Kama hutajikubali mwenyewe, ukafurahia
muonekanekano wako, ukasema hivi ndiyo nilivyo kama unanipenda twende
kazi na kama hunipendi nipotezee basi hata kama ukipendwa na ulimwengu
mzima haitasaidia kitu. Wanawake tunajali sana kuhusu muonekano, yaani
namna tunavyoonekana kwa watu hasa wapenzi wetu ndiyo kila kitu kwetu.
Tunatumia muda mwingi kujaribu kuuridhisha ulimwengu na namna
tunavyoonekana kuliko kujiridhisha wenyewe.
Nijambo zuri kupendeza kuwa na muonekano
mzuri na kuvutia, lakini kama mwanamke unapaswa kujua nini maana ya
kupendeza, kuwa na muonekano mzuri na kuvutia? Kuwa na matako makubwa
haimaanishi kupendeza, kwa mweupe haimaanishi kupendeza, kuwa mrefu
haimaanishi kupendeza, kuwa na nywele ndefu haimaanishi kupendeza, kuwa
na kucha ndefu haimaanishi kupendeza?.
Kupendeza ni ile hali ya kuufanya
muonekano wako kuwa bora zaidi, kuvaa nguo kutokana na umbo lako, kuwa
msafi na kunukia. Kuwa na muonekano ambao hautakufanya ujihisi vibaya au
kila saa kujishukushuku. Wanawake wengi hasa mabinti siku hizi
wanachanganya vitu wanadhani kujikoboa na kuongezea makalio ndiyo
kupendeza, wanadhani kuvaa nguo fupi na kuka auchi ndiyo kupendeza.
Kupendeza na kuvutia kunaanzia katika
nafsi yako, umepigwa pasi huna tako la mwendo kasi unaangalia na kusema
ni nguo gani nikivaa itanipendeza na itanifanya kuwa comfortable. Yaani
sio unavaa tight za mahips halafu ukitongozwa unaanza kuwaza namna ya
kuivua, sisemi usivae lakini uvae ukiwa unajiamini hata wakati wakuvua
uwe na uwezo wakusema hapa niliongezea ili iendane na nguo flani.
Lakini sio uvae kisketi kifupi halafu
kila saa unaona aibu na kujiona uko uchi, vaa kisketi kifupi kwakua
unapenda na unajiona unapendeza zaidi na si kwakua ulimwengu mzima
unataka uvae hivyo au kwakuwa baby anapenda hivyo, no vaa kinachokufanya
ujisikia vizuri. Jisikie vizuri kuhusu wewe kabla ya kutaka wengine
wafurahie kukuona.
Mungu angejua wanaume wote wanapenda
makalio makubwa angeumba wanawake wenye matako makubwa tu, angejua
wanapenda weupe angeumba wazungu tu lakini anajua kuwa kila mtu anapenda
chake hivyo kama Mungu hajakupa makalio makubwa na akaja mwanaume
anataka makalio ya mwendo kasi muambie Baba umekosea njia humu pasi tu,
kama kifu chako cha mwendo kasi na yeye anataka saa sita muambie
umekosea njia.
Huna haja ya kujibanabana kuweka kila
kitu feki katika mwili wako mpaka ukitoka bafuni anasahau ni mwanamke
gani ameoa. Hambu anza leo, jikubali ulivyo na jipendezeshe kutokana na
muonekano wako, kama marafiki zako hawapendi waambie wakatafute marafiki
wengine kama bwana wako hependi muambie akatafute mwingine kwani
hujajiumba wewe, acha kujionea aibu umzuri hivyo hivyo ulivyo jikubali.
Wengine unakuta ni wake za watu, upo na
mwanaume kakupenda mpaka kakuoa lakini bado huridhiki unadhani labda
umbaya au unajisikia vibaya akiongea na wanawake wengine eti kisa wewe
si mweupe, huna sijui kifua cha namna gani? Kuwa na wasiwasi na
kutokujikubali kutamsukuma kutokukupenda, kama wewe mwenyewe hujipendi
unadhani ni nani atakupenda? Hembu jipende na tambua kua namna ulivyo
ndiyo Mungu alivyotaka.
No comments:
Post a Comment