“Oke nimeamini umeumbika sawa, kama asingekuwa Sweedy basi ningekuoa mimi. Bado sija chelewa. Nina nafasi kubwa ya kukuoa”Huo ndio ulikuwa mwanzo wa usaliti wa ndoa.
“Hata mimi nakiri umbo lako ni zuri na lakuvutia. Najuta kuolewa na huyu mchovu asiye na umuhimu wowote ndani ya ndoa”
Mzee
Jophu alidakia “Ni kweli, sio vyote ving’aavyo dhahabu. Vingine
aluminiamu ama bati,”alitulia kidogo na kumkodolea macho yaliyojaa
ubembe, kisha akanyanyua mkono wa Getruda na kumbusu kiganjani, akakohoa
kidogo na kusema “Sawa, tupange tukutane wapi?”Ilikuwa ni sauti ya
nzito ya Jophu ikinguruma varandani kwangu.
“Mimi
naona tukutane Hoteli yake Sweedy mwenyewe, pale sea breez inn hotel
ili tuwaonyeshe watu na hata wafanyakazi wake kuwa Sweedy ni dhaifu”Mke
wangu alianza dharau akitaka wakutane kwenye hotel yangu, ili kunidhalilisha.
“Kesho
saa kumi jioni, nafikiri utakuwa muda muafaka wa kujipumzisha,”Getruda
alizungumza huku akimtolea Jophu macho ya kurembua na ya unyenyekevu.
“Aaaa!, kesho mbali. Ok kumbe saa hizo karibu giza. Sawa usikose mpenzi”Walipigana mabusu ya kuagana na Mzee Jophu alimalizia .
“Niote njozi njema usiku. Tena zilizo jaa mahaba”
“Usijali mpenzi, zote nzuri zitakuwa juu yako”Mzee Jophu alitoka na mke wangu alirudi na kunifuata kule chumbani, kwa kusema kweli moyo wangu ulipata sononeko la roho, nilibaki nikiyaganga maumivu ya moyoni.
Walipanga
sehemu ya kukutana bila ya kukosa, wote walikuwa na shauku moja.
Ilikuwa jioni tulivu watu walikuwa wana kunywa na kula. Alionekana Mzee
Jophu akiingia na mke wangu SEA BREEZ INN HOTEL. Waliongozana hadi
mapokezi, na kuandika jina la kunikashfu kwenye kitabu cha wageni, bila
aibu mbele ya wafanyakazi wangu. Hata kama walifanya hivyo wasingefanya
kwenye hoteli yangu, wangeenda sehemu wasio julikana.Yote walionifanyia ni kunidhalilisha.
“Jina
tuandike nani Mzee” muhudumu aliongea kwa wasiwasi, baada ya kumwona
mke wangu, ambaye alikuwa kama bosi wake.Mzee Jophu aligeuza shingo
kumtizama Getruda, Kabla hajajibu kitu mke wangu alidakia “Andika Sweedy
dhaifu”
“Hapana bosi, anatakiwa kuandika jina lake kamili .Hilo sio jina kamili” aliongea kwa sauti ya chini huku akitetemeka. Alihisi mawili, kupokea tusi ama kibao.
“Sio jina kamili.Unafahamu jina lake?”
“Sifahamu”
“Kama hufahamu , mbona unasema si jina lake kamili?”Yule kijana akaanza kutizama chini kwa hofu.
“Nimekuambia uandike jina nililokutajia,upesi”
“Mama .Siwezi kuandika jina hilo”
“Wee,
mpumbavu nini!.Nimekuambia andika, kama hutaki huna kazi. Fungasha
virago uondoke,”Getruda alizidi kumuamrisha sambamba na kidole
alichoelekeza jichoni.
Ilimbidi
akubaliane na matakwa ya bosi wake, kwa kuwa hakuwa na sauti na alijua
Getruda ni mke wangu, asingefanya hivyo kibarua kingeota nyasi
haraka.Walichukua chumba, kila aina ya vinywaji viliingizwa
chumbani humo bila ya aibu.Kijana alishindwa kuvumilia yote
aliyoyaona.Aliumia rohoni na kuona kama yaliyotendwa alitendewa
yeye.Hakupenda kuona mke wa tajiri yake akifanya mambo ya kishenzi, tena
ofisini kwake bila aibu.
Chumba
changu kilijaa utulivu uliovunjwa na muziki wa taratibu uliosikika
redioni.Nilikuwa nimejipumzisha kitandani chali, nikiwa nasikilisa
mwambao ambao uliniwezesha kusikia mtu ambaye angeponyeza kitufe cha
kengele getini. Mawazo yangu yalilenga matatizo yaliokabili mwilini
mwangu.Hasa gonjwa ambalo limenifanya nimruhusu mke wangu awe na bosi
wangu. Mara simu ilianza kuita,nilishituka na kutizama mahala
nilipoiweka.Nilipoiona, nikanyoosha mkono kwenye droo ya kitanda na
kuiokota upesi.Sikutizama hata kwenye kioo kuona namba za
aliyepiga,niliipokea mara moja na kuipeleka sikioni.
“Hallo Sweedy hapa. Nani mwenzangu?”
Nilisikia
upande wa pili ukijibu kwa kuhemea juu juu.“Mimi John naongea, Mzee
nimemuona mama amechukua chumba yupo na Mzee mmoja, ameandika jina la
mgeni Sweedy dhaifu” sauti ya John iliingia lakini hata hivyo nilihisi
masikio kuchuja herufi.Nilishituka na kubaki mdomo wazi nikiwa nimetoa
macho kwa mshangaa mkubwa.Nilihisi mapigo ya moyo yakienda kasi zaidi.
“Umesema umemuona mke wangu wapi?”
Sikuamini nilirudia kwa ukali kidogo.
“Hapa hotelini kwako,mzee”
“Khaa,nisubiri nakuja.Wala usiwashitue”
“Sawa,mzee”
Nilikata
simu kwa ghadhabu kali.Sikupenda kupoteza muda, nilichukua bastola na
kuificha kibindoni. Nilifungua mlango kwa upesi na kutoka varandani,
nilionekana kuchanganyikiwa .Nilipofika varandani nikajikuta sikuwa
nimevaa viatu.Ndipo niliporudi kuvaa.Nikiwa nje ya jengo ,nilimpigia
simu dereva wa teksi niliyefahamiana nae aje kunichukua.Haikuchukua muda
, niliona gari jeupe lililo pigwa msitari mweusi katikati likiegeshwa
nje kwangu,nilitambua ni gari la bwana Jangala, yule dereva mashuhuri wa
teksi pale soko kuu Arusha.
“Bw.Jangala naomba unifikishe hotelini kwangu.Nimesahau kidogo,hivi nikiasi gani?”
“Mzee,umsahaulifu kweli.Unaonekana mwenye mawazo mengi.Kutoka hapa njiro mpaka pale Sakina ni sh,elfu tano tu,mzee”
“Hakuna tabu.Washagari twende.Samahani nina haraka,hivyo ikakupasa kutembea mwendo wa kasi”
“Sawa,
mteja kwangu ni mtukufu”Jangala alisema akikanyaga mafuta, wakati huo
gari likizunguka ‘Kiplefti’ ya kwanza kutoka kijenge juu.Nilielekea moja
kwa moja ilikushuhudia uzalilishaji.
“Ama
zangu ama zao, heri niwaue nami nife”Nilitulia kidogo nikitafakari
,nimbinu gani nitumie ilikuwa kuwanasa wote kwa mpigo.Yaani kumkabidhi
Jophu imekuwa nongwa.Ajabu ni kwamba hazijapita hata siku mbili
ananidhalilisha? Kweli rafiki mkia wa fisi.
No comments:
Post a Comment