Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Friday, August 24, 2018

Naacha Buku 15 za Matumizi Kila Siku Home ila Nakuta Amepika Ugali na Dagaa au Matembele...

Nimevumilia vya kutosha hii tabia sasa naona itakua imefika kikomo.

Naishi na mpenzi wangu hatujafunga ndoa tatizo nashindwa kumuelewa kila siku niendapo kazini na kurudi jioni lazima nimuachie elfu kumi na tano 15,000/-kusudi nikirudi jioni nikute mezani kumependeza nadhani mmenielewa cha ajabu jamani nakuta ugali na dagaa akibadili sana tembere kaomba kwa jirani

Huu ni ungwana jamani? kumuambia nashindwa naona kama takua naingilia mambo ya jikoni ambayo hayanihusu na nisipokula huo ugali ananuna, pia kesho yake nisipo acha hela nikirudi hatuongea mnuno mwanzo mwisho

Sielewi nifanyeje na Nilikuwa nafikiria Kumuoa

No comments:

Post a Comment