Kuingia
katika mahusiano mapya ya kimapenzi ama uchumba huwa ni furaha lakini
pia inakuweka katika wakati mgumu pia. Unaingiwa na hisia ambazo
hujawahi kuwa nazo, Mpenzi wako anakufurahisha na wewe pia
unamfurahusha.
Lakini
inaweza kuibuka sitofahamu wakati ambapo wewe hutaki ama hujiskii
kufanya mapenzi, kwa sababu unataka kuendelea kuwa mwaminifu mpaka siku
ile ya ndoa ama sababu yoyote ile nyingine, unayo haki ya kujizuia
kutofanya tendo la ngono mpaka ile siku mtakayo funga ndoa na kuwa mwili mmoja. Uwe mwanamke ama mwanamme kumbuka mwili ni wako na maamuzi ni yako.
1. Usilale kwake
Iwapo
hautaki kufanya mapenzi na mpenzi wako, basi ni vizuri usijiingize
katika hali ambazo zitachangia nyinyi wawili kuingiwa na hamu ya
mapenzi. Iwapo umetoka deti na mpenzi wako, usijaribu kumsindikiza hadi
kwake ama kuenda njia moja. Pia hutakiwi kuwa unazunguka sehemu ambazo
mpenzi wako anaishi wakati kama huo kwa sababu inaweza kuchangia pakubwa
kuingiwa na tamaa.
2. Usiwe mlevi
Kuna
baadhi ya watu wanafikiria ya kuwa matumizi ya vinywaji ukiwa na mpenzi
wako inapunguza hisia za kufanya mapenzi. Well, labda inaweza kuwa ni
kweli lakini kulingana na utafiti ni kuwa mtu mlevi anapoteza mwelekeo
wa kufanya maamuzi yafaayo. Hivyo ukiwa umeathirika na ulevi pamoja na
mpenzi wako, kuna asilimia kubwa ya kufanya maamuzi ambayo si sawa.
3. Toa visababu ambavyo havitomkwanza mpenzi wako
Unaweza
kutoa visababu kama vile unaumwa na kichwa, hujiskii vizuri nk. Ingawa
kutumia uongo kwa mpenzi wako si jambo zuri, ni muhimu sana iwapo
itakuja kwa maswala ya kufanya mapenzi ama kama hujiskii kufanya mambo
mengine ambayo yanahusiana na wewe. Hivyo ni muhimu kupatia mambo
mengine kipao mbele.
4. Fungua roho yako
Hii
ndio njia nzuri zaidi kujizuia kutofanya mapenzi. Kukaa na mpenzi wako
katika kikao na kumueleza ndani na nje kuhusiana na wewe kujizuia
kutofanya mapenzi ni jambo nzuri zaidi kwa nyote wawili. Kumueleza
ukweli mpenzi wako kutatoa ile nafasi ya kwako kuonekana kama unayapenda
mahusiano yenu na hauhitaji kuficha ama kudanganya katika mahusiano
yenu.
Iwapo
atakubali basi itadhahirisha ya kuwa yeye anatilia maanani mahusiano
yenu. Kama atakataa basi bila shaka mahusiano yenu hayatokuwa marefu
Monday, October 22, 2018
Jinsi ya Kujizuia Kufanya Mapenzi Katika Mahusiano Mapya
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment