Wanaume wengi hudhani ni vigumu sana
kuwafurahisha wanawake lakini si hivyo, ni jambo rahisi, matendo yako
kwenye mambo madogo madogo ya kimapenzi na kuchunga ulimi wako vinaweza
kumfanya mwanamke wako kuwa na furaha kupita kiasi na kama yeye akiwa na
furaha basi ndugu yangu maisha yako yatakua na amani na wewe utakua na
furaha.
Kwa kawaida wanaume kuna vitu tunaviona
vya kawaida sana na vya kipuuzi lakini kwa wanawake ni vitu muhimu na
tunatakiwa kuwa makini tunapovizungumzia. Katika kukusaidia tu ndugu
yangu katika mahusiano hapa nimekuandalia mambo matano ambayo unapaswa
kuwa makini unapoyaongelea, hizi ni kauli tano ambazo mwanaume ni dhambi
kabisa kumuambia mwanamke.
(1) Hiyo Nguo imekutoa vizuri imefanya makalio yako yaonekane makubwa;
Ingawa wanwake hupenda sana kusifiwa na kauli yako ilianza vizuri
lakini umemalizia vibaya kumuambia ‘imefanya makalio yako yawe makubwa’
nisawa na kumuambia umepigwa pasi na hata kama hatakujibu utamuumiza
mbaya na kumuondolea kujiamini.
Sio kwamba alikuwa hajui kuwa makalio
yake si ya mwendo kasi lakini kwa kumuambia wewe tena ukasema kapendeza
kwasababu yanaonekana makubwa basi unamuambia kua unapenda makalio
makubwa na kipindi chote hicho mlivyokuwa naye basi ulikua unavumilia tu
na hufurahii. Ndugu yangu katika mahusiano achana na hiyo kauli, ishia
tu kumuambia umependeza basi!
(2) Kweli kabisa anza Diet;
Hapa ni yeye kaja kukuambia kuwa anajihisi mnene na anataka kuanza diet
ili apungue, ndugu yangu acha kujifanya kiherehere kuwa eti kweli
anahitaji kupungua, hata kama unaona anahitaji kupungua mwanangu wewe
sema tu unavutiwa hivyo hivyo na tena ukimshika shika kumuambia ndiyo
unavyopenda mwili unakua na pakushika sio mifupa mitupu.
Akizidi kusisitiza wewe muambie hata
kama anafanya hiyo diet basi asipungue sana. Hapo utakua umemuambia kuwa
unampenda jinsi alivyo na unafurahia vile alivyo. Kumuambia kweli
kabisa unatakiwa kufanya dieti ni sawa na kumuambia kuwa wewe ni mnene
na siku nyingi nilitamani upungue sifurahii kabisa ulivyo. Kuwa makini
na muonekano wa mwanamke, utamnyima raha na akikosa raha hutakuwa na
raha.
(3) Kwanini usiwe kama yule rafiki yako;
Bila kujali unatolea mfano kitu gani lakini kamwe usimsifie rafiki yake
na kumkosoa yeye hata kama ni kwa utani. Usiseme kwanini usingenunua
rangi kama ya flani, au kwanini huwi mpole kama flani na mambo kama
hayo, kutole amfano kuwa anatakiwa kua kama flani inamaana unampenda na
kumfurahia flani kuliko yeye. Hata kama nia yako si hiyo lakini acha
kumlinganisha na rafiki zake au wanawake wengine.
(4) Kweli alipendeza…;
Mmetoka out mlienda kwanye sherehe au sehemu na marafiki zake na wakati
mnarudi au mko nyumbani anaanza kumsifia rafiki yake mmoja alivyokua
kapendeza, ndugu yangu huo ni mtego usiongeze neno hata kama uliona
kweli kapendeza. Kumuambia kweli alipendeza utakua umefanya makosa
matatu, kosa la kwanza ulikuwa unamuangalia sana rafiki yake labda
umemtamani ndiyo maana ulijua kapendeza.
Kosa la pili umemuambia yeye hakupendeza
kwani utakuwa labda ulimlinganisha na kosa la tatu hujali hisia zake
unamuwaza huyo aloambiwa kapendeza. Msikilize tu na kama utachangia sema
tu mbona kawaida tu hata hukuona kipya. Kwanini utafute matatizo ya
bure muhimu ni usiponde sana kwani ukiponda zaidi atastuka unaongea vile
ili kumfurahisha na si kweli, jibu kidogo kama vile hutaki na badilisha
stori mara moja.
(5) Hivi huwezi kunyamaza;
Anaongea sana, analalamika sana lakini hupaswi kumuambia kua anaongea
au kulalamika sana kwani utamfanya azidi kuongea sana na kulalamika kuwa
unamuambia anaongea na kulalamika sana. Najua ushachanganyikiwa zaidi
lakini ndivyo wanawake walivyo, hutoa stress zao kwa kuongea, ni njia ya
kujitetea ni silaha ya mapambano kwao.
Kwa maana hiyo hata kama anaongea sana
analalmika sana wewe umilia au jaribu kuzidi kumuonyesha mapenzi.
Kulalamika kuwa anaonge ana kulalamika sana utampa kitu kingine cha
kulalamika na utazidi kuchanganyikiwa zaidi kwani haitasaidia
kumnyamazisha. Nikazi ya mwanaume kumpenda mwanamke bila kuuliza au
kutaka kujua kwanini anampenda na wala usitake kumuelewa kwani kamwe
hutamuelewa wewe mpende tu.
No comments:
Post a Comment