Awali katika machapisho yetu tumeshawahi kuzungumzia swala ya mbinu ya
kumkontrol mwanamke kama rimoti kwa kutumia mbinu ya ‘nanga’. Well, leo
kama Nesi Mapenzi tumemua kuiweka wazi mbinu ya ‘utabiri’ kama moja wapo
ya Sanaa Ya Kutongoza ambazo tumekuwa tukizichapisha hapa.
Ok, hebu tuanze kwa kuuliza maswali. Je ushawahi kuwa na girl friend?
Kama huna girlfriend mpaka siku ya leo unangojea nini? [Soma: Jinsi ya kupata mpenzi haraka]
Na kama umekuwa na girlfriend muda huu wote, je wewe na huyu girlfriend
wako mnaishi vipi? Je mnazozana, mnakosana, ama hamuelewani?
Katika mahusiano haswa inapotokea kuwa nyote wawili mnapendana lakini
kuna mmoja wenu hajaridhika na mwenzake basi mara nyingi ukifanya
uchunguzi utakuja kugundua kuwa mmoja kati ya nyinyi wawili huwa ana
mchepuko/ mpango wa kando.
Na mara nyingi inauma sana iwapo huyo ambaye anakuwa na mpango wa kando
ni mpenzi wako, na mbaya zaidi ni pale ambapo bado unampenda huyu mpenzi
wako.
Kwa kueleza kifupi ni kuwa umegundua kuwa mpenzi wako ana mpenzi wa
kando na wewe hujaridhika na hio hatua ya yeye kutaka kukuacha na
kumfuata huyo mwingine.
Ikifikia hapa utachukua hatua gani ili asikuache? Hapa ndipo hii mbinu ya ‘utabiri’ inaingia kati.
Hebu tuuchukulie huu mfano. Wakati mteja ameingia katika duka flani
anataka kununua bidhaa lakini hajaridhishwa na bidhaa anazoziona na
anataka kuenda katika duka la pili huwa mhudumu kwa kawaida hamkatizi
tamaa yake ya kuenda katika duka la pili bali humpa mawazo na hutabiri
kile ambacho atapatana nacho katika duka la pili. Kwa kawaida
atamwambia, “Jiskie huru kuenda katika duka flani na flani , lakini
kumbuka kuwa maduka hayo huwa bei zao ziko juu kupita kiasi, ama
hutapata bidhaa mahususi unayotafuta, ama utadhulumiwa nk.
So, huyu mhudumu amefanya nini hapa? Rahisi! Kama huyu mteja
ameshawishika na kuamua kubaki hapo, atakuwa ameshinda. Kama huyu mteja
ameamua kuenda katika duka la pili, na kugundua kuwa kile alichoambiwa
ni kweli na kurudi tena, atakuwa pia ameshinda. Na kama ataenda na
hatarudi, basi hakutakuwa na utofauti wowote kama vile awali.
Sasa hebu fikiria kidogo jinsi ya kuitumia mbinu hii kwa girlfriend wako
ama kwa mpenzi wako. Unaweza kutumia hii mbinu kumvunja nguvu iwapo
kuna mwanaume flani yeyote pale ambaye anamtatiza kihisia.
Kwa mfano unaweza kumwambia, “Uko huru kuendelea na yeye, ni kawaida,
inakubalika. Lakini najua kufikia hadi sasa umeshagundua kuwa huyo
unayemfuata ana tabia ambayo si nzuri kwako, tabia ambayo inakutatiza na
kukusumbua... na utapata kugundua tabia nyingine mbaya zaidi kadri
ambapo utazidi kuendelea kuwa na yeye.”
Hapa moja kwa moja atajaribu kuvuta taswira za tabia zozote mbaya ambazo ashawahi kuzishuhudia kutoka kwa huyu mwanaume.
NB: Kumbuka utabiri unaoutoa hapa utakuwa hauna uhusiano mmoja
kwa moja na huyu mwanaume bali unasema na kubahatisha tu. Lakini kwa
mwanamke atadhania kuwa tayari unamjua huyu mwanaume na tabia zake.
So moja kwa moja kama huyu mwanamke kweli ana hisia kwako anaweza kubadili msimamo wake na kukubali kuendelea na wewe.
Upo!?
Saturday, October 6, 2018
Home
/
Unlabelled
/
Jinsi Ya Kutumia Mbinu Ya Utabiri Kumvunja Nguvu Mwanamke Ili Abaki Na Wewe Milele
Jinsi Ya Kutumia Mbinu Ya Utabiri Kumvunja Nguvu Mwanamke Ili Abaki Na Wewe Milele
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment