Mwanaume anaweza kukupenda sana na wewe
ukaona kabisa kuwa anakupenda. Lakini unapaswa kujua kitu kimoja,
wanaume wengi hawaoi kwasababu wanapenda, kwasababu wana pesa na
wanadhani wanaweza kuhudumia familia au kwasababu wanahofia kukupoteza.
Wanaume wengi huoa kwa sababu kuu mbili,
sababu ya kwanza ni ya ngono, kwamba wanaoa kwakua wanataka mtu
wakufanya naye mapenzi kila wakati wanapohitaji. Hii nimeiweka sababu ya
kwanza lakini si sababu kubwa sana kwa wanaume, wanaume wengi huoa kwa
sababu ya kazi za ngumbani.
Hapa nifafanue kidigo na wanawake muwe
makini, wanaume wengi ni wavivu katika kufua, kufanya usafi wanyumba,
kupijka, kuosha vyombo, kutandika kitanda na vitu kama hivyo. Wanapenda
kuona hivyo vitu vinafanyika na wanaamini kuwa wanawake wana nguvu za
ajabu kuvifanya vitu hivyo.
Anaweza kupata ngono sehemu yoyote,
anaweza kuzaa na mwanamke yoyote lakini kama akirudi nyumbani anakutana
na nguo chafu, anakutana na vyombo vya juzi, anakutana na vumbi kila
sehemu na anakila kitu cha kumfanya aoe basi ataoa.
Hii ndiyo maana kama mwanamke
ukijifanyisha mke ukahamia kwake na ukawa unamfanyia yote hayo miaka
itaenda bila ndoa, unamtimizia kila kitu, unamfanyia kila kitu ambacho
angependa mke amfanyie sasa akuoe wanini. Lakini hiyo sio mada yangu ya
leo.
Mada yangu nikuwa unapoingia kwenye ndoa
acha kiburi, eti kwakua una kazi na una kakipato unajifanya hufui,
unajifanya hupiki, eti unataka nayeye asaidie kazi za ndani au
mfanyakazi wa ndani ndiyo afanye kila kitu. Unanunua chakula kila siku
hotelini au kila siku anakula chakula cha house girl!
Nikuambie kitu utaachika au atatafuta
sehemu ambayo anafanyiwa vitu hivyo. Kwa mwanaume mpaka ajihisi mwanaume
nilazima awe na mwanamke wa kumpikia, wakumfulia, wakumfanyia usafi
ndani na vitu kama hivyo usipo vifanya wewe atavitafuta kwa mtu mwingine
kwani ndiyo ambavyo vinamfanya ajihisi mwanaume.
Kama ambavyo wewe ukiwa na mwanaume
ambaye hatoi matumizi na hakuhudumii kwa chochote hujisikii kupendwa
hata kama kitandani shughuli yake ni pevu ndiyo hivyo hivyo kwa
mwanaume. Lazima awe na mtu wa kumuambia kuwa leo nataka kula kitu flani
akatoa pesa na kikapikwa, kama hufanyi hivyo jua kuna anayefanya
kwaajili yako.
Usijifanye uko bize sana, eti kwakua una
mfanyakzi basi unafurahia, eti kwakua na yeye hakuulizi kwanini hupiki
hata mara moja moja, kwanini nguo zake anafua Dada wakazi, kwanini Dada
wakazi anaingia mpaka chumbani na mambo kama hayo.
Usidhani anafurahia, usidhani hapati
wivu pale rafiki zake wanapoongelea kuhusu wake zao kufua na kupika.
Pale rafiki zake wanapowapigia simu wake zao kuwaambia wanataka kula
nini. Namna unavyoumia shoga zako wakisema namna wanavyoletewa zawadi,
namna wanavyohudumiwa ndivyo anavyoumia.
Ukiolewa hata kama wewe nia Raisi jua
kuwa kazi za nyumbani ni zako. Sikwamba ufanye kila kitu bali ufanye
angalau kitu kimoja, mfanyakazi wa ndani asiisngie chumbani kwako au
kufua nguo za mumeo, mpikie mumeo hata mara moja kwa wiki chakula
anachokipenda, hayo ndiyo majukumu ya mke wa mtu.
Usifanye hivyo kama adhabu au kwakuhisi
kama ni kitu cha kukudhalilisha eti kwakuwa na wewe unaingiza pesa, eti
una elimu kuliko yeye, kipato chako ni kikubwa kuliko chake na mambo
kama hayo. Fanya hivyo kwakua wewe ni mke na unajisikia fahari kumfanyia
hivyo.
Kama hujisikii fahari kumpikia mumeo,
hujisikii fahari kumfulia na kutandika kitanda ili akione kisafi basi
jipime, humpendi huyo mwanaume na uko kwenye ndoa kwasababu nyingine
zaidi ya mapenzi. Mwanamke anayependa anajua huo ni wajibu wake na sio
kwamba tu atautimiza bali pia atautimiza kwa mapenzi.
No comments:
Post a Comment