SUALA la kuoa lipo tu licha ya kwamba wapo wanaochelewa kuingia kwenye
maisha hayo wakihisi inaweza kusitisha furaha ya maisha yao. Nasema
hivyo kwa kuwa najua wapo wanaoamini kuoa ama kuolewa ni kujiingiza
kwenye matatizo.
Dhana hiyo haina mashiko kiviile, asikuambie mtu unapoingia kwenye ndoa
na mtu anayekupenda na wewe unampenda kwa dhati, karaha hakuna licha ya
kwamba kugombana kwa hapa na pale hakuwezi kukosekana.
Hata hivyo, nikiri tu kwamba, zipo ndoa ambazo ni ndoano. Yaani unakuta
mtu kaingia kwenye ndoa na mtu ambaye hakuwa amedhamiria, matokeo yake
kadiri siku zinavyokwenda anahisi ameingia chaka na anaishia kuomba ndoa
isiwepo.
Leo nataka kuwazungumzia wanawake ambao ni majanga na ukijichanganya ukaingia nao kwenye maisha ya ndoa, utakiona cha mtemakuni.
10. Asiyeridhika na penzi unalompa
Wapo wanawake ambao wewe unaweza kujitahidi kumpatia mapenzi kadiri
unavyoweza lakini yeye hatosheki. Anakuchukulia wewe ni dhaifu sana na
wakati mwingine kuhisi yupo mwingine anayeweza kumpa zaidi ya kile
unachompa, huyu ni tatizo.
9. Wivu kupindukia
Hatukatai, wivu ni muhimu sana kwenye suala la mapenzi lakini kuna ule
wivu uliopindukia kiasi cha kuwa kero. Walio kwenye ndoa wananielewa
namaanisha nini.
Kwa kifupi mtu mwenye mapenzi ya dhati na mwenziye lazima awe na wivu
lakini ukiwa na ule wa kupinduki ni tatizo linaloweza kuitibua ndoa.
8. Anaona unamsaliti kila mara
Huku kunatokana na kutokujiamini tu. Ukioa mwanamke ambaye kila wakati
unapokuwa mbali naye anahisi unamsaliti, huyo hakuamini na kamwe
hamuwezi kudumu. Mara kadhaa mtakuwa mkigombana akihisi una mwingine
kumbe hakuna ukweli katika hilo.
7. Anahisi amekosea kuwa na wewe
Wapo wanawake ambao wanapoingia kwenye ndoa baada ya muda wanahisi
wamekosea kuolewa na mwanaume huyo. Unakuta mke wa mtu anahisi fulani
ambaye zamani alikuwa kwenye uhusiano naye angekuwa sahihi zaidi baada
ya kuona upungufu fulani kwa huyo aliyemuoa.
6. Yuko kimasilahi zaidi
Kuna wanawake ambao ukiwaoa wanakuwa na furaha na wewe ukiwa unazo tu,
ukiishiwa wanaanza kununa na kuleta visirani vya hapa na pale. Hawa ni
tatizo, mwanamke wa kweli ni yule anayeridhika kuwa na wewe kwenye shida
na raha
5. Yuko tayari kuachana na wewe
Hivi hujawahi kumsikia mke wa mtu akimwambia mumewe; ‘Kama vipi
tuachane, kwanza kwetu sijafukuzwa na nilikuwa nakula, nalala, navaa.”
Mwanamke anayeweza kumtamkia mume wake maneno haya, huyo si mke na kamwe
hawezi kukufanya uwe na furaha.
4. Hapendi ndugu zako
Waswahili wanasema ukipenda boga, penda na ua lake. Kama utatokea kuoa
mwanamke ambaye anakupenda wewe tu lakini akija ndugu, rafiki au mtu
mwingine wa karibu yako anabadilika, huyo ana matatizo kwani atakufanya
utengwe na jamii yako.
3. Anajali mafanikio binafsi
Siku zote wawili waliotokea kupendana wakioana wanakuwa mwili mmoja hivyo lazima watakuwa wanawaza na kufanya maamuzi pamoja.
Ogopa sana mwanamke anayependa kutumia kipato chake kufanya mambo
binafsi tena kwa siri. Kwa mfano kusaidia kwao, kujenga nyumba kwao,
kuanzisha miradi yake bila kukushirikisha.
2. Eti akizaa utamzeesha
Hili kwa wale wanaopenda kuoa masistaduu. Wapo ambao wakitajiwa suala la
kuzaa mara baada ya kuingia kwenye ndoa wanagoma wakidai eti
watazeeshwa hivyo waachwe kwanza wale ujana. Wakati huo unaweza kukuta
mwanaume anataka mtoto ili apate ile heshima, mke anagoma kwa sababu
hiyo isiyo na msingi, hili ni tatizo.
1. Anataka awe na sauti
Mwanaume siku zote atabaki kuwa kiongozi wa familia lakini wapo baadhi
ya wanawake hawataki kukubaliana katika hilo. Wengi wanalazimisha usawa
na wengine wakitaka wao ndiyo wawe na sauti kuliko wanaume zao
Thursday, October 18, 2018
Fahamu Sifa za Mwanamke Asiyefaa Kuolewa Asilani
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment