Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Saturday, October 27, 2018

Nimefinywa Vibaya, Siijui Kesho Yangu- Wema Sepetu



Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amefunguka kuwa hayuko tayari kuendelea kufanya vitu ambavyo vitamdhalilisha yeye pamoja na familia yake na kudai kuwa matukio yaliyotokea yamemuumiza japokuwa haifahamu kesho yake.

Wema ametoa kauli hiyo leo Oktoba 25 katika mkutano na wanahabari wakati akiomba radhi watanzania na mamlaka husika kufuatia kusambaa kwa video pamoja na picha zake mtandaoni zikionesha akiwa faragha na mchumba wake mpya.

"Watu wanaweza wasiamini kuwa nimebadilika kutokana na historia yangu, lakini kitendo hiki kimeniumiza na nimejifunza na sitaki kuona vitendo kama hivi vikitokea tena katika maisha yangu, japo siijui kesho yangu", amesema Wema Sepetu.

Wema amesisitiza kuwa, "Nakiri nimefinywa vibaya, nitakuwa binadamu wa ajabu sana kama nikisema sijaumizwa, naomba radhi kwa hili lililotokea, namuomba Mungu aniongoze katika maisha yangu mapya kwa kuwa ndiye muweza wa yote".

Oktoba 17, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram Wema alichapisha picha inayomuonesha akiwa na mpenzi wake mpya kitandani huku akikataa kupokea maoni yoyote kutoka kwa mashabiki wake baada ya kufunga sehemu ya 'Comment', ambapo katika picha hiyo wema aliandika,'My future husband', akimaanisha kuwa huyo ndiye mumewe mtarajiwa.

No comments:

Post a Comment