Kila siku mara moja au nyingine huwa tunawatext wanawake. Aidha wawe ni
wapenzi wetu, tunaowatongoza ama marafiki zetu. Na kila siku huwa
tunapatwa na changamoto mbalimbali kutokana na matangamano yetu. So huwa
kunakosekana nini? Ifuatayo ni orodha ya mambo 5 makuu ambayo wanaume
wengi hukosea wakati wanapomtext mwanamke, na jinsi ya kutatua.
Zama nasi...
#1 kukata tamaa mapema kwa mwanamke
Kosa kuu ambalo wanaume wengi hufanya ni kukata tamaa mapema wakati
wanapomtext mwanamke. Watamtext mwanamke, na kama hatajibu jumbe zake
(ama kujibu kiuchache) watachukulia kuwa mwanamke huyu amepoteza
interest na wanakata tamaa. Hili ni kosa kuu sana.
Kama inavyojulikana kikawaida ni kuwa mwanamke anaweza kutojibu meseji
zako, na sababu hizo hazina uhusiano moja kwa moja na kutokuwa na
interest kwako. Kwa mfano, anawezakuwa labda yuko busy, katika mood
mbaya, ama labda hayuko sure ni kitu gani cha kukujibu kwa meseji.
Kiufupi ni kuwa haujui kile ambacho kinazunguka kwa akili ya mwanamke,
so haina haja ya kufikiria jambo baya.
So, iwapo kama mwanamke hakukujibu ama hayuko interested na wewe, lakini
bado unataka kuongea na yeye, hivi ndivyo unavyopaswa kufanya; Mpe muda
wa kutosha (siku chache ama hata wiki) halafu anza kumhusisha kwa
meseji. Kama vile texts zozote za kawaida, hapa utakuwa unataka
kuhakikisha kuwa unamvutia, unamfurahisha na unamchesha. Na zaidi ni
kuwa unapaswa kutafuta swali ambalo litamlazimu yeye kureply meseji
yako. Yote hayo, huu hapa ni mfano mzuri wa meseji ambayo itamhusisha
mwanamke yeyote:
Hello mrembo...hivi kweli uko hai? Nitume kikosi cha maninja kije kikunusuru ama?
Yaweke maneno yako kuwa ya ucheshi, yawe na kamchezo flani na bila shaka
utamfanya huyu mwanamke kutabasamu na kuwa katika hali ya kuchangamka.
Kama utaweza kumfanya atabasamu basi muda mchache tu atakujibu.
2. Kutext mara nyingi.
Hakuna kitu ambacho kinaweza kuua nafasi yako kwa mwanamke kama kumtumia
jumbe mara nyingi. Humfanya mwanaume aonekane mwenye tamaa hivyo
kumfukuza mwanamke.
Kwa kuepuka haya yote hizi hapa ni njia unazoweza kuzitumia ambazo zinaweza kukusaidia kumtext mwanamke wakati sawa.
♥Unapomtext mwanamke, hakikisha kuwa jumbe zinakuwa 1:1, Unahakikisha
kuwa kila meseji anayotuma unaijibu na moja (pia hakikisha urefu unakuwa
sambamba)
♥Acha kumtext na jumbe zisizo na mwelekeo. Usimjibu mwanamke jumbe
wakati ambapo haihitaji jibu. Kwa mfano, si lazima uijibu text ya
mwanamke ya 'usiku mwema' kama utamwambia 'nawe pia'. Ikifikia hatua hii
mazungumzo yenu yatakuwa yameisha. Inachotakiwa kutoka kwako ni
kuhakikisha kuwa jumbe ya mwisho inaisha kutoka kwake.
♥Weka fikra ya wengi. Wakati ambapo unamtext mwanamke mmoja, huwa
kawaida unakuwa na mtazamo finyu wa kumfiria sana mwanamke huyu ukiogopa
asikuache. Well, kutatua swala hili, lile unalotakiwa kufanya ni
kuhakikisha kuwa katika akili yako weka ya kuwa una wanawake kadhaa
ambao wanakufukuzia. Hii itakusaidia kuondoa uhitaji mwingi wowote.
3. Kuchukulia jumbe unazomtumia serious.
Kuna hali tofauti tofauti ya kuwa serious na mwanamke wakati wa
mazungumzo lakini kutumia jumbe si moja wapo. Kujifanya kuwa serious
wakati wa kumtext mwanamke kunachosha na hakuna mtu anapenda. Hivyo weka
seriousness zako mbali kabisa na ulete hali ya ''nataka-tujuane-nawe''.
Wakati unapomtext mwanamke, unapaswa kumakinika kuleta furaha.
Sasa, njia nzuri ya kuhakikisha kuwa unamfanya mwanamke anakuwa na
shangwe wakati wote ni kwa kutumia 'emoticons'. Wanaume wengi
wanajitenga kutumia emoticon wakidhania kuwa ni mambo ya wanawake,
ukweli ni kuwa ni mambo ya wanawake na wanawake wanapenda kutumia
emoticon. Pia zinasaidia kwa kuwa kile utakachokisema kwa kutumia
emoticon mwanamke hatakipuuza. Hatobahatisha hisia zako kamwe kwa kuwa
emoticon zinasaidia kupitisha ujumbe unaodhaminia. Na matokeo yake ni
kuwa unaepukana na drama zozote zitakazojitokeza.
4. Kutotext wanawake wengi.
Wakati mwanaume anatext mwanamke mmoja, ni rahisi kwake kumaliza
maongezi yake mapema kwa kuwa hana fikra pevu kama vile tulivyotangulia
kusema awali. Kama unataka kuwa na fikra pevu na uwezo rahisi wa
kutangamana na wanawake basi ni lazima uwe unatext wanawake wengi.
[Soma: Njia 5 rahisi za kumwomba mwanamke namba ya simu]
Kufanya mazungumzo mengi na wanawake wengi kunakupa ufahamu na mbinu
pana za kuweza kuzungumza na wanawake. Ustadi huu utakuja wenyewe iwapo
utajikita kuongea na wanawake wengi na tofauti tofauti katika meseji
zako. So kinachohitajika kwako ni kutafuta namba za wanawake tofauti
tofauti na uanze kuongea nao kupitia jumbe.
5. Tunasahau lengo kuu la kumtext mwanamke.
Wakati mwingine wanaume wanasahau kwa nini wanawatumia jumbe wanawake.
Wanakita kuongea mambo ya mbele, nyuma na ovyo bila msingi wowote ule.
Wanasahau ile taswira kuu ya kumtext mwanamke. Taswira kuu kama tujuavyo
ni kuhakikisha unatoka deti na mwanamke huyu. [Soma: Njia nzuri ya kumuomba mwanamke mtoke mkale bata]
Lakini usichukulie kuwa kuchat na mwanamke kupitia texts imepangwa, la.
Unapaswa kutumia mfumo ule wa kawaida wa kuleta ucheshi, mzaha nk, kama
tulivyoelezea awali. Hivyo basi, mbinu zako za kumtext mwanamke lazima
ziwe za kuvutia, za nakshi na ambazo zitaleta msisimko ndani yake. Kama
utamtext mwanamke bila mpangilia ama lengo flani, basi bila shaka
atapoteza hamu na kuenda zake. [Download: Kitabu chetu cha SMS tofauti tofauti umtumie mwanamke]
Saturday, October 6, 2018
Masharti Ya Kumtext Mwanamke - Makosa 5 Unayoyafanya
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment