Nimeficha ficha haya mambo ila najiona kabisa naangamia hivyo ni bora
leo niombe ushauri maana hapa pana watu wazima, wanasaikolojia na
viongozi wa dini.
Mkasa wangu ni wa hakika na bado nipo katika mateso hata sasa.
Wakati nipo balehe nilikutana na wasichana mbali mbali waliouteka moyo
wangu na nikawaeleza hisia zangu, kwa bahati mbaya nilijibiwa karaha na
kutoswa sababu ya maisha yangu ya dhiki.
Hali ilikwenda hivyo kwa muda mrefu mpaka moyo wangu ukajenga chuki na
wanawake, niliwaona hawana usawa na sio wa kuwa nao karibu.
Katika utafutaji wangu wa maisha ghafla mambo yakabadilika na nikawa
nina pesa na kuishi vizuri na nikaanza kujenga nyumba na pia nikawa na
miradi pamoja na gari ya kutembelea.
Ni hapo ndipo wasichana wakaanza kuwa karibu na mimi na kunihitaji
kimapenzi, na mimi nilishajenga chuki moyoni na nikapanga kuwakomoa,
nikajikuta natembea na wanawake wengi tofauti kuanzia wanafunzi, walimu,
wasichana tu wa mtaani, machangudoa na wapenzi wa watu.
Nikajikuta dhaifu mbele ya wanawake yaani siwezi kulala hata siku moja
peke yangu bila mwanamke na pia mda mwingine nilifanya mapenzi na
wasichana wawili tofauti kwa siku moja, haswa kama huyo wa pili
aliyenitafuta ni mzuri sana.
Haya mambo sipangi bali najikuta tu inatokea na kila nikimaliza najuta
na kusema ndio mara ya mwisho ila punde tu naingia katika vishawishi
tena, nilioa mke safi kabisa ili niepuke hali hii ila tuliachana baada
ya kunifumania mara kadhaa.
Sasa nina mke mwengine na safari hii nimeoa mke wa ndoto yangu mtoto
mzuri sana shombe shombe kiasi kwamba marafiki wanasema kweli mwamba
umepata kifaa.
Ila bado ninajikuta natembea na rafiki zake pia wasichana wa mtandaoni
kama vile Jf, Badoo, Fb nk na pia nimekuwa maarufu madanguro mengi sana
mpaka naona noma.
Mara kadhaa nasafirisha mademu wakali toka mikoa tofauti na kunifuata
mimi, sihongi sana na wala sijatetereka ki uchumi na wala sijaathirika
ila tu najiuliza nini kipo nyuma ya nguvu hii inayonishinda kujizuia?
Kilichonifanya nijione naingia katika hatari ni kwamba, juzi kushinda
jana nilikwenda guest na msichana fulani nilikutana nae juu juu tu,
tukafanya mapenzi na tulipomaliza wakati tunatoka kuna jitu la miraba
minne lilikuwa likituangalia sana na yule msichana akashtuka sana.
Baadae nilipomuuliza akasema yule jamaa anafanya kazi na mume wake ni FFU kitengo cha doria.
Hakika nikaona hiki ni kifo cha wazi sasa na nimefikia pabaya, haya mambo sipangi ila imekuwa kama ulevi na siwezi kuacha.
Naombeni ushauri wa kunijenga wadau
Friday, August 24, 2018
Nina Mke Mzuri ila Nimekuwa Mtumwa wa Wanawake
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment