Nilipofika kazini, nilikabidhi pesa kwa Tajiri yangu Mzee Jophu tukiwa katika maongezi ya mabadiliko ya kibiashara. Tulisikia mlango ukigongwa kwa nje, bila kujali wala kujua ni nani mtu huyo, Mzee Jophu aliamuru aingie, Aliingia na alikuwa sekretari wa Mzee Jophu.
“Boss, samahani kuna wageni wa Sweedy wanamuhitaji” sekretari aliongea akijikanyaga kanyaga na kuuma vidole.Alionekana kumuogopa sana bosi wake.
“Sawa waambie wasubiri kidogo” Mzee Jophu alijibu kwa kifupi na kuendelea na mazungumzo nami.
Tuliongea
na kumaliza, Mzee Jophu alikuwa wa kwanza kutoka kinyume na mashariti
yake, tuliongozana kujua nani alikuwa ananiita. Kwenye viti vya mapokezi
ya wageni, nilimuona baba na mama, mama mwingine wa makamo ambaye
simfahamu, pembeni ya yule mama nisiye mfahamu nilimuona binti mwingine
mrembo. Kwa haraka ubongo ulifanya kazi yake kwa bidii na kukumbuka kuwa
niliwapa kazi wazazi wangu kunitafutia mchumba baada ya kuzunguka kila
kona ya dunia bila mafanikio. Kumbukumbu hiyo iliutesa moyo wangu kwani
nilishapata mchumba mwingine, tena mzuri kuliko yule niliyeletewa na
wazazi, japo nae alikuwa mzuri lakini kamwe asingefurukuta kwa
Jennifer.Ndivyo nilivyo hisi moyoni na wasiwasi ukawa umejidhatiti
akilini.
“Baba
shikamoo, mama shikamoo!, Mama shikamoo!, Dada habari yako!
Niliwasalimia wote nikipita kwa mstari huku nikiwashika mikono. Pia mzee
Jophu naye alifanya hivyo hivyo nilivyofanya mimi. Lakini cha ajabu
aliposhikana mkono na binti yule akabaki amemshika muda
mrefu, macho ya upendo yakiwa yanatambaa usoni mwake. Nilishtuka pale
yule binti alipovuta kujinasua mikononi mwa Mzee Jophu.
Baba hakupenda kufanya mambo kwa siri, alizungumza yote mbele ya mzee Jophu mama na yule mama mwingine na binti yule.
“Mwanangu
unayemuona pembeni ya mama yako ni mama mkweo na msichana unae muona
hapo ni mkeo kazi uliyotutuma tumeikamilisha. Sidhani kuna la ziada zaidi ya kuhitimisha ndoa kanisani” Baba alizungumza na alitegemea kuona furaha, lakini furaha yangu ilifunikwa na uzuri wa Jennifer niliyeonja penzi lake Nchini Thailand.
“Mbona huongei wala huonyeshi furaha” Baba aliniuliza kwa mshangao.
“Baba
ningeomba tuzungumze faragha kidogo. Kuna mambo mengine hayafai
kuzungumza mbele ya mama na watu wengine, nilipoongea hivyo baba alikiri
na kujikuta akitikisa kichwa kuafiki yale niliyoyasema.
Tuliondoka eneo lile na kulizunguka nyuma ya jengo la kazini. “Baba nimekuita mazungumzo ya pembeni nina jipya lililojitokeza”
“Jipya lipi zaidi ya hili nililo kuletea? Baba alizidi kunikazia macho ya ukali.
“Ndio
hilo ni jipya ulilolileta wewe nashukuru. Lakini hata mimi nina jipya
nililopata nikiwa Nchini Thailand kikazi”Baba alionekana mwenye furaha
iliyotoka moyoni, alihisi pengine nimemletea zawadi, kumbe asijue ni
ujumbe wa kumkataa binti walionitafutia.
“Umeniletea suti nini mwanangu Sweedy?” Baba aliuliza huku akiwa ametoa tabasamu zito la kupokea zawadi.
“Hapana baba, ila ninaomba radhi kwa usumbufu.”
“Usumbufu gani?. Sema”
“Nimewasumbua
kunitafuti mchumba. Baba nikiwa Bangkok Nchini Thailand nimebahatika
kupata mchumba ninayetegemea kufunga naye ndoa.”
“Eti
nini”? usinichezee naona unataka radhi ya wazazi, hatuelewi kila kitu
tumemaliza. Mahari tumeshalipa tunachosubiri ni ndoa tu. Halina mjadala”
Baba aliongea kwa ukali, mishipa ya shingoni ilimtoka, ghafla macho
yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu.
“Naomba uniambie sasa hivi. Unamuoa yule binti au laa! Sitaki uniambie nikupe muda” Baba alizidi kufoka kwa sauti. Sauti yake
ilienda mpaka alipokuwa mama na mama wa yule binti na binti. “Baba
nisamehe sauti hiyo inasafiri naomba yaishe”Mara anakuja mama akikimbia
huku kanga zikimdondoka alikwapua kanga na kufika pale nilipokuwa na
baba.
“Baba Sweedy kuna nini? Mama aliuliza kwa kudadisi .
“Mwanao anataka kututia aibu.”Baba alisema akinikazia jicho la ghadhabu.
“Aibu gani tena?”Mama akauliza akiwa anamtumbulia macho Baba.
“Mwanao
hataki tena kuoa.Anasema binti tuliyemtafutia hajampenda.Na ameshapata
mchumba huko alikotoka” Baba aliongea kwa sauti ya taratibu iliyojaa
uchungu.
“Hakuna
pingamizi lazima aoe la sivyo atazunguka hii dunia wakumwoa hatamuona.
Hata huyo anayesema amempata pia atamkataa. Kama sisi sio…… nilimkatisha
mama aliyekuwa anaongea kama kuniachia radhi.
“Mama
sasa naona mnaniachia laana, basi nitamuoa binti huyo.” Muda mfupi
niliona maneno hayo yalirudisha furaha zao. Hawakupenda nichelewe kuoa,
mipango ya harusi ilifanyika na tarehe ya harusi ilipangwa.
Wiki
tatu kabla ya kusafiri kwenda nchini Thailand. Nilipokubali wazazi wote
walirudi kule tulipowaacha mama wa binti, binti mwenyewe ambaye ndiye
mke wangu mtarajiwa na mzee Jophu. Lakini tukiwa katika mazungumzo mimi
na wazazi wangu, huku nyuma Mzee Jophu alikuwa akiongea na mama wa binti
aliongea kuwa anamuhitaji yule binti amuoe yeye na sio mimi tena mambo
hayo yalifanyika haraka na kwa siri, si tu kwa maneno bali Mzee Jophu
alimpatia hela nyingi kuliko zile za wazazi wangu walizolipa.
“Mama
kamata laki tano hizi ni zako bado nitakuongeza” kwa shida ya mwanamama
yule alizipokea na kuziweka kibindoni kwa haraka huku akimuahidi
kuvunja ndoa isifungwe, aliniamini angetumia njia yoyote ya kukwamisha
ndoa. Ni mambo ya kusikitisha, mzee Jophu pamoja na kuwa baba wa familia
ya watoto watatu, bado alihitaji mke wa pembeni aliamini kwa pesa zake
nisingeweza kufurukuta “Pesa inazungumza. Pesa ni kila kitu.Haki pasipo
haki kwa tajiri ni haki” mzee Jophu alizidi kuzungumza.
Tuliporudi
pale nilishangaa kumuona Mzee Jophu akiwa na hasira alikunja ndita
aliponiona tofauti na mwanzoni. Nilijiuliza nina kosa gani, kama ni
mazungumzo yetu yalikuwa mazuri nimemfanya nini boss mbona ananitupia
jicho la ukali, nilishindwa kujua kilichoendelea kwa wakati huo.Mama
mkwe mtarajiwa nae alipindua midomo yake na kuibetua kama iliyoteguka
jicho la dharau lilinitizama kuanzia chini ya unyayo hadi juu ya nywele,
kisha kabla ya yote nilisikia akisema “Kijana wenu hana hadhi ya kumuoa
mwanangu. Kwa jinsi ninavyomuona” nilistaajabu kusikia sauti
iliyoambatana na kusonywa.
“Kwa nini mama Getu?. Amefanya nini mwanangu?” Mama alimuliza kwa sauti ya chini.
“Mwanao
hana nidhamu. Uso wake umetawaliwa na dharau. Hawezi kumuoa mwanngu”
aliongea kama kawaida alinitupia macho ya kunitazama kama mtu
aliyejinyea japo maneno yake niliona na niliyasikia yakinichoma moyoni
mwangu. Nilikabwa na fundo kali la ghadhabu nikaamua kumuheshimu tu,
kama si heshima basi ningeropoka neno lolote baya nae limkere moyoni.
Mzee Jophu alikuwa kimya pembeni , macho yakipepesa kwa kuibia na furaha iliyojificha ilionekana usoni mwake, lakini sikuweza kugundua kwanini mama yule alibadilika yeye na Mzee Jophu.
Mama
na baba walimuomba radhi awasamehe kuzaa mtoto asiye na nidhamu na
anisamehe, walijua pengine hasira ile ni kile kitendo cha mimi kumuambia
baba siko tayari kumuoa mwanae kwani nilipata mchumba Thailand. Lakini
mama mkwe mtarajiwa msimamo wake ulikuwa pale pale, hakutaka nimuoe
mwanae, na alitaka arudishe mahari, kwa kile kitendo cha kusema
“Mtoto wenu hana nidhamu” hata alipoulizwa nidhamu gani alishindwa na kubaki akisema.
“Sitaki
nasema basi. Chukueni hela zenu na ng’ombe zenu nne, sikotayari
kumuozesha mwanangu” Aliendelea kuwa na msimamo wake. Kwa maneno ya mama
yule yalikuwa ni furaha kwangu, kwani ningemkosa basi ningeenda kumuoa
Jennifer na kwa upande mwingine yalinikera sana, hasa alipozidi kusema
sina hadhi ya kumuoa mwanae. Eti nina dharau, nilishindwa kumuelewa
alikuwa na maana gani?.
Baba
na mama yangu walinivuta pembeni na kuzungumza kama dakika takribani
tatu, kisha wakarudi na kuomba waondoke wakayazungumze nyumbani.
Waliondoka wote, baba, mama, mama Getruda na Getruda. Hawakutaka
kuyazungumza pale kwani ilikuwa sio sehemu yake. Tulibaki mimi na mzee
Jophu, lakini sikumuona akiwa na furaha kama nilivyomzoea, hakutaka
kuongea na mimi.
“Boss
mbona unaonekana una hasira nini hasa nilichokukosea. Nimeona
umebadilika” kimya kilitanda sikupata jibu lolote zaidi ya kunitazama na
kuondoka zake.
Kesho
asubuhi nilipowasili kazini, nilifanya kazi vizuri kama kawaida nikiwa
naongea na baba na mama kwenye simu. Mara Boss Mzee Jophu anaingia na
wakati huo nilimaliza maongezi na kukata simu, nilipomsalimia hakuitikia
salamu yangu, bali alinitupia barua mezani, na kusema “Sina shida na
salamu yako. Barua hiyo na unijibu haraka iwezekanavyo.Nakupa nusu saa”
aliondoka na kufunga mlango kwa kishindo kikubwa.
Nilishindwa
kumuelewa, lakini kwa matendo yake nilihisi na kuamini barua ile
ilikuwa ya kufukuzwa kazi, lakini nilishindwa kuelewa kosa hasa lilikuwa
lipi?. Homa ya kufukuzwa kazi ikaniingia, nilishindwa kuisoma ile
barua, niliinamisha kichwa nikiwaza.
“Hivi
kama nitakuwa nimefukuzwa kazi nitaenda wapi? Nitamuonaje Jennifer
tena? Nauli sina ya kwenda Bangkok” Ghafla mawazo yakanijia nilikumbuka
kuwa boss alinipa muda wa nusu saa kuijibu barua yake. Ndipo nilipoanza
kuifungua barua huku mikono na vidole vyote kwa
pamoja vikitetemeka kama mgonjwa wa degedege. Nilifanikiwa kufungua
Barua. Kitu cha kwanza kukutana nacho ni maneno yaliyoandikwa kwa herufi
kubwa.
YAH: UPIMAJI WA AFYA KWA AFISA MAUZO, JOPHU MINING TRANSPORT CO.LTD.
Moyo
wangu ulipasuka kwa furaha “nilihisi ni ridandasi kumbe ni kupima afya
hilo halina shida. Ngoja niendelee kusoma” nilijisemea kimoyomoyo.
HUSIKA
NA KICHWA CHA HABARI HAPO JUU, TUMEPATA BARUA KUWA WAFANYAKAZI WA
KAMPUNI YETU WANAHITAJIKA KUPIMA AFYA ZAO, HASA UKIMWI NA AFISA MAUZO
AWE WA KWANZA . BODI ILIPANGA KIKAO CHA SIRI.
MKURUGENZI WA KAMPUNI
JOPHU KUNDY.
Nilimaliza
kusoma barua, lakini hata hivyo moyoni nilijiuliza “Kwanini Mzee Jophu
na msalimia haniitikii, halafu akanipa barua ya kwenda kupima afya
yangu, au anahisi nina virusi nini?. Ama anataka kunitafutia kosa ili
anifukuze kazi nini?. Kwanini ananikasirikia, ni kwa vile wazazi wangu
wamekuja kuongelea maswala ya kuoa hapa kazini au ni nini?.” Nilizidi
kutumbukia kwenye kisima cha mawazo kem kem, bila kupata jibu muafaka.
Kwa ujumla nilishindwa kuelewa wazo halisi la Boss kunitaka nikapime
afya yangu, na nikiwa mtu wa kwanza kazini kupima virusi na kwa nini
alinikasirikia. Muda niliopewa na Mzee Jophu ulitimia, hakupenda
kupoteza muda, aliingia ofisini kwangu na kuniuliza,
“Sweedy umeisoma barua niliyokupatia?. Naomba majibu. Utaenda kupima au hutakwenda?”
“Nitakwenda boss, lakini kwani ni lazima kupima?”
“Ndio, ni lazima hasa wewe” Mzee Jophu alinijibu kwa uhakika.
“Kwa
nini mimi iwe lazima, asiwe mfanyakazi mwingine. Boss unanitisha sana
hasa unaposema ni lazima mimi, na cha kushangaza boss hutaki kuitikia
salamu zangu. Nimekukosea nini, naomba uniambie, ndipo nami nikujibu
kuhusu jibu la kupima” Niliongea nikilalamika kidhaifu kwa boss,
niliogopa mabadiliko ya boss.
“Ok,
usihofu kuhusu kutoitikia salamu yako. Nilijaribu kukutingisha tu
unajua Sweedy mimi na wewe dam dam. Pia watu wanatufananisha kama mtu na
mdogo wake, wengine wanajua dhahiri kuwa wewe ni mdogo wangu wa toka
nitoke. Nilikuwa nakupima imani yako, hivi wewe hushangai toka nikuajiri
kazi hatujawahi kukasirikiana iwe sasa? Wewe ndiye ninaye kuamini
katika kampuni yangu, hata nikifa leo, wewe ndiye utakaye shikilia mali
mpaka watoto wangu watakapokomaa kiakili. Umenielewa Sweedy? Ondoa shaka
yale yote ni matani.” Mzee Jophu aliamua kuficha ukweli uliopo moyoni mwake,
alinichukia mno! kwa muda mfupi tu toka amuone Getruda, binti mrembo,
hakutaka nijue nini kilichotaka kuendelea, alizidi kunifumba kwa maneno
ya uwongo na kunifanya nimuamini kuliko siku za nyuma.
Nilipandisha
pumzi na kushusha kwa nguvu “oophhhh!” “Ni kweli boss lakini ilinifanya
niwe na alama ya kuuliza ndani ya ubongo wangu, hata hivyo sikuamini
kuwa ni wewe ulinibadilikia kiasi hicho. Kuhusu kupima nani kakupa wazo
hili?”.
“Ok,
swali zuri, nilipata barua kutoka mamlaka ya Uhamiaji, kwamba si ruhusa
mtu kutoka nje ya Nchi bila kupima afya, hivyo wewe kama Afisa mauzo
bila kupima hutaenda Nchini Thailand lakini utakapopima utaendelea na
kazi yako kama kawaida.”
“Hakuna
shida boss mimi nitapima virusi najiamini sina kitu, mimi sio mkware”
Nilimjibu. Furaha yangu nikutaka kwenda nchini Thailand nikaonane na
Jennifer .
“Kesho
asubuhi watakuja Daktari kukutoa damu. Hutaenda huko hospitalini, cheo
chako kinakulinda na sitaki uhangaike. Watakuja na kukupima na wiki ya
tatu utaenda Nchini Thailand kama hutakuwa na virusi. Sio sheria yangu
hapana ni serikali”Akasema Boss akizunguka zunguka pale
ofisini.Alionekana mwenye furahabaada yakukubali kuopimwa.
“Nitakuongezea mshaharaasilimia hamsini wa mwanzoni”Alizidi kunipa motisha.
“Nitafurahi Bossi” .
Tukiwa
kwenye maongezi nilisikia simu ikiita. Nilipoitoa mfukoni niliona namba
za baba juu ya kio cha simu. Niliipokea na kuanza kuongea .
“Shikamoo baba.Mama hajambo?”
“Marahaba!.
Wote wazima wanakusalimu. Jiandae kwa harusi yule mama amekubali umuoe
mwanae. Ni baada ya kwenda kwenye mila na desturi, amepewa faini ya
kutaka kurudisha mahari. Umenielewa mwanangu?”
“Ndio baba. Kweli amekubali nimuoe mwanae?. Hata siamini nitajitahidi kukusanya mchango wa harusi”
“Sawa jitahidi mwanangu” Tulimaliza maongezi na kukata simu.
Nilipomtizama
Mzee Jophu alinitupia macho ya lawama, lakini hata hivyo nilichukulia
usemi wa kupima imani kumbe yeye maneno ya yule mama kukubali nimuoe
mwanae yalimuumiza roho sana, na alikiri kumuua mama Getruda
kwa kumsaliti na kumchukulia laki zake tano, lakini kwa upande wa mama
Getruda hakula wala hakuzitumia hata senti tano yoyote, alipanga
kumrudishia baada ya kushindwa kuzuia ndoa isifanyike.
No comments:
Post a Comment