“Leo
lazima, sijali kuumwa kwako au laa!,Kila siku unalalamika, tumbo,
kichomi, kutapika, mara uchovu, leo ni leo”. Taratibu alianza kunitomasa
wakati huo nilikuwa nimetulia kama yule mdudu kifaulongo na minong’ono
ya kuweweseka kama mgojwa niliendelea kuitoa.
“Mume wangu amka basi tufanye.” Getruda alinihimiza huku akiwa amenishika mkono wangu kidogo akininyanyua .
“Subiri kidogo naumwa na homa”
“Imekuwa homa leo” kwa kweli mke wangu alichoka na idadi ya magonjwa niliokuwa nikimtajia kila leo.
“Eti
homa, utashaa leo, sikusikilizi ninachotaka ni penzi tu, usiniletee
hadithi za riwaya, zile hadithi ndefu za kubuni, sizihitaji kabisa!,
wewe mwanaume gani? Hivyooo!” Getruda mke wangu alianza kunidharau baada
ya kuona sina lolote. Nilianza kulia nikilaumu ugonjwa ulioniingia
nikiwa na ndoa yangu, niliulaani ugonjwa huo nilitamani nikatwe vidole
kuliko kuwa na udhaifu wa nguvu za kiume. Kilio changu kilikuwa chungu
mwenye na roho yangu. Pamoja na kunywa dawa za mitishamba kutoka kwa wamasai aina ya mchuma mbele bado nizidi kupata mateso ya unyumba.
“Mke
wangu unadiriki kunikashifu. Kunitukana mtusi ya nguoni!, kweli
umenichoka” nilijaribu kumlaumu mke wangu, lakini haikusaidia kitu.
“Ndio,
nimekuchoka, naomba talaka yangu asubuhi hii hii, longolongo sitaki”
mke wangu alibadilika ghafla na kunitizama kwa hasira kali, kama
kungekuwa na uwezekano wa kuniadhibu basi angeniadhibu ipasavyo. Niliona
bila kuwa mpole ndoa ingekuwa ndoano, ingesambaratika na ningekuwa
mseja.
“Mke
wangu naomba upunguze jazba nikueleze…” niliongea kwa sauti ya unyonge
iliyona lengelenge la machozi kunitoka, nikiwa na wasiwasi mkubwa wa
kumkosa Getruda. Sikupenda niachane na Getruda mke niliyepewa na wazazi,
mke mwenye hali ya ubikira, ambaye hajawahi kuguswa.
“Nimeshachoka na mambo yako ya ajabu, unataka kunieleza nini?”
“Najua
utanichukia nikikueleza kilichonisibu pia hutaamini yaliyonikuta
mwenzio”. Niliongea machozi yakinilengalenga machoni, roho iliniuma na
kujiona nisiye na faida wala umuhimu kuishi duniani, nilitamani kufa
ilinisiendelee na mateso. Kilio changu kilikuwa cha huzuni mno!, moyo wa
huruma ukamuingia mke wangu, masikini akaniomba nimuelezee.
“Mume
wangu haya nielezee kilicho kusibu, usiogope kuwa wazi usinifiche
chochote kama kuna uwezekano nitakusaidia mpenzi” sauti ya mke wangu
niliisikia na kuifananisha na sauti ya malaika wa neema. Nikajikaza huku
nikiwa na churuzika machozi yaliyolowanisha kope machoni.
“Mke
wangu hujafa hujaumbika, nisikilize kama mtu asikilizavyo maneno ya
Mungu, nilikuwa kiwandani kwenye uchanganyaji wake Kemikali, bahati
mbaya kemikali yatindikali ilinidondokea kwenye ngozi karibu na uume
wangu na kunisababishia udhaifu mwilini, naomba usiniache mpenzi, naomba
unisamehe kama nimekukosea mpenzi, naamini nimekukosea. Sikuyataka bali
yametokea bahati mbaya” Niliongea uwongo uliofanana na ukweli, kadri
nilivyozungumza ndivyo nilivyozidi kulia, sikupenda kuongea uwongo bali
ilinibidi niongee uwongo mtupu ilikuinusuru ndoa na aibu yangu ,
sikumwangikiwa na tindikali, ni ugonjwa ulionitokea ambao sikujua
ulitokea wapi na nani aliyeniletea ugonjwa huo, je ni Jenipher au ni
nani?”
“Sasa
kama ulikuwa unajua unamatatizo kwanini ulinioa mpenzi?, unanitesa,
umepoteza muda wangu bure” Getruda alizidi kulalamika japo alinionea
huruma.
“Kumbe ndio maana kila siku ana lalamika na kunitajia magonjwa mengi yote hayo ni kukwepa…” Getruda aliwaza akilini.
“Mke
wangu matatizo yalitokea siku tatu kabla ya ndoa, wala sikujua
nimeadhirika na tindikali hiyo, ningejua ningehairisha kufunga ndoa ili
upate mume rijali” maneno yangu yalimuingia Getruda mke wangu na kuamini
kuwa ni kweli nilipata ajali ya kumwagikiwa na tindikali.
“Nitaishi
vipi bila kupata matunda ya ndoa, naomba uniambie nitaishi vipi?,
nitaishi hivi mpaka lini, sijawahi kukutana na mwanaume, nilitegemea
wewe ndiye ungevunja boma langu, sasa itakuwa vipi? Naomba mawazo yako”
macho ya huruma yalitua usoni mwangu, niliyekuwa nimetulia kama
mtuhumiwa aliyesubiri hukumu ya kunyongwa.
“Mke wangu hilo usitie shaka. Hakuna kinachoharibika nivumilie kidogo”
“Siwezi kukuvumilia tena mume wangu. Naomba talaka haraka”Nilitamani kuondoka , ikiwezekana kuihama nyumba yangu,nikifikiri jambo hilo lingenisaidia lakini nikajikuta nikikatisha mawazo na nafsi.Nilitulia kama sekunde kadhaa hivi nikijaribu kuganga maumivu.
“Uliapa
mbele ya mchungaji kwamba utaishi na mimi kwa uvumilivu…”Kabla
sijamalizia maneno yangu , nikakatishwa na sauti ya ukali .
“Ndio. Nimevumilia nimechoka, naomba uelewa kwamba namimi nina homoni”Getruda akasema akinitizama kama mtu alieniandalia tusi.
“Nataka niende nchi za nje kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi”
“Nchi gani?”
“Uingereza….” Nilipumua
kidogo kisha nikaendelea kumweleza, wakati huu nikimueleza, nilikuwa
siamini kwamba angeweza kulielewa lile nililotaka alifahamu na kulitii
“Getruda nakupenda na kiliwaahidi wazazi wangu nitaishi na wewe hadi
mungu atakapo chukua roho zetu”
“Sweedy unajua maana ya ndoa kweli?”Getruda akaniuliza akiwa amenitumbulia macho.
“Ndio”Nikajibu kwa sauti ndogo na ya upole kabisa,nikiwa nimeinamisha kicha kama kondoo.
“Kama
unajua maana yake.Mbona sioni nini maana ya ndoa kati yangu na
wewe?”Hapo nikavuta pumzi ndefu na kuziachia kwa nguvu,
“Ooooopphhhh”.Ikafikia wakati mwingine hata kujionea mwenyewe huruma.
“Si nishakuambia tatizo langu?”Nilizidi kutukutika moyoni.
“Basi kama unataka nisivunje ndoa yetu nitafutie ndugu yako aniridhishe kimapenzi mpaka utakapo pona”
“Sina ndugu yangu wakiume mke wangu.Kwa nini usiwe na subira?”Machozi sasa yakaanza kunidondoka kama maji ya dripu, nilihisi kudhulumiwa haki yangu , ingawa nilitaka njia ya amani kati yangu na mke wangu.
“Ngoja
ngoja yaumiza matumbo”nilimtizama Getruda, mke wangu nikagungua hakuwa
na nafasi tena ya kunisubiri. Macho yake tu, yalikuwa jawabu tosha
kwamba angeondoka kwenda kutafuta mume mwingine.
“Nasubiri
unijibu upesi, sitaki mzaha tena. Ushanipotezea muda mwingi sana
Sweedy”Sauti ya kupaza niliisikia ikigonga ngoma za masikio yangu,
nilijaribu kumtupia macho ya huruma,kuwa pengine angepunguza maneno.
Sikuweza kumjibu chochote,badala yake nikabaki kimya kama niliyeletewa
habari ya msiba wa ndugu yangu wa karibu.
“Dharau
yako itakuponza. Wala sitaki talaka yako.Naondoka, narudi kwetu mwili
wangu bado unaniruhusu kuolewa.Kama ni bikra bado ninayo kama ni kuzaa
ndio kabisaa.Kwanini nikose mume.Uzuri wangu tosha nishahidi kwamba
sitokaa kwetu mwezi bila kuolewa”Getruda aliongea na kunyanyuka kitini
ambako alielekea chumbani. Nilibaki nikimtizama bila kunena neno juu yetu.Sikutarajia kuona kile kilichopo mbele yangu wakati huo.Nilimuona Getruda akiwa kabeba begi kubwa languo akitoka nalo nje varandani.
“Mke
wangu tafadhali naomba uweke begi chini tuongee.Unapochukua uamuzi huo
si suluhisho. Ni busara kusuluhisha mgogoro ili kuhuisha uhusiano mwema
,tangu kuumbwa kwa familia hakuna hata moja isiyopata ubishi na mgogoro
ndani ya nyumba…..”nilivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu ,ni
dhahiri nilichoka kuitetea ndoa yangu isianguke.Wakati huo Getruda
alinitupia jicho, begi lake akiwa kalishikilia mkononi.Nikavuta hatua na
kumfikia karibu, nilimshika mkono nikijaribu kumbembeleza, “Tafadhali
usinishike.Muda wa kuishi nawewe umeisha.Mume gani usiye…”Nilimkatisha
maneno yake, “Ni samehe mke wangu,nitaendelea kukuita mke wangu kwa
sababu nakupenda, naomba uwe na subira. Unyumba nikuvumiliana, kuna leo
na kesho, kumbuka hujafa hujaumbika, jambo hili linaweza kukukuta hata
wewe,pengine ukapata ajali.Sikupenda kuwa hivi mpenzi…. hili ni jambo la
kawaida, muhimu ni jinsi ya kutatua mikwaruzo hii.Mfano ungekuwa wewe
mwenye matatizo haya ungelifanya nini?”
Niliongea taratibu na kwa busara nikijaribu kumshauri Getruda , mke wangu. Alivuta pumzi na kuzishusha.
“Naomba unipe uhuru.Utakubali niwe naingiza mume mwenzio ndani?”
“Hapana.
Utakuwa ni unyanyapaa wakijinsia.Getruda unataka kuniumiza moyo
wangu.Nakupenda na nimekuomba uwe na subira,pengine nimajaribu ya
mungu”Nilivumilia kulia ikashindikana,machozi yalinitoka bila
kutegemea.Nilitamani nibaki peke yangu ,ingawa sikuweza kuamini kama
kweli Getruda angenihifadhia siri yangu.Angeenda kuwaeleza nini wazazi
wake.Kuna mtu anaweza kuvunja ndoa bila kufarakana, migogoro ya
kiunyumba?.Mawazo hayo yalizidi kuniumiza na kunikera moyoni.
“Chagua
moja….”Alitulia , akalamba midomo yake kisha kunitizama kwa
dharau.Dharau hiyo niliigundua kwamba nikwa vile aliniona si lolote si
chochote kwake.
“Unasema unanipenda sana?”
“Kwani hujui hilo?”
“Sijui kwa sababu wewe mwenyewe hujanionyeshea upendo wako kwangu”
“Hivi umesema unanipenda vile?”
“Ndio…najua umekuwa wimbo”
“Naomba unichagulie maisha nitakayoishi kuanzia sasa”
“Basi nitakuacha uchague unachotaka mpenzi bora usinidhalilishe.”
“Sina chaguo lingine zaidi ya kunitafutia ndugu yako yeyote”Alisema tena akionekana siriasi.
No comments:
Post a Comment