
Nilikuwa
natoka kazini saa kumi jioni, lakini cha ajabu nilikuwa nikitafuta
sehemu ya kupoteza muda ili mradi nirudi nyumbani usiku. Nikiamini mke
wangu atakuwa amelala. Siku zote nilitumia njia hiyo, hata kunywa pombe
nikajifunza ilimradi nikwepe kugungulika udhaifu wangu.Si mitishamba
wala hospitali za kawaida kote nilienda bado ikawa si kitu.
Siku moja mke wangu aliamua kuelekea kazini kuuliza kuhusu ratiba ya kazi zangu. Alimkuta Mzee Jophu mwenyewe.
“Shikamoo baba” Mke wangu akamsalimu pale alipofungua mlango wa Mzee Jophu.
“Marahabaa mchumba mzuri”Mzee Jophu akaitikia salamu kamavile anamuona mke wangu mtoto mdogo.
Hata hivo Getruda ,mke wangu hakujali aliona ni utani tu kwani anajua dhahiri ni shemeji yake.
“Shemeji
nimekuja ninashida”Getruda akasema na kusubiri kitu ambacho angeelezwa.
Mzee Jophu alionekana kutingwa na shughuli nyingi pale ofisini.
Aliinua kichwa chake na kumtizama Getruda kwa macho ya huba.
“Shida gani shemeji?”
“Wala usishituke ni shida ndogo tu”Getruda akasema akiweka pete yake ya ndoa vema.
“Shemu sema kama ni pesa. Nikupatia au nimambo ya familia unataka kunieleza?”
“Ndio, ulijua je?”
“Najua maana nyie wanawake mmeumbwa na aibu sana. Jambo dogo unaweza ukaogopa kumueleza mwanaume”
“Nijambo dogo kwa kulitizama lakini kwa undani nijambo kubwa”
“Sawa ulitaka tukalizungumzie faragha kidogo?”
“Hapana shem. Naomba nikueleze hapa hapa”
“Sawa
nimekuruhusu. Lakini nilipendelea tutoke tukazungumze nje ya ofisi
kwani mambo ambayo haya husiani na ofisi tunayazungumzia nje ya ofisi”
“Naomba nizungumzie hapa , ni kwamba sitatumia hata dakika tatu”
“Ok, sema”
“Naomba unieleze, mume wangu anatoka kazini saa ngapi?”
“Wewe
kwani kakuambia anatoka saa ngapi?”Mzee Jophu hakujibu swali kama
alivyoulizwa bali nae aliligeuza swali upande wa Mke wangu.
“Anasema saa tano usiku”
“Basi inawezekana, kwani mama unaweza kuniambia, maana ya kazi?”
Mzee Jophu alimuuliza swali kwa mtego wa kasa
“Kazi kama ninavyoifahamu ni kitu au ni shuhuli inayoniletea kipato,”
“Ahaa kumbe unajua, mama nenda nitakuambia, maana yake siku nyingine ukiwa na muda.”
“Lakini bado hujanijibu mume wangu hutoka saa ngapi kazi kwako?”
“Saa kumi jioni?”
“Kaaa!. Saa kumi jioni halafu hufika nyumbani saa sita usiku?”
“Inamaana
Sweedy hurudi nyumbani usiku?”Mzee Jophu alimtolea Getruda macho ya
mshangao, huku akishika kiuno kana kwamba haamini maneno ya Getruda.
“Ndio shemeji”
“Siamini
kabisa. Siku zingine huwa na mruhusu saa tisa na siku za jumamosi
anatoka saa sita mchana”Mzee Jophu alizidi kuongezea chumvi.Nia yake ni
kuvunja ndoa yangu ili afaidi yeye.Alipania kuvuruga ndoa yangu.Siku jua
hata nguvu zangu ya kiume zilipoisha ni kwasababu yake.Yeye ndiye
alituma watu ambao walivaa kama Daktari kuja kunipiga sindano ya kuua
nguvu ya kiume.
“Shemeji inamaana maneno yako niyakweli kabisa”
“Shem
nikudanganye iliiweje?.Sitaki kukuvunjia ndoa yako lakini ukweli mumeo
hakupendi. Anasema sana kila siku hapa kazini kwamba mpaka sasa hajawahi
kufanya tendo la ndoa na wewe.Eti mke gani wa kutafutiwa na
wazazi.Anampango wa kukufanya kijakazi pale nyumbani kwake….”
“Eti
nini?.Shemeji naweza kuyaamini maneno yako kwani ni miezi miwili sasa
hajanigusa kabisa. Kila siku anasingizia kuchoka na kuumwa.Raha ya ndoa
iko wapi shem?.Naomba unipe ushauri nimechoka kuvumilia na mateso haya”
“Usichoke
shemeji vumilia tabia itabadilika. Yule bwana anapenda watoto wa shule
sana na mshahara wake mwingi huishia huko.Juzi tu kashikwa ugoni na
mtoto wa shulwe ambapo alitolea faini laki saba, huwezi kuamini lakini
ndivyo ilivyotokea. Mumeo ni mkware kweli…Naomab ausije ukamueleza
maneno haya naomba ufanye siri, nitakueleza mengi siwezi kuvumilia
ukateseka bure binti wa watu”
“Ahsante sana. Leo atanikoma nyumbani”Getruda
aliondoka akiwa na mawazo chungu zima.Machozi yalimlenga lenga
machoni.Moyo uliuuma sana. Waliagana na Getruda, lakini moyoni Mzee
Jophu alibaki na sononeko la upendo kwa mke wangu, Na aliamini kumpata,
kwa jinsi alivyo nitumia Daktari wanipige sindano ya kuuwa nguvu za
kiume, aliamini njia hiyo aliyotumia ya kuuwa nguvu za uume,wangu
ungeshindika kumpata Mke wangu basi angeniuwa kabisa
“Yaani
Sweedy ndivyo alivyo?.Nimemtunzia boma langu iliawe wa kwanza kulibomoa
lakini hataki, anapambana na watoto wa shule?.Haipiti hata siku moja
haachi kusema naumwa sijui kichomi mara nimechoka kumbe anachoshwa na
hao makahaba wa shule?”Getruda alizidi kuwaza njia nzima .Hakuwa
anaelewa sehemu alipokuwa alisha pita nyumba yetu.
Ilikuwa
siku ya juma mosi siku hii aliyotokea kazini,hakuweza kuzungumza
chochote na mimi.Alionekana mwenye ghadhabu kali . Hakutaka hata
kunikaribia, alikwenda kujipumzisha kitandani.Macho yake fika
yalinijulisha kwamba alikasirika sana. Nami niliogopa kumuuliza kwani
nilijua lazima alichukia kutokana na matatizo yangu.Sikuwa nalingine
kichwani.Wakati wa kulala ulipofika ,nilitoka sebleni ambako nilikuwa
nikitizama mkanda wa dini, na kuelekea chumbani.Nilijawa na wasiwasi
kwamba usiku huo kungekuwa na kitimtim kikali, dalili niliiona toka
mapema kabisa.Sikuwa na amani na maisha yangu, hofu kubwa ilikuwa kwa
mke wangu ambaye hakuwa na raha kila aliponiona.Sasa hasira yake ikawa
kubwa pale alipopewa maneno ya uchochezi na tajiri yangu.Nilitembea kwa
kunyata ilitu asisikie kwamba naelekea kitandani.Kwa sasa nikajongea na
kukifikia kitanda.Nilipandisha mguu wa kushoto kwa hadhari sana
asishituke. Pia nilihakikisha kitanda hakichezi, jambo hilo nililifanya
kwa makini zaidi.Wakati huu napandisha mguu macho yangu yalitizama usoni
kwamba mke wangu angeshituka ama vipi. Nilifanikiwa kupandisha mguu wa
kwanza, sasa nikajaribu wa pili kuupandisha kitandani. Laiti ningekuwa
na uwezo ningejitafutia kitanda changu.Ukweli ndoa yangu niliiona chungu
na iliyojaa mateso makubwa sana. Nilikuwa mtu wa wasiwasi tupu.Kitu
kingine, nilijiona nisiye na dhamani duniani, nilitamani nife kuliko
kuishi kwa shida lakini wasiwasi wangu ukawa huko ahera nikukimbiliako
je? Ni kwema aba ndio nitakimbilia mateso mengine?.Nilizidi kuzama
kwenye dimbi la mawazo.
Nikafanikiwa
kupanda kitandani bila mkewangu kushituka,nilihisi angeshituka angetaka
tendo la ndoa wakati huo huo.Sikutaka kulala zaidi ya kulala macho
wazi, nilijua nikishikwa na usingizi ningeweza kukoroma ambapo mke wangu
angeamka, kwani nilijijua toka niliwa shuleni kwamba nimkoromaji mkubwa
hata mtu nyumba ya jirani angesikia.
Sikulala
kabisa, nilihakikisha simgusi hata kwa shuka ambapo angeamka na
kunisumbua.Saa kumi na robo nilisikia jooo za jirani zikiwika nikajua
kwamba kunakaribia kupambazuka. Nikiwa kitandani nilishuhudia miale ya
mwanga ikiingia kupitia dirishani.Nikajua tayari palisha kucha.Mpaka
wakati huo mke wangu hajazugumza kitu chochote na mimi.
Ilikuwa
siku ya Jumapili,siku ya mapumziko,nilikuwa nyumbani na Mke wangu
lakini maongezi yetu yalikuwa juu ya unyumba wetu,si kuhusu maendeleo.
“Hivi
mume wangu umenioa ili niwe pambo lako au kama TV unitizame tu au
laa!.Naomba unieleze nimevumilia vya kutosha”Getruda alisema kwa hasira
baada ya kunitengea chai mezani.
Nilishindwa
hata kuokota kikombe nikabaki nimeduwaa. Nikanyamaza kimya, nilishindwa
niongee uwongo gani,kwani kila siku nilikuwa muongo wa kupindukia,mara
naumwa, mara nimechoka kazini, mara sijisikii,zote hizo zilikuwa njia za
kukwepa aibu.
“Sema”Mke wangu alifoka kwa kunihimiza.
“Kwani baada ya ndoa ni haki kunitendea hivi?Kila siku hupandi kitandani mpaka mimi nishikwe na usingizi………”
Nilinyamaza
kwa muda dakika tatu, kichwa nikiwa nimekiinamisha kama kondoo, kisha
nikameza mate na kulamba mdomo, kila nilipotaka kuongea nilijikuta
machozi yakitiririka kwa kasi,nilihisi labda nililogwa na
walimwengu,kweli imani ya kishirikina ilitawala ndani ya ubongo.Niliamua
kujikaza na kuanza kuongoa uwongo.
“Mke wangu shughuli zangu nzito sana, halafu ni za usiku mno!huwa nachoka nashindwa kufanya tendo la ndoa na wewe”.
“Eti
nini? kwa hiyo kuna wengine unaofanya nao?. Si ndio, hao machangu wa
shule ndio wanakusababishia unione kama mboga zilizochacha eee!.Eti
nashindwa kufanya tendo la ndoa na wewe”.Mke wangu aliongea kwa kufoka
huku akibana sauti na pua akiniigiza nilivyo sema.
“Hapana
mke wangu” nilimjibu kwa sauti ya kidhaifu iliojaa uwoga na simanzi.
Nilikuwa niiingia baa na kunywa, niliporejea nyumbani uliku usiku wa
manane nikiwa chakari. Mke wangu hakuweza kugundua mapema, hata mimi
mwenyewe sikujua ugonjwa huu niliupata wapi.
“Mume wangu”
“Naam mke wangu”Nilimwitikia nikiwa nimeangalia chini,kwa mbali mapigo ya moyo yalinidunda.
“Eti unasubutu kuniitikia.Wewe mwanaume kweli?”
Sikutegemea maneno hayo.Nikahisi mwili kufa ganzi.Nilijiona ninaye dhalilisha hapa ulimwenguni.
“Unafurahia nikuite mume wangu,sivyo?”
“Ndio”Nikaitikia kwa sauti ambayo hata mimi mwenyewe sikuisikia vizuri.
Nikanyamaza,nilijikuta machozi yakinitoka.Kwa kweli moyo uliniuma lakini sikuwa na lakufanya.
“Sasa unataka nikuite mume wangu wakati huwezi?”
“Getruda siwezi nini?”
“Kwani umenioa ilinikupikie tu?”
“Hapana”Nilijibu kwa hofu.
“Sasa unategemea mimi nitaishi vipi?”Safari hii Getruda alishika kiuno.
“Mke wangu vuta subira,nitapona”
“Kwani unaumwa?”
“Ndio, sin’shakuambia naumwa?”Nilikuwa na kila sababu ya kumnyenyekea.
“Hivi
Sweedy unataka kunifanya mtoto.Kwa taarifa yako nimeshajua siri
zako.Juzi umeshikwa ugoni na mwanafunzi ukatozwa laki saba.Na nimepata
tetesi kwamba unapenda hawa wa kusoma”Getruda alinishikia kibwebwe.
“Huu ni uzushi wa watu wasipenda niwe nawe.Naomba usisikilize maneno ya wafitini”
“Sio wafitini.Niwatu wanaokujua kwa ukaribu tabia yako”
Zogo lilikuwa kubwa ambalo lilichukua masaa sita.Baada ya hapo mke wangu akaondoka kwenda mjini.
Hakuwa
na safari bali aliamua kwenda mjini kununua gazeti la Mwanasport,
lililoandikwa mwongozo wa kumridhisha mwenzi kiunyumba, na kuliweka
kwenye meza makusudi ilinilione.
“Haya nakuuliza umesoma gazeti nililokuwekea kwenye meza?”
“Gazeti lipi mke wangu?” nilimuuliza kwa sauti ya chini.
“Hili hapa” mke wangu alinionyesha huku akinipatia nisome.
“Mwongozo wa njia za kumridhisha mwenzi kiunyumba”
“Aaaaa! Gazeti hili, kipengele hiki nisha soma….” Nilijaribu kuchangamka kijanja, lakini huzuni ilibaki pale pale.
“Uongo” Getruda alinishupalia
“Haki
ya Mungu, nimesoma kipengele hicho tena kinasisitiza swala la unyumba,
mume amtendee haki mkewe na mkewe amtendee mume haki yake, tena hii
hapa….” Nilijaribu kujitetea kwa unafiki.
Nilichukuwa
gazeti lile na kupitisha macho juu juu kwa haraka na kumwambia nimesoma
ndani vizuri. Nilifahamu sana nia yake haswa ilikuwa ni nini?
Nilimtizama mke wangu kwa masikitiko na kumuonea huruma, lakini
ningefanya nini ili kumridhisha, nae aridhike japo mara moja.
“Samahani mke wangu siku hizi na choka kwa shughuli nzito si mchana wala usiku, hata nimesahau kufanya mapenzi nawe”
“Hivi wewe unavyosema siku hivi, ina maana toka tufunge ndoa, tumeshafanya chochote na sasa karibu miezi miwili na nusu?”
“Basi ni samehe mke wangu”
“Nikusamehe kwa lipi?. Usinipotezee muda ninachoomba ni haki yangu bwana”
“Naomba unipe muda wa wiki nzima”
“Sitaki,
ninacholilia ni haki yangu.Kwani kanisani uliapa kwamba utanitendea
hivi. Ulinioa wanini kama hukunipenda, naomba talaka yangu haraka…”
“Umeenda mbali sana mke wangu…”
“Mimi
sio mkeo kuanzia sasa. Naomba uelewe. We mwanaume gani?”Getruda
alionekana mwenye hasira ,nikaamua kutulia kama niliyenyeshewa na mvua.
Akrabu
za saa zilionyesha saa tisa na robo usiku, mke wangu alijawa na
fukutiko la moyo lililokuwa zito, japo alikuwa na hasira lakini
alijitahidi kuiondoa ili kunitamanisha. Muda mfupi aliingia chumbani na
kufuata kabati lake lenye makorokoro yote ambayo yanampendezesha
mwanamke kuwa kivutio mumewe au mchumba au mwanaume rijali. Alichukua
muda kidogo akijipodoa na kujipara, mafuta sijui lotion, cream,
manukato, wanjaa lipshine nk. Hakuishia hapo alivaa sketi fupo, ambayo
wanaita kimini kilichoonyesha mapaja yaliyonona, na kibilauzi kifupi,
wengi huita “kitopu” chenye kuonyesha kitovu kilichoumbika sawia, usoni
alipaka poda kwa mbali na kujipulizia manukato yenye harufu ya mahaba.
Mke mwenye sura mufti, nyororo kwa macho ya kuita japo mke wangu
alijitahidi kwa vitu vyote hivyo lakini ilikuwa sawa na kupiga kinyago
ukwenzi, nilibaki kama zoba na mbege.
Juhudi
zote za kujipara manukato, tabasamum nono! Nilibaki kuwa sikuuwona
uzuri ule, kumbe ni kwasababu nilikuwa siyawezi. Uzalendo nae
ulimshinda, ndipo alipaanza kuuliza.
“Mume wangu urembo wote nilonao bado hunitamani? niambie unanipenda au hunipendi” “Nakupenda”
“Sasa kama unanipenda mbona hunifa…” alizidi kulalama kila siku, kila dakika, kila sekunde.
“Nisamehe
mke wangu ongea taratibu jirani watasikia”. Niliongea kwa sauti ya
chini nikiwa nimempigia magoti mke wangu, sikupenda jirani watambue
udhaifu nilionao.
“Nirahisi
kupata msamaha wangu, lakini nataka ufanye ninachokuambia, umenielewa
mume wangu” mke wangu alipunguza ukali kidogo na kuanza kupitisha mkono
wake wa kushoto akipapasa kifuani mwangu.
“Haya
twende tukatizame mkanda wa X kwenye video ya chumbani” mke wangu
aliongea kwa kunibembeleza, aliamini yeye kama mwanamke lazima
ambembeleze mumewe,amfanyie vile vitu anavyopenda ili penzi likomaa na
kufika kileleni.
Tulifika
chumbani nilijitupa kitandani kigoigoi, roho ikiniuma “Ugonjwa huo wa
kuuwa nguvu za kiume niliupata wapi? Au huyu mke ni jini nini? Mbona
nimemuoa na uume wangu kukosa nguvu, kwanini? Mbona jenifer
nilimridhisha vya kutosha. Mama mkwe kaniloga nini?. Hataki niwe na
mwanae” Alitoa mkanda kwenye droo za kanda kisha akasema “Mkanda huu
nimeaununua kwa ajili yako. Najitahidi kila namana kukuvuta jirani nami
mpenzi” Getruda aliongea huku akitoa tabasamu nono.
“Halafu baada ya kuangalia nini kiendeleee?” niliongea kwa wasi wasi mkubwa tena kwa kuropoka, nilihisi kuchanganyikiwa.
“Kwani wewe umenioa niwe nani kwako, au nifanye nini. Niambie sio kuropoka maneno yasiona maana” Getruda alizidi kufoka.
“Vitu vingine vinaleta kero, sijui huyu ni mzigo, au nini?” Getruda alijisemea kimoyo moyo.
“Basi yaishe mpenzi, punguza hasira”
“Ooo! Kumbe ulikuwa unataka tujifunze kitu”
“Ndio, ili tujifunze wazungu wanavyoridhishana”. Getruda alipunguza hasira kidogo yote hayo ni kunifanya nisisimke.
“Kaaa!
Pamoja nami?” Kwa kweli nilichanganyikiwa kabisa, nilikkuwa nikiropoka
maneno yasiona msingi, hata nilivyomjibu aliniona limbukeni.
“Kwani
ajabu, ndio nikae nawe!” Getruda alizidi kushikwa na hasira usiku mzima
hatuku lala ni kukoromeana, maneno ya lawama na mengine ya kuomba
msamaha.
“Nikae
na wewe tu?” nilizidi kumyumbisha kwa maneno ya ajabu ilimradi
papambazuke niondoke mikononi mwake. Nilitamani pakuche niondoke niende
kazini.
“Hukubali eee!, niambie hutaki?”
“Aaaaa! Na kubali kabisa bila hofu” jibu hilo lilimfurahisha Getruda mke wangu aliamini ningefanya mapenzi muda mfupi.
“Basi
vizuri, nitashukuru mume wangu, na nitakupa unachotaka, japo sijawahi
kufanya ngono lakini nitakuachia ufanye utakavyo taka.” Mara moja
alianza kuimba
“Basi mume wangu Sweedy, wewe ni wewe
sina mwingine, kama ni kundi la ndege msituni basi wewe ndio chaguo
langu, wengine sioni, nakupenda peke yako naomba uangaze pendo letu
ling’are giza,…” Alitunga wimbo wa muda mfupi.
Getruda,
mke wangu alinifuata kitandani baada ya kuweka mkanda wa mapenzi,
alinikumbatiam tukaanza kuviringishana huku na kule. Lakini wasi wasi
ulinijaa pale nilipo kumbuka mapenzi na mke wangu, niliamini hakuna
chochote kingeendelea zaidi ya kumtesa Getruda. Wala sikuwa tayari ajue
udhaifu wangu, nilihofu pindi angejua basi angeomba talaka, hata hivyo
siri ingekuwa hadharani, kila kona ya dunia.
Baada ya kuchoka mabusu, alilala kwa chali akiwa ananitizama, kwa hofu nilitizama pembeni, sikuweza kumuangalia usoni.
“Niangalie
basi nijue unanipenda” nilipomtizama kwa kujikaza, nilisikia akisema
(Ooooohhh! Honey you look at me, without uttering any word”) “Ooooohhh!
Mpenzi unanitizama bila kunena neno!” Nilituliza macho uso mwa Getruda,
uso ulijaa ubembe. Ingawa nilifahamu shauku ya
mke wangu lakini nilishindwa nimfanyie nini ili nionekane kidume na mume
hodari, sio sifa ya kuoa tu ndoa Kanisani. Lakini lazima nimburudishe
mke wangu hata kwa kumshika shika maungo yake, ili kumtuliza asionekane
mwenye sikitiko moyoni.
Hata
hivyo mke wangu hakuchoka na vitimbi vyangu, aliendelea kunishika
shika, ili kuniondoa uchovu. Aliona muhimu na dawa ni kwenda na mimi
bafuni kuoga, tulienda bafuni na kuanza kuoga pamoja, lakini hakuona
uume wangu ukisisimka hata kidogo. Hofu ilianza kumuingia hakuamini
alivyonihisi aliona ni uchovu tu wa kawaida. Hakuwa na roho ya kukata
tamaa, kule bafuni alijitahidi kuushika na kupapasa maungo yangu,
sikuonyesha dalili yeyote ile.
Getruda akaniogesha nami nikamuogesha.Tulipomaliza akachukua sabuni na bush la kuogea tukaelekea chumbani tukiwa tumefunga taulo. Getruda alionekana kuwa na hasira kali moyoni.
“Mume
wangu naona hunipendi kutoka rohoni, Bali ulilazimishwa na wazazi wako
sio hivi hivi ni miezi miwili sasa inatimia toka unioe hutaki kufanya
tendo la ndoa. Heshima ya ndoa iko wapi? Naomba unieleze kama hinitaki
niondoke au nini kimekusibu?”
Wakati
ananielezea machozi yalikuwa yanambubujika, aliamini kulia sio
suluhisho, taratibu alifuta machozi kwa lesso, alinisogelea karibu na
kunizungushia mikono kiunoni, huku akininong’oneza “Sweedy kuna kitu
chochote nisichokuridhisha mume wangu. Naomba unieleze niweze
kujirekebisha. “Tafadhali niambie sasa hivi. Nahitaji kujua, nitaishi
vipi bila mapenzi yako?”
“Kila
kitu unaniridhisha ila ni…ni…nina…ni….” nilikokoteza maneno
yaliyochanganyikanana kigugumizi, nilishindwa kutamka vizuri nilihisi
homa kali, nilijua ndoa ingeingia dosari.
“Ila una nini?. Sema mbona humaliziii?” alinikaripia kwa sauti.
“Unaumwa?” aliniuliza.
“Aaaa!, hata kidogo,” nilimjibu kwa sauti ya chini,
“Au…..penginenimekuudhi
bila mimi kufahamu…., maana mama husema mimi ni mkaidi na sijui namna
ya kumtunza mtu, ni kweli?” Getruda alizidi kunidadisi.
“Hapana” niliitikia kwa sauti ya majonzi.
“Oke, hivi ni kusema kwa sababu ya kazi ndio umenisogeza pembeni?”
“Hivyo ni vibaya mke wangu, nakuahidi nitajitahidi kukupa penzi nono!, ambalo litafuta kumbukumbu zote nilizo kukera”
“Kama sivyo, basi naomba unibusu, nijisikie furaha moyoni” mke wangu aliongea huku akinisogelea karibu zaidi.
Nilisita
kidogo kisha nikainamisha kichwa na uso kutokeza upande wa midomo yake
na kumbus kwa uvivu uvivu (Kigoigoi). Nilipomgusa tu midomo yake, mara
alinikumbatia vilivyo, kwa mikono yake na kuning’ang’ania na mabusu ya
mfululizo na muda mrefu na hata aliponiachia hilihisi joto lenye
uvuguvugu nikilikosa. Mwanzoni nilimbusu kwa wasi wasi na shingo upande,
lakini baadae nikaadhiriwa na mabusu motomoto ya Getruda nikajikuta
ashiki zikiwa zimesisimua mwili mzima, nilijibu mashambulizi kwa mabusu
ya nguvu huku nikihema roho juu juu.
Baada
ya mabusu yaliotuweka hali ya mapenzi, kwani ashiki zilimpanda na
kutaka penzi wakati huo huo bila kucheleweshwa. Akrabu ya saa ya ukutani
ilionyesha saa kumi na moja na nusu, karibu na kupambazuka. Majogoo
yalikuwa yakiwika kila kona ya wafugaji wa kuku.
“Mume wangu sikiliza” Getruda aliniambia, usoni macho yalikuwa yamelegea na kurembua rembua.
“Eee! Sema mama watoto” nilikohoa kinafiki na kusema.
“Karibu
kunapambazuka. Nataka uondoe mawazo ya biashara, madeni, sijue kazi
mawazo yako yote weka kuhusu penzi langu na wewe, naomba uniridhishe kwa
penzi motomoto.Kwani siku sitini sasa toka unioe
hujafanya tendo la ndoa na mimi. Hivyo leo ni mwisho, usipofanya tendo
la ndoa, talaka yangu naomba, siwezi kukaa kama pambo, katuni ndani ya
nyumba yako. Sijaja kukupikia hapa tumbo liende mbele, mimi sio kijakazi
wako, uelewe leo, mimi ni mkeo tena wa ndoa” Getruda alibadilika ghafla
na hakutaka kucheka na mimi, alikua anahitaji haki yake.
“Hayo
yote uliyosema nimeyatia akilini ila naomba unipe mu….” Kabla
sijamalizia maneno, nilikatishwana sauti ya ukali ya Getruda.
“Nikupe nini?, mbona sikuelewi?”
“Fahamu
kwamba ninahitaji kuwa na mtoto . Nataka nami niitwe mama Fulani, si
jina langu Getruda” Getruda alizidi kunifokea, nilishindwa kuelewa
ninani aliyekuwa ananitesa kiasi hicho.Niliwafikiria wabaya wangu wote
akilini sikupata aliyenitendea ushenzi huo.
“Ndio…”
niliitikia kwa sauti ndogo na ya huruma hata mimi mwenyewe sikuamini
ilitoka kwenye kinywa changu, wasi wasi ulinijaa moyoni, nilihisi
kuumbuka niliwalaumu wazazi walionitafutia mke. Laiti ningelijua kuwa
nina matatizo hayo nisinge Kubali kuoa.
“Haya
nenda ukazime taa basi basi mpenzi” Getruda alizidi kunifanya miguu
ilegee na kukosa nguvu ya kutembea, nafsi ilinyauka kama jani la tumbaku
lililosubiri kusagwa, jasho la woga lilinichuruzika. Sehemu ya kuzima
taa ilikuwa karibu kama hatua tatu lakini niliona umbali wa kilometer
ishirini.
Nilijikamua kikakamavu na kuinuka kwenye kitanda, kwa uvivu nikajongea kwenye
swichi ya taa. Kilikuwa kitendo cha sekunde tano lakini nilifanya
dakika saba.nilipofika kwenye swichi nilizima taa, mwili ulikuwa
ukitetemeka sio kwa baridi bali ni hofu juu ya kufanya tendo la mapenzi
na Mke wangu.
Nilitamani
kumfukuza mke wangu kwa kero nilizopata si usiku wala mchana, lakini
nilishindwa nianzie wapi na niishie wapi?. Licha ya kushindwa
kumfukuza,niliogopa siri ingefichuka na kila mwanadamu angenitupia jicho la lawama.
Nilibuni
haraka haraka mbinu za kuinusuru ndoa yangu,ili Mke wangu asigundue
matatizo niliyo nayo,nilirudi kitandani na kijisogeza ukutani mwa
kitanda,taratibu niliingiza vidole vya mkono wa kulia kwenye mkono
wangu,mwisho wa kinywa karibu na koromeo,na hazikupita sekunde
nane,nilitapika mfululizo. Sehemu ile ya ubavu wangu kwenye
kitanda.Niliamini kwa kufanya hivyo mke wangu angeanini kuwa mimi ni
mgonjwa. Lakini cha ajabu alianza kunivua nguo zangu badala ya kufikiri
njia ya kuondoa matapishi kitandani, alianza kunivua suruali. Alichoka
na maneno yangu ya kila siku nikilalamika, kuumwa,mara tumbo, kichomi,
kutapika, kichwa nk.
Baada
ya kunivua nguo, alivua na za kwake pia. “Maji ukiyavulia nguo huna
budi kuyaoga”alisema kwa sauti iliojaa hasira na mahaba. Mapigo ya moyo
wa Getruda yalianza kwenda kasi na mwili mzima ulisisimka baada ya
kunivua nguo zote.
Good
ReplyDelete