mwanamke
adhaifike mbele yako. Kando na mambo hayo manne makuu unapaswa kujihami
na mambo haya ambayo yatakufanya uuteke moyo wake:
#1 Lazima uwe mmakinivu na maswala yake ya ndani. Wakati mwingine
wanaume huchoshwa kusikia malalamishi ya mwanamke lakini siri kuu ya
kumteka mwanamke ni kuwa msikivu kwa kila kitu anachokuambia coz
atakuona kama jangina wake wa maisha.
#2 Mpe saport kwa kila kitu. Kuna wakati anaweza kuongea mambo
ambayo kwa msingi unaona kuwa hawezi kutimiza. Akifikia hapo wewe
unapaswa kunyamaza tu. Unapaswa umpe sapoti kwa kila kitu. Haijalishi
kama unamuelewa au la, unapaswa umsaidie tu. Bora tu mambo yake
anayojaribu kutimiza hayamdhuru yeyote ama yeye mwenyewe.
#3 Muulize maswali. Unaweza kuona labda jambo hili halina maana
yeyote. Lakini ukiwa unamuuliza maswali mara kwa mara kuhusiana na
miradi yake ama mambo anayofanya siku baada ya nyingine utakuja
kumuelewa zaidi. Hii itasaidia kwa sababu atakuona unajihusisha na
maswala yale ya maisha hivyo atavutiwa na wewe na utatumia swala hili
kama udhaifu wake.
Upo!?
Monday, August 20, 2018
Jinsi Ya Kumdhaifisha Mwanamke Ili Akupende
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment